Kama umeuliwa kaka, dada, mama, mjomba, shangazi, rafiki, baba, ndugu na jamaa, je uko tayari kuandamana kupigania haki yako uliyenusurika kuuliwa? Uko tayari kupigania haki ya aliyeuliwa? Au utasaliti damu ya waliouliwa?
Je wewe ambaye hukuguswa na msiba, ila kanisa lako limefungwa, je uko tayari kuandamana kwa amani kwa ajili ya haki yako ya kusali?
Je wewe unayejiita mzalendo, unakerwa na vita inayopelekwa vyama vya siasa vya upinzani, uko tayari kuandamana kwa ajili ya haki zako za kisiasa?
Je wewe unayempenda Tundu Lissu, taarifa ni kwamba wamepanga kutumia mahakama kumfunga jela, je uko tayari kuandamana kwa amani kwa ajili ya haki ya Tundu Lissu?
Je wewe ambaye unajinasibu ni mzalendo unayempenda Mh Polepole, je uko tayari kuandamana kwa ajili ya haki ya uhai ya Mh Polepole?
Wewe ambaye unajiita mu RC wa kindakindaki, ulimiumizwa na jaribio la Padre Kitima kuuwawa, ukaumizwa na matukio ya utekaji wa viongozi wako, umeumizwa na tukio la kanisa kudhalilishwa, kufedheshwa, upo tayari kuandamana kwa amani kudai haki yako ya kiimani?
Je wewe mzalendo unayeumizwa na maisha duni ya Watanzania huku ukiona watoto wa watesi wetu wakiendesha magari ya thamani na matumizi mabaya ya fedha za Watanzania, upo tayari kupambania haki za walala hoi?
Je wewe mzalendo uko tayari kusimama kudai katiba mpya?
Mzalendo wewe, uko tayari kuhesabiwa kudai mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi ili upate kiongozi umpendaye?
Nakuuliza wewe kijana ambaye huna ajira, kesho yako huijui, wenye mamlaka hawana majibu ya maswali yako, uko tayari kuandamana kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi yako ili zikusaidie?
Tunakubaliana kwamba ndugu zetu wameuliwa, vichwa vimepasuliwa, ubongo umemwagika, mioyo imepasuka, mapafu yao yalitobolewa kwa risasi, utumbo na maini yao vilichinjwa chinjwa kwa risasi. Upo tayari kuisaliti damu ya walolala? Au upo tayari kusimama na damu hiyo?
Inawezekana swali letu likawa moja, je damu za wapendwa wetu waliouliwa kinyama, bado miili yao imetokomezwa kwa kuchomwa moto, imezikwa kinyemela, tutausahau ukweli huo kama ambavyo wauaji wetu hudai “Watanzania ni mang’ombe”?
Ni matumaini yangu, kila kijana, kila aloguswa na mauaji haya anao wajibu.
Silaha yetu pekee ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa mkosoaji wa maovu yanayofanywa na hawa wauaji wetu. Kwa kufanya hivyo wataamua wao wenyewe wauwe Watanzania wote au wawaache wote.
Kijana, kijana, kijana, amka. Usiwe mjinga na mpumbavu.
Tarehe 9/12 tushiriki katika maandamano ya amani. Tutoke wote, tupaze sauti kubwa dunia yote, malaika na Mungu wapate kutusikia.
Kataa, kataa, kataa habari za kipuuzi za maridhiano. Hakuna maridhiano katika huzuni, hakuna maridhiano wakati ambao ndugu zetu wameuliwa kinyama na kwa kisasi.
Kataa, kataa, kataa. Usishiriki dhambi kijana, kataa.