GEN Z ya Tanzania tuna akili sana

🤣🤣🤣
 
Uzi wako wa jana nilikuunga mkono lakini wa leo🚮
Wewe sio Gen Z! Ni m'baba mwenye kitambi fisadi lililokubuu unakula kodi zetu kutwa! au ni Chawa uliyepewa buku 7 kuanzisha kampeni ya kutupumbaza Gen Z wa Tz

Muda utafika waliokufa watafufuka.
Leo nimekupenda bure
 
Kila nchi na majira yake, kila jambo na wakati wake, kila uovu ni zao la mbegu flani ya uovu iliyopandwa kwa mda mrefu. Mataifa huwa yanaqnguka pale mihimili yake inalega kwa sababu ya kutokutoa haki.
Maandamano ya kenye ni matokea ya hali uovu ambao hakuna aliyejali kuukabili sio jambo la siku moja , finance bill ilitumika tu kama trigger.
Kwa Tanzania haya ya kenye ni leaning point, ni fursa ya kujitafakari na kumisha zaidi misingi ya haki ambayo huzaa umoja, amani, uzalendo na upendo pia.
 
Hamna kitu kama hicho kitakachokuja kutokea tanzania Kila mtu apambane na maisha yake
 
WATU WA MJINI HAWANA MSIMAMO KAMA WATU WA NYIKANI

Gen Z imeanza nyikani Ngorongoro watu wa mjini wameshindwa kuipa mbinyo serikali ya chama dola kongwe uliyopo madarakani kwa miaka zaidi ya 60

WATU WA NYIKANI NGORONGORO WATOA TAMKO ZITO LA KARNE TAREHE 22 AGOSTI 2024 KWA SERIKALI "TUMECHOKA, KESHO TUNAINGIA BARABARANI"

View: https://m.youtube.com/watch?v=pQJZG68rzEw
Ila sauti ya kutoka nyikani Ngorongoro imefanya serikali ya CCM kwa mara ya kwanza kuingia woga na kufuta sheria ya kufuta vijiji, ila mjini mnakaribishwa ktk maandamano hamjitokezi

Watu wa mjini mliambiwa muhamie Burundi kama tozo hazitaki, mkagwaya na kuishia mitandaoni tu.

Leo kina Lukuvi, Prof. Kabudi imebidi waende wenyewe kuomba msamaha na kufuta udhalimu wa sheria ya kupora ardhi za wenyeji wa nyikani nyanda za juu kaskazini huko Ngorongoro Arusha




Watu wa mijini wanadharaulika na CCM maana baada ya maandamano mijini wanakwenda kulala majumbani mwao kwa kupenda vitanda vyao kuliko kupigana haki zao za kiraia, kikatiba, dai la kutaka kodi zao sistumike kifahari kwa kununua magari ya fahari kwa viongozi n.k wanaomba kama hisani wakati Prof. Kabudi kakiri leo akiwa nyikani Ngorongoro kuwa mamlaka ya wananchi kwa katiba ndiyo yanayoamua hatima yao na siyo serikali.


Lakini watu wa mjini mamlaka hayo wameyakabidhi serikali na kubaki kulialia bila kuchukua hatua za kikatiba ikiwemo maandamano yasiyo na kikomo, au kujikusanya ktk eneo maalum kwa siku kadhaa kuonesha kukakataa sheria mbovu n.k
 
WATU WA MJINI WAKIANDAMANA
Kisha wanakwenda kulala, wanapiga kura kisha wanaachia makada wa,CCM wahesabu kura zao wao wanaenda kulala ktk vitanda vyao n.k Yaani udhaifu wa watu wa mjini ni tofauti na watu wa nyikani kama Ngorongoro

PICHA MAKTABA WATU NA MATEMBEZI YA MABANGO, MAANA HAYA SIYO MAANDAMANO
 
NYOMI ZA DERBY YA YANGA NA SIMBA


Watakuambia siasa haiwahusu, wao siku nzima, wiki yote, miezi kadhaa mfululizo wa kifua na pumzi ya kubishana nani zaidi na kufurahi pesa za magoli ya rais wanapocheza kimataifa


Lakini hawawezi kudai huduma za maji safi ya bomba, hospitali zenye wafanyakazi, madawa na vifaa tiba kwa kuwa wanalipa kodi lakini 'wajanja' hawa wa mjini huduma hizo hawapati, wanaona hayawahusu ...

Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Luhanga Mpina CHADEMA, TLS ,n.k wanawapigabia ila ni watu wa nyikani kama Ngorongoro ndiyo wanaelea somo watu wa mjini hawajitokezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…