Unavoidable Servant
JF-Expert Member
- Oct 13, 2021
- 1,728
- 4,545
Tangu lini ccm inahitaji kura ya mtu kushinda uchaguzi?Nawasalimu Kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huu ni uchambuzi mfupi tu wa "facts".
1. Samia alikuwa makamu wa Rais WA Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dr JPJM. 2015-2020.
2. Magufuli alikuja kuliokoa jahazi lililokuwa linazama mikononi mwa Kikwete.
3. Magufuli alikuwa kiungo muhimu sana aliyeifufua CCM ambayo ilikuwa imejifia kwenye UFISADI, UDHAIFU na MAUCHAFU ya kila aina. Hata watu waliokuwa wanavaa manguo ya kijani walipigwa mawe.
4. Wakati wa Magufuli, CCM iliimarika na kustawi. Hata vijana wakapata hamasa ya kuishabikia.
5. Hayo yote yalifanyika kwa sababu, kwanza Magufuli alikuwa si mwanasiasa wa maneno maneno. Utendaji wake wa miaka mitano unajidhihirisha.
6. Samia hakuwahi kuwa na mvuto wa Kisiasa wakati wa Magufuli. Alibebwa bebwa tu. Hata watu wengi hawakumjua wala kumtilia maanani.
7. Samia sio president material. Hana ushawishi wa maneno wala wa vitendo. Hata akisimama jukwaani hana nguvu ya kisiasa.
7) (a) Hawezi kujipambanua kisiasa. Akigombea atafeli kabla hajaanza (isipokuwa tu labda kwa usaidizi wa state apparatus).
b) Hawezi kupambana katika ulingo wa Kisiasa. Ni mchovu.
c) Hana ushawishi kwa wananchi. Ushawishi ni karama ambayo hana. Hana kismati. (labda atumie uchawi na mapete ya kiganga).
d) Ameshawavuruga watu makundi kwa makundi (wamachinga, mamantilie, vijana, TOZO, Bandari ya bagamoyo, Bwawa la Nyerere, mgao wa umeme, maji pamoja na kurudisha mafisadi serikalini). Hili ni doa.
NB: CCM wakitaka waaibike 2025 wamuweke huyu mama. Watapata aibu ya karne.
Lisukuma gang wahed jinga kabisa.