General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Kati ya mwaka 1997 - 2005 General Tyre ilikuwa ikilipa VAT Tsh 375,000,000/= hadi 500,000,000/= kwa mwezi.Nikija kwenye kodi zingine ndio utashangaa hawa viongozi wanaolilia madaraka hadi kufikiwa kuwanunua wachungaji na masheikh huku wakiwahawezi kutawala hata kuku ndio nashindwa kuelewa Tanzania tuna laana ya nani.
Utasikia chama chajenga nchi wakati wao ndio waliacha mambo mazuri ya awamu ya kwanza yateketee.
 
"NSSF ikatoa mkopo wa dola 10 milion Serikali ikiwa mdhamini wa mkopo huo. Badala ya kununua mitambo mipya mitambo ya zamani ikapakwa rangi na fedha zote zikatokomea. Utashangaa leo unaambiwa deni la Taifa linazidi kuongezeka ukichunguza utakuta linaongezeka kwa mambo kama haya". Wakati mwingine matatizo ya africa yanachangiwa na waafrika wenyewe na si kweli kama tulivyoaminishwa kwenye somo la historia kwamba wakoloni ndio walitifanya maskini,Mkoloni mweusi ni mbaya kuliko mkoloni mweupe.
Na sasa NSSF upatikanaji wa mafao unawekewa masharti mengi sana ili kufidia ulaji kama huu
 
Hivi ule mpango wa kukifufua hiki kiwanda cha general tyre imeshindikana? Hii ni awamu ya viwanda kwa nn hilo licfanyiwe kazi. Tunaletewa matairi mabovu toka China.

Mi naomba kwa mheshimiwa Rais ajitahidi kujenga kiwanda cha matairi ya magari na pikipiki. Hii hudums ni muhimu na watumiaji ni wengi sasa hivi ndani ya nchi ye2.
 
Ngoja tuwape miaka mingine mitano CCM, pengine wataweza kukifufua
 
Back
Top Bottom