Gen z mexico tayari wamesha angusha serikali ndani ya siku moja na sisi tunatakiwa kuthibiti ikulu na bunge basi sio kuzunguka tu barabarani.
=====================
Maelfu ya watu wamejitokeza mitaani nchini Mexico kupaza sauti dhidi ya ongezeko la uhalifu, ufisadi na ukosefu wa uwajibikaji. Maandamano hayo yaliandaliwa na vijana wa kizazi cha Gen Z lakini yakavutia washiriki wa rika mbalimbali, wakiwemo wanaharakati wakongwe wa vyama vya upinzani pamoja na wafuasi wa aliyekuwa Meya wa Michoacan, Carlos Manzo, ambaye alipigwa risasi na kuuawa katika tukio la umma la Siku ya Wafu mapema mwezi huu.
Huko Mexico City, kundi dogo la waandamanaji waliokuwa wamefunika nyuso zao walivunja uzio uliokuwa umezunguka Ikulu ya Taifa ambako anaishi Rais Claudia Sheinbaum. Tukio hilo lilisababisha makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia ambao walitumia gesi ya machozi kulingana na taarifa za vyombo vya habari.
Waziri wa Usalama wa Umma wa jiji hilo, Pablo Vazquez, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa polisi 100 walijeruhiwa, huku 40 kati yao wakihitaji matibabu hospitalini.
Aidha, wananchi 20 nao walipata majeraha, Vazquez aliambia kituo cha habari cha Milenio.
Aliongeza kuwa watu 20 walikamatwa na wengine 20 wakachukuliwa kwa makosa ya kiutawala.
---------------------------
Thousands of people have rallied across Mexico, protesting against growing crime, corruption and impunity, in demonstrations that were organised by members of Generation Z.
The marches on Saturday were attended by people from several age groups, including older activists from opposition parties, as well as supporters of the slain Michoacan Mayor Carlos Manzo, who was who was shot dead at a public Day of the Dead event earlier this month.
In Mexico City, a small group of hooded protesters tore down fences around the National Palace where President Claudia Sheinbaum lives, prompting a clash with riot police who deployed tear gas, according to media reports.
Mexico City’s public safety secretary, Pablo Vazquez, said in a news conference that 100 police officers were injured, including 40 who required hospital treatment.
Another 20 civilians were also injured, Vazquez told local media outlet Milenio.
The public safety secretary also said 20 people were arrested and another 20 “referred for administrative offences”
Source: Al Jzeera