George Simbachawene ni nani hasa?

George Simbachawene ni nani hasa?

Mzee simuelewagi vizuri, wakati mwingine anaonekana mwema wakati mwingine kama vile hana analojua, ila yupo composed....Nilifanya naye kazi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga nika m define vibaya sana kuna namna alinikwaza katika ujenzi wa nyumba za wakimbizi wale wa Chogo. Lakini ipo siku kuna ndugu yangu alikamatwa na mpambe wa JPM, very recent kabla ya umauti wa JPM, yeye ndiye aliyemtoa kwenye ile kadhia nikamwona ana busara sana....Any way Salute mzee!
Jina lake la kati ni Huruma na ndivyo alivyo si mtu mwenye roho ya kwanini.

Hushiriki ibada pale St Albans kwa miaka mingi sana na ni mcha Mungu.

Mimi namfahamu kwa kukutana nae pale St Albans.

Sehemu kubwa ya waasisi (establishment) husali makanisa ya St Albans, St Joseph na Azania (mzee Lowasa &).
 
Miaka alokuwa pale UDSM.
Aiseee! Basi Magu na ubabe wake hajawahi isema hii kitu! Na kama aliwahi isema basi ni siri mno!

Ni sawa na kwamba Magu kaanza kuumwa tatizo la moyo toka akiwa UDSM, hadi tangazo lake lakuomba msaada lilitolewa, akiwa UDSM! Lakini akiwa Rais hakuna mtu aliwahi hoji au uliza! Alipofariki tu! Watu wakalitoa lile tangazo
 
Aiseee! Basi Magu na ubabe wake hajawahi isema hii kitu! Na kama aliwahi isema basi ni siri mno!

Ni sawa na kwamba Magu kaanza kuumwa tatizo la moyo toka akiwa UDSM, hadi tangazo lake lakuomba msaada lilitolewa, akiwa UDSM! Lakini akiwa Rais hakuna mtu aliwahi hoji au uliza! Alipofariki tu! Watu wakalitoa lile tangazo
Ni kwamba hufuatilii tu lakini JPM alilisema hili la kuendesha Taxi akiwa UDSM alipokuwa akifungua Kijazi interchange mwezi February 2021.

Na alisema alikuwa akifanya hivyo kufatuta "disposable income" na kituo chake kilikuwa ni Ubungo.

Nafikiri ilikuwa ni ziara yake ya siku tatu na ya mwisho jiji Dar kabla hajafariki.
 
Hamumjui vizuri huyo mzee... ni mkali vibaya mno na ni kauzu ile mbaya!

Picha linaanza yuko vizuri financially na hakuna mtoto wake yoyote aliyesoma nje ya nchi na yuko strictly vibaya mno kwenye malezi ya watoto.

Ni wakubwa serikalini hao, wale watiifu na wanaojituma + wachapakazi na wanajitambua.


Huwa hapendi Kiki za kijinga na za kishamba. Yuko kwenye orodha ya marais wajao miaka mingi ijayo... anaandaliwa nafkiri.


Ana mwanae wa kiume anaitwa "James Simbachawene" naona huyu kijana alikata kamba, kunyoanyoa vipanki na kuvaa visuruali vya kubana... kalisoma chuo cha usimamizi wa fedha haka kakijana. Kanajaribu kujifanya kahuni na kablazameni ila nafkiri mzee anapambana kukazaba kaache ujinga wake kawe kakijana smart kafuate nyayo za baba.

KONGOLE KWAKO MZEE SIMBACHAWENE 👍🏾
 
NI mmoja ya mawaziri waliodumu katika Baraza la Mawaziri tangu awamu ya JK, Magufuli na sasa Mama, pamoja na panga pangua za baraza la mawaziri

View attachment 2551539

Na ameshapewa majukumu Wizara ya Utumishi , Wizara Mambo ya ndani, Waziri ofisi ya Waziri. Moja ya Wizara ziliozokaribu kiutendaji na Ikulu

Ni nani hasa? Safari yake ya kisiasa na utumishi serikalini ikoje? Najua kama binadamu hakosi mapungufu lakini anaonekana ni mtu mtaratibu, hekima na busa nyingi mbali ya kuonekana kuwa na elimu ya kawaida.

Bila shaka inahitaji Uzalendo usio na mashaka kusurvive mabaraza ya marais watatu
Huyu kimaadili ya uongozi na ubinadamu wake huwa namfananisha na mjukuu wangu Mizengo Kayanza Peter Pinda. Hawa watu wakati mwingine unasema pengine walikosea kuingia kwenye Siasa ila walitakiwa wawe viongozi kwenye nyumba zetu za Ibada. Yaani wako kwenye level ile ambayo binadamu wa kawaida kabisa aliyeumbwa na Mungu, anatakiwa kuwa.

Una jicho kali, angalau na wewe umeliona hilo. Huyu mtu mimi pia nampenda sana
 
Huyu jamaa kwa ndumba yuko vizur sana nlishapewa na mtu anayekaa jiran yake Kinyerezi mtaa wa Zimbiri jamaa analeta Makalumanzila Mchana Kweupe wamepiga makaniki yao meusi wanafanya yao bila stress
Kwani manyau nyau na manabii na mashehe na mapadri tofauti ipo wapi zote si imani tuu
 
Huyu kimaadili ya uongozi na ubinadamu wake huwa namfananisha na mjukuu wangu Mizengo Kayanza Peter Pinda. Hawa watu wakati mwingine unasema pengine walikosea kuingia kwenye Siasa ila walitakiwa wawe viongozi kwenye nyumba zetu za Ibada. Yaani wako kwenye level ile ambayo binadamu wa kawaida kabisa aliyeumbwa na Mungu, anatakiwa kuwa.

Una jicho kali, angalau na wewe umeliona hilo. Huyu mtu mimi pia nampenda sana
Ahsante Mkubwa, ila umewaita wajukuu je wewe nini mkubwa kiasi hiko au ni kinyume chake wewe ni mjukuu wa mmoja kati ya hao.

Kwa wizara alizopitia, na kudumu kwake naona uPM unaweza kumfaa sijajua masuala mengine ambayo hatuyajui
 
Hapana! Sio kwenye sekeseke la Lissu bwana! Akiwa Waziri wa Tamisemi, alitajwa kuhusika na uzembe kwenye report ya Prof Osro kuwa akiwa Waziri wa Madini enzi wa Jakaya aliachia mali zetu zikasepa tu hivi hivi! Ndiyo maana aliachia ngazi yeye na Prof Muhongo
Kwa hiyo tuseme alionesha uwajibikaji?
 
Back
Top Bottom