WATU WA MJINI HAWANA MSIMAMO KAMA WATU WA NYIKANI
Gen Z imeanza nyikani Ngorongoro watu wa mjini wameshindwa kuipa mbinyo serikali ya chama dola kongwe uliyopo madarakani kwa miaka zaidi ya 60
WATU WA NYIKANI NGORONGORO WATOA TAMKO ZITO LA KARNE TAREHE 22 AGOSTI 2024 KWA SERIKALI "TUMECHOKA, KESHO TUNAINGIA BARABARANI"
View: https://m.youtube.com/watch?v=pQJZG68rzEw
Ila sauti ya kutoka nyikani Ngorongoro imefanya serikali ya CCM kwa mara ya kwanza kuingia woga na kufuta sheria ya kufuta vijiji, ila mjini mnakaribishwa ktk maandamano hamjitokezi
Watu wa mjini mliambiwa muhamie Burundi kama tozo hazitaki, mkagwaya na kuishia mitandaoni tu.
Leo kina Lukuvi, Prof. Kabudi imebidi waende wenyewe kuomba msamaha na kufuta udhalimu wa sheria ya kupora ardhi za wenyeji wa nyikani nyanda za juu kaskazini huko Ngorongoro Arusha
Watu wa mijini wanadharaulika na CCM maana baada ya maandamano mijini wanakwenda kulala majumbani mwao kwa kupenda vitanda vyao kuliko kupigana haki zao za kiraia, kikatiba, dai la kutaka kodi zao sistumike kifahari kwa kununua magari ya fahari kwa viongozi n.k wanaomba kama hisani wakati Prof. Kabudi kakiri leo akiwa nyikani Ngorongoro kuwa mamlaka ya wananchi kwa katiba ndiyo yanayoamua hatima yao na siyo serikali.
Lakini watu wa mjini mamlaka hayo wameyakabidhi serikali na kubaki kulialia bila kuchukua hatua za kikatiba ikiwemo maandamano yasiyo na kikomo, au kujikusanya ktk eneo maalum kwa siku kadhaa kuonesha kukakataa sheria mbovu n.k