GEN Z ya Tanzania tuna akili sana

GEN Z ya Tanzania tuna akili sana

Yaani katika kitu nimewakubali gen z ya Tanzania ni kutokuandamana sababu kuna mizee ambayo ujanani kwao ilichezea pesa Sasa hivi maisha Yao magumu yanaanza kushawishi vijana eti waandamane hivi jamani Kwa akili ya kawaida yaani kijana afe azikwe aoze halafu lizee liishi liponde raha Kwa damu ya kijana iliyomwagika hii ni akili au matope.

Yaani enzi zao yalizubaa nchi ikaliwa na Nyerere wakabaki kuchekacheka tu kumbe Nyerere alikua tapeli namba Moja halafu nashangaa watu wanakalia kumuita mtu tapeli kama Nyerere eti baba wa Taifa hii kauli inanikeraga sana. Nyerere ndio mwanzo wa maisha mabovu ya watanzania ila mizee ilishindwa kumuambia ukweli Leo hii inasema vijana tuandamane nasema hapa haandamani mtu mpaka mfe na njaa nyie wazee.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kenya ni nchi ya kiafrika ambayo imekaribia demokrasia ya kweli kwa muda mrefu, kwa mtazamo wangu....

Au ni kwa vile muanzilishi wa hiyo nchi hakuamini kabisa kwenye ujamaa

Watu wanaongea wazi kuhusu mambo nyeti, na inachukuliwa kawaida. Kuna chama cha wapinga dini kule, mahakama kuu ilitangaza lgbtq wanaweza kuwa na chama chao cha NGO, Kenya ni kama uzunguni flani😅

Watanzania wana haki ya kuandamana, shida wanazo, ila sasa hawajazoea kwasababu ya jinsi serikali inavyochukulia ukosoaji na jinsi inavyobana uhuru wa watu

CCM ikiona mnaandamana itachomeka mtu huko ndani awavuruge
 
Wewe ni dogo sana, hata huu uhuru wa kuandika utumbo wako hapa, kuna watu walioupigania,

Tuliokuwepo enzi Nyerere, Redio moja na magazeti ya serikali tu, ndio tunajua Hali ilikuwaje,

Kuna watu waliwekwa kizuizini ndio ukapata nafasi ya kuandika huu utumbo,

Naudia Tena punguza kiherehere,
Mbona mashambulizi kwa Paul15 Mgoshii.
 
Nyerere alikua tapeli namba Moja halafu nashangaa watu wanakalia kumuita mtu tapeli kama Nyerere eti baba wa Taifa hii kauli inanikeraga sana. Nyerere ndio mwanzo wa maisha mabovu ya watanzania ila mizee ilishindwa kumuambia ukweli
Tom Mboya wa Kenya aliwahi kusema ujamaa wa ni 'euphemism for laziness' yaani 'tafsida ya uvivu'

Alijua katiba inampa nguvu nyingi raisi ila hakurekebisha

Alikataa wazo la Kwameh Nkrumah kuunganisha Africa nzima

Alifeli sehemu nyingi
 
Pension zao mmegawana sasa nani wa kulaumiwa hapo
Wapeni hela zao wazee na muache kuwaomba ooh nikufanyie chap chap nipe 10m
10m ya nyko
Hakuna cha Gen z wala A
Nyerere hakuwa mwema ila hakuuza madini yote zaidi ya Mwadui akabakiza 3%
Sasa nyie mnaiga jina la Gen Z mko confused 😕 hamjui muandamane kwa lipi

Wenu mstaafu mtarajiwa
Ila zangu napata zote na saving juu 😄
 
Yaani katika kitu nimewakubali gen z ya Tanzania ni kutokuandamana sababu kuna mizee ambayo ujanani kwao ilichezea pesa Sasa hivi maisha Yao magumu yanaanza kushawishi vijana eti waandamane hivi jamani Kwa akili ya kawaida yaani kijana afe azikwe aoze halafu lizee liishi liponde raha Kwa damu ya kijana iliyomwagika hii ni akili au matope.

Yaani enzi zao yalizubaa nchi ikaliwa na Nyerere wakabaki kuchekacheka tu kumbe Nyerere alikua tapeli namba Moja halafu nashangaa watu wanakalia kumuita mtu tapeli kama Nyerere eti baba wa Taifa hii kauli inanikeraga sana. Nyerere ndio mwanzo wa maisha mabovu ya watanzania ila mizee ilishindwa kumuambia ukweli Leo hii inasema vijana tuandamane nasema hapa haandamani mtu mpaka mfe na njaa nyie wazee.
Nyerere amekufa mwaka 1999, hadi sasa ni miaka 25, robo ya karne bado wapumbavu wanalaumu kufeli kwao kwa kumsingizia Nyerere.

Mnaropoka tu ila hamujui mnachoandika. Hivi mnajuwa kuwa Nyerere alizuia kuchimbwa madini kwenye migodi kwa sababu miaka ya 1960-80s nchi haikuwa na wasomi? Kuna maeneo kama North mara aliweka kambi ya JKT ya Buhemba ili watu wasichimbe.

Alisema kama sisi hatuna uwezo wa kuchumba, tusubiri kizazi kijacho kije kipate elimu ndipo tuanze exploration. Na uchimbaji madini ulianza mwaka 1997 wakati wa Mkapa na mpaka sasa madini yaliyochimbwa hayafiki 5% ya yaliyopo chini ya ardhi.

Sasa mnamlaumu Nyerere kwa kitu gani wakati aliwawekea akiba ya raslimali??
 
Uzi wako wa jana nilikuunga mkono lakini wa leo🚮
Wewe sio Gen Z! Ni m'baba mwenye kitambi fisadi lililokubuu unakula kodi zetu kutwa! au ni Chawa uliyepewa buku 7 kuanzisha kampeni ya kutupumbaza Gen Z wa Tz

Muda utafika waliokufa watafufuka.
Njaa yake inampa hasira na kaamua kuimaliza kwa kuja na uzi wa kumlaumu Nyerere aliyekufa 1999.
 
Nyerere amekufa mwaka 1999, hadi sasa ni miaka 25, robo ya karne bado wapumbavu wanalaumu kufeli kwao kwa kumsingizia Nyerere.

Mnaropoka tu ila hamujui mnachoandika. Hivi mnajuwa kuwa Nyerere alizuia kuchimbwa madini kwenye migodi kwa sababu miaka ya 1960-80s nchi haikuwa na wasomi? Kuna maeneo kama North mara aliweka kambi ya JKT ya Buhemba ili watu wasichimbe.

Alisema kama sisi hatuna uwezo wa kuchumba, tusubiri kizazi kijacho kije kipate elimu ndipo tuanze exploration. Na uchimbaji madini ulianza mwaka 1997 wakati wa Mkapa na mpaka sasa madini yaliyochimbwa hayafiki 5% ya yaliyopo chini ya ardhi.

Sasa mnamlaumu Nyerere kwa kitu gani wakati aliwawekea akiba ya raslimali??
Mtoto mdogo huyu maziwa mdomoni, akili zao ndio hizi.
 
Back
Top Bottom