PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
"Maandamano yawe ya AMANI". "Mtu akitaka kuchoma property adhibitiwe papo hapo".

Napigilia msumari kwenye kariri hizo. Hiyo ndio iwe kauli mbiu za maandamano. Tusitoe kisingizio kwa Serikali kupambana na waandamanaji. Hata kama nyumbani kwako una silaha, iache nyumbani unapokuja kwenye maandamano. Sisi raia hatuwezi kuishinda Serikali kwa kutumia silaha. Uzuri ni kwamba ulimwengu uliona yaliyotokea tarehe 29 Oktoba na sijasikia hata chombo kimoja cha kimataifa au nchi moja iliyosifia yaliyofanywa na Serikali yetu. Kwa hiyo tutakuwa tunaungwa mkono na kila mtu ambaye hajajizima data. Maandamano hayo yatakuwa pia kuwaenzi waliouawa au kujeruhiwa tarehe 29 Oktoba. Damu yao isiwe imemwagika bure.

Naunga mkono hoja kwa asilimia 101. Aluta continua.
 
Habari zenu wakuu!!
Ukweli ni kwamba maandamano ya october 29 yameonyesha mwongozo kwamba watanzania tunaweza na sio waoga kama wengi wanavyodai .

Haya yajayo ya tarehe 9 december siku ya kumbukizi ya uhuru wa nchi yetu ya Tanganyika tudhamilie kuyafanya yawe ni maandamano ambayo hayajawai tokeo kwa nchi yoyote ile dunia yakawe ni non stop mpaka CCM iachie nchi rasmi hakuna kurudi nyuma na wala tusitegemee jeshi letu hili la ulinzi .

Watanzania tutoke kwa wingi Gen z sana sana kwa wingi acha hawa wazee wa CCM baby boomers wabakie nyumbani na wajukuu.
 
Kinumbo, swali lako halina tija kwa sasa. Tuzingatie tu tuendapo. Huenda Mbaga JR aliona fikra zake zilikuwa sahihi wakati huo. Sasa amebadilisha mawazo kwa sababu yo yote ile. Kama ameongoka na anataka kuja upande wetu, tumpokee tu na kuongeza nguvu zetu. Hakuna tija kumdadisi ilikuwaje.
 
Sawa kabisa.
 
Ni vyema mkafanya kwa Amani na Kulinda Mali za Watanzania wenzenu, Chadema waliwahi kuandamana Miaka ya Karibuni kwa Amani bila kuiba wala kuharibu mali za Watanzania Wenzao. Mbinu ya kwanza ya kufanikiwa ni kulinda Mali ili wasipate sababu ya kuua watu. Mbinu ya pili ni Idadi. Kama watu wakiwa wengi kiasi cha kuasili mizunguko ya shughuli za kawaida mjini bila Vurugu. Lengo linaweza kutimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ