Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

Wakati wa mwendazake CCM yote ilikuwa inategemea kichwa kimoja tu kufanya maamzi na ilikuwa no kosa la jinai kumkosoa mwenyekiti kwa hiyo ulihitajika unafiki was kiwango cha kujipendekeza tu ili Mambo yako yaende
Ilikuwa ni rahisi kumkosoa Mungu na ukaishi kuliko kiumbe kilichozaliwa na mwanadamu usilione jua RIP Ben,lwajaba,Azore,and others.
 
Baraza la Madiwani Geita limeukataa Mkoa wa Chato, je JPM angekuepo wangeweza kukataa hiki kitu!! CCM wakikusifia au wakikubaliana na wewe ujue wana maslahi au ni Unafiki tu.

Wanajitahidi kufuta Legacy ya Shujaa wetu! Sio sahihi Hata kidogo.

View attachment 1799934
kipindi cha mwendazake hii habari isngeripotiwa, wangefukuzwa wote udiwani na wangepewa armed robbery na uhujumu uchumi.
 
Watu wana akili finyu sana!?
what is the big deal kwa sehemu kuwa mkoa!!?
zaidi ni kusogeza huduma kwa jamii
 
JPM alikuwa ni muona mbaaali Sana, watu wenye mawazo mafupi, baada ya miaka michache ijayo, watakuwa wamejielewa ujinga wao, Mimi Naamini Leo wameukataa mkoa wa Chatto, lkn miaka ijayo, Chatto itakuwa mkoa tuu
 
ni ufujaji wa fedha za umma kufikiria kwa sasa kuanzisha Mkoa, nchi ambayo watu wake walio wengi bado wanaishi ktk dimbwi la umasikini halafu viongozi wake wanakaa na kufikiria jinsi ya kuongeza gharama za uendeshaji wa Serikali!!!! ili tu baadhi yao wanufaike!!!!

Hapana tuwe na huruma kwa wananchi wetu ambao bado hatuja wagomboa kutoka ktk dimbwi la umasikini,

Tunaiomba sana tena sana Serikali ya Rais Samia Suluhu iendelee kubana na KUDHIBITI matumizi ya serikali, kusiibuke matumizi holela kwa kuanzisha au hata kuajiri lundo la watumishi kwa mkupuo kama tulivyoona siku za hivi karibuni wakati uwezo wa fedha bado mdogo kuwahudumia, ni gharama kubwa sana kwa taifa letu ambalo kimsingi bado tuna chechemea.
 
Baraza la Madiwani Geita limeukataa Mkoa wa Chato, je JPM angekuepo wangeweza kukataa hiki kitu!! CCM wakikusifia au wakikubaliana na wewe ujue wana maslahi au ni Unafiki tu.

Wanajitahidi kufuta Legacy ya Shujaa wetu! Sio sahihi Hata kidogo.

View attachment 1799934
Mtu yule angekuwepo madiwani wote wangeuwawa.
 
Back
Top Bottom