George Stinney, mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani

Kunyongwa ni aina ya kifo inayohusisha either kuminywa/ kukabwa/ kuvunjwa sehemu za shingo. ' Electrocution' haihusishi shingo, hivyo hakunyongwa, bali ametekelezewa adhabu ya kifo kwa kiti cha umeme.
Dogo acha hizo, hiyo ni execution sio lazima shingo inyongwe
 
Ofcourse, execution sio lazima shingo inyongwe, ila wewe ndio umetaka kuinsunuate kwamba electrocution (execution by electricity) ni kunyongwa, kitu ambacho nimepinga. Otherwise, hata execution by 'Lethal injection' (sindano ya sumu) pia ungesema ni kunyongwa.
 
Ndo maana maandiko yanapobainisha kwamba hakuna dhambi kubwa na ndogo huwa sijawahi kuelewa! Kuna watu naamini kabisa walistahili sehemu mbaya na yenye mateso zaidi ya yale tunayosimuliwa juu ya jehanam!
 
R.I.P George naani wengi walioshiriki udhalimu huo hawapo duniani ama tuseme ni wakati wa mola kutenda yaliyo ya haki.
 
Ofcourse, execution sio lazima shingo inyongwe, ila wewe ndio umetaka kuinsunuate kwamba electrocution (execution by electricity) ni kunyongwa, kitu ambacho nimepinga. Otherwise, hata execution by 'Lethal injection' (sindano ya sumu) pia ungesema ni kunyongwa.
Yes, nayo ni kunyongwa tu. Hukumu huwa ni kuuwawa, sasa kulingana na mazoea toka zama na zama ambapo ilikuwa lazima utiwe kitanzi, basi njia yeyote itakayotumiwa kukunyofoa roho yako, tunai- generalize ni kunyongwa tu
 
Niliiona clip ya tukio hili youtube, hakika niliumia sana.
 
Wazungu wabaya sana
nawashangaa watu wanaowapapalikia bora magu uwanyooshe hata kidogo tu japo kidogo
 
Mnamo mwaka 2014 Mahakama ya South Carolina nchini Marekani ilitengua hukumu ya iliyotolewa na mahakama hiyo ya kumnyonga hadi kufa mtoto George Stinney Jr, ikiwa miaka 70 imeshapita tangu anyongwe.

George aliyehukumiwa kunyongwa mwaka 1944 kwa kuwaua watoto wenzake wawili wa kizungu. Kesi ya George iliendeshwa kwa ubaguzi wa hali ya juu, ambapo hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja aliyeruhusiwa kuingia mahakamani zaidi ya askari aliyemkamata George.

Hata hivyo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia hatiani mtoto huyo, ambaye alihukumiwa kunyongwa kwenye kesi iliyoendeshwa na watu weupe tu. Wazazi wa George hawakuruhusiwa kuingia mahakamani hapo, hata kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi walilazimika kuhama.

George alitiwa hatiani baada ya kuwa ndiye mtu wa mwisho kuonekana akiwa na watoto wawili wa kike wa kizungu, ambao waliuawa kwenye mazingira ya kutatanisha na miili yao kutupwa kwenye dimbwi.

Miaka hiyo kulikuwa na ubaguzi mkubwa wa rangi ambapo watu weusi walikuwa hawasikilizwi wala kupewa haki zao, na walitengwa. Siku ya kunyongwa George aliuawa kwa kuwekwa kwenye kiti cha umeme, na kumfanya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuhukumiwa hivyo nchini Marekani.

Binafsi:

Imenisikitisha sana alikufa kifo cha kikatili sana apumzike kwa amani mtoto george jr.
FB_IMG_1539176824717.jpeg
 
hadithi ya afrola ulela cjaelewa imekuja hapa kufanyaje au tulieeee
 
Mnamo mwaka 2014 Mahakama ya South Carolina nchini Marekani ilitengua hukumu ya iliyotolewa na mahakama hiyo ya kumnyonga hadi kufa mtoto George Stinney Jr, ikiwa miaka 70 imeshapita tangu anyongwe.

George aliyehukumiwa kunyongwa mwaka 1944 kwa kuwaua watoto wenzake wawili wa kizungu. Kesi ya George iliendeshwa kwa ubaguzi wa hali ya juu, ambapo hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja aliyeruhusiwa kuingia mahakamani zaidi ya askari aliyemkamata George.

Hata hivyo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia hatiani mtoto huyo, ambaye alihukumiwa kunyongwa kwenye kesi iliyoendeshwa na watu weupe tu. Wazazi wa George hawakuruhusiwa kuingia mahakamani hapo, hata kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi walilazimika kuhama.

George alitiwa hatiani baada ya kuwa ndiye mtu wa mwisho kuonekana akiwa na watoto wawili wa kike wa kizungu, ambao waliuawa kwenye mazingira ya kutatanisha na miili yao kutupwa kwenye dimbwi.

Miaka hiyo kulikuwa na ubaguzi mkubwa wa rangi ambapo watu weusi walikuwa hawasikilizwi wala kupewa haki zao, na walitengwa. Siku ya kunyongwa George aliuawa kwa kuwekwa kwenye kiti cha umeme, na kumfanya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuhukumiwa hivyo nchini Marekani.

Binafsi:

Imenisikitisha sana alikufa kifo cha kikatili sana apumzike kwa amani mtoto george jr.View attachment 893391
ooohhpsss so sad indeed ".. daaahh
 
Back
Top Bottom