George Simbachawene ni nani hasa?

Hata JPM si alikuwa dereva wa gari za kukodi (taxi) miaka ilee maeneo ya Sinza.

Kuna viongozi wengi wamepitia maisha halisi ya mtanzania lakini baadhi yao hujitia hamnazo.
Mwaka gani?? Unaweza share nasisi hii kitu? Magu sijawahi msikia akisema hii kitu!
 
Jina lake la kati ni Huruma na ndivyo alivyo si mtu mwenye roho ya kwanini.

Hushiriki ibada pale St Albans kwa miaka mingi sana na ni mcha Mungu.

Mimi namfahamu kwa kukutana nae pale St Albans.

Sehemu kubwa ya waasisi (establishment) husali makanisa ya St Albans, St Joseph na Azania (mzee Lowasa &).
 
Miaka alokuwa pale UDSM.
Aiseee! Basi Magu na ubabe wake hajawahi isema hii kitu! Na kama aliwahi isema basi ni siri mno!

Ni sawa na kwamba Magu kaanza kuumwa tatizo la moyo toka akiwa UDSM, hadi tangazo lake lakuomba msaada lilitolewa, akiwa UDSM! Lakini akiwa Rais hakuna mtu aliwahi hoji au uliza! Alipofariki tu! Watu wakalitoa lile tangazo
 
Ni kwamba hufuatilii tu lakini JPM alilisema hili la kuendesha Taxi akiwa UDSM alipokuwa akifungua Kijazi interchange mwezi February 2021.

Na alisema alikuwa akifanya hivyo kufatuta "disposable income" na kituo chake kilikuwa ni Ubungo.

Nafikiri ilikuwa ni ziara yake ya siku tatu na ya mwisho jiji Dar kabla hajafariki.
 
Hamumjui vizuri huyo mzee... ni mkali vibaya mno na ni kauzu ile mbaya!

Picha linaanza yuko vizuri financially na hakuna mtoto wake yoyote aliyesoma nje ya nchi na yuko strictly vibaya mno kwenye malezi ya watoto.

Ni wakubwa serikalini hao, wale watiifu na wanaojituma + wachapakazi na wanajitambua.


Huwa hapendi Kiki za kijinga na za kishamba. Yuko kwenye orodha ya marais wajao miaka mingi ijayo... anaandaliwa nafkiri.


Ana mwanae wa kiume anaitwa "James Simbachawene" naona huyu kijana alikata kamba, kunyoanyoa vipanki na kuvaa visuruali vya kubana... kalisoma chuo cha usimamizi wa fedha haka kakijana. Kanajaribu kujifanya kahuni na kablazameni ila nafkiri mzee anapambana kukazaba kaache ujinga wake kawe kakijana smart kafuate nyayo za baba.

KONGOLE KWAKO MZEE SIMBACHAWENE 👍🏾
 
Huyu kimaadili ya uongozi na ubinadamu wake huwa namfananisha na mjukuu wangu Mizengo Kayanza Peter Pinda. Hawa watu wakati mwingine unasema pengine walikosea kuingia kwenye Siasa ila walitakiwa wawe viongozi kwenye nyumba zetu za Ibada. Yaani wako kwenye level ile ambayo binadamu wa kawaida kabisa aliyeumbwa na Mungu, anatakiwa kuwa.

Una jicho kali, angalau na wewe umeliona hilo. Huyu mtu mimi pia nampenda sana
 
Huyu jamaa kwa ndumba yuko vizur sana nlishapewa na mtu anayekaa jiran yake Kinyerezi mtaa wa Zimbiri jamaa analeta Makalumanzila Mchana Kweupe wamepiga makaniki yao meusi wanafanya yao bila stress
Kwani manyau nyau na manabii na mashehe na mapadri tofauti ipo wapi zote si imani tuu
 
Ahsante Mkubwa, ila umewaita wajukuu je wewe nini mkubwa kiasi hiko au ni kinyume chake wewe ni mjukuu wa mmoja kati ya hao.

Kwa wizara alizopitia, na kudumu kwake naona uPM unaweza kumfaa sijajua masuala mengine ambayo hatuyajui
 
Kwa hiyo tuseme alionesha uwajibikaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…