Gerson Msigwa: Huwezi kukurupuka kumfukuza mtu, pengine hata wakaguzi wa CAG nao ukaguzi wao una dosari

Kama kawaida yao washaanza yale ya kusafishana! Hawa wanaona raia kama misukule. Possibly we are! Maana wangeshatoka madarakani...
 
Kati ya CAG na Msigwa, Nani ni mtaalamu wa Ukaguzi!? Sasa tumsikilize CAG au Msigwa!? Au Msigwa nae ana mamlaka ya kumkagua CAG!!??
 
Tayari!!! Bila mabadiliko ya kwel hawa watu wataifilisi Nchi!!
 
Kama ni hivyo,Sasa kwa Nini wao Bunge wachukuwe muda mrefu sana kujadili report ya CAG!?
 
1. Kama wakifanikiwa kubadilisha maudhui ya ripoti ya CAG itakuwa ndio ripoti pekee ya rejea kubatilisha ripoti zote zilizowahi kutolewa na ofisi ya CGA hivyo Kichere atakuwa amekosa sifa za kuendelea kushukilia ofisi hiyo maana inavyppnesha anatumika kisiasa kuchafua watusmishi na kuwapamba wengine kwa maslahi binafsi.

Atakuwa ndio CGA wa kwanza kuja kufunguliwa mashitaka ambayo hataamini kwanini alikuwa anajipendekeza kwa wanasiasa na kuandika ripoti za uongo wakati akijua maudhui yake hayakuwa na ukweli wowote.
 
Ngoja tuone
 
Majizi ndiyo yamejazana serikalini kuanzia jumba jeupe mpaka mashinani. Yanalindana chini ya lichama lao kongwe lililogeuka kuwa la mafisadi tu.
 
Yani hoja km yako, zinatia kichefu chefu. Hivi unajua maana collective responsibility? Ebu nikuulize, wakati Mwinyi anajiuzulu nafasi yake alikuwa ametenda yeye kosa au watendaji wake wa chini? Mzee Lowasa wakati anajiuzulu alikuwa ametenda yeye makosa au watendaji wake wa chini? Walimu 6 huko Tabora waliotuhumiwa kuvujisha mtihani na hatimae kukaa jela takribani miaka mitatu na baadae mahakama kusema hawakuwa na makosa na kuachiliwa hivi majuzi wao hawakuwa watu?

Kinachosemwa na wananchi ni kuona waliotuhumiwa wote wanaachia ofisi kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zao, na ikibainika hawakuwa na makosa wataendelea na kazi km awali. Kwanini wao wana dinda kuachia ofisi kwani ni mali Yao. Kwani hao niliowatolea mfano hapo juu wao hawakuwa na moyo wa nyama?

Achana na ushaabiki wa kisiasa kwenye mambo ya msingi na nyeti kuliko hata nyeti ulizonazo. Watu wajifunze kuishi bila gari za serikali, mafao ya serikali, nyumba za serikali, na kupenda ubwanyenye mbele ya Watanzania wenzao. Tabia za baadhi ya viongozi wa Kitanzania kupenda kunyanyua makwapa na kupandisha mabega huku wakilamba asali kwa ncha ya kisu ndivyo vinavyosababisha ugumu wa kujiuzuru kwa manufaa ya umma pindi anapotuhumiwa.

Nimemaliza.
 
Kwa utetezi dhaifu kiasi hicho, Bw. Msigwa, bila kujua au kukusudia, amewatia hatiani watuhumiwa wote wa ripoti ya CAG pamoja mamlaka za uteuzi/uwajibikaji. Incredible!!!

Tupeni Katiba mpya haya tutayashughulikia kikamilifu 100%, once and for all.
 
Hii nchi vitimbi vingi sana.Huko juu wenzetu wanaokula na kusaza sijui kama wanaifikiria Tz
 
Aache kupotosha umma.
Kwa uzoefu tu, TAARIFA YA CAG NI SAHIHI ZAIDI YA ASILIMIA 98.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…