Mnamo mwaka 2014 Mahakama ya South Carolina nchini Marekani ilitengua hukumu ya iliyotolewa na mahakama hiyo ya kumnyonga hadi kufa mtoto George Stinney Jr, ikiwa miaka 70 imeshapita tangu anyongwe.
George aliyehukumiwa kunyongwa mwaka 1944 kwa kuwaua watoto wenzake wawili wa kizungu. Kesi ya George iliendeshwa kwa ubaguzi wa hali ya juu, ambapo hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja aliyeruhusiwa kuingia mahakamani zaidi ya askari aliyemkamata George.
Hata hivyo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia hatiani mtoto huyo, ambaye alihukumiwa kunyongwa kwenye kesi iliyoendeshwa na watu weupe tu. Wazazi wa George hawakuruhusiwa kuingia mahakamani hapo, hata kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi walilazimika kuhama.
George alitiwa hatiani baada ya kuwa ndiye mtu wa mwisho kuonekana akiwa na watoto wawili wa kike wa kizungu, ambao waliuawa kwenye mazingira ya kutatanisha na miili yao kutupwa kwenye dimbwi.
Miaka hiyo kulikuwa na ubaguzi mkubwa wa rangi ambapo watu weusi walikuwa hawasikilizwi wala kupewa haki zao, na walitengwa. Siku ya kunyongwa George aliuawa kwa kuwekwa kwenye kiti cha umeme, na kumfanya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuhukumiwa hivyo nchini Marekani.
Binafsi:
Imenisikitisha sana alikufa kifo cha kikatili sana apumzike kwa amani mtoto george jr.
View attachment 893391