Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

UFAFANUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria.

Gerson Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali
Yafungulieni na Magazeti jamani
 
UFAFANUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria.

Gerson Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali
Hawa wasaidizi wa Mh Rais ndio walio fungia hivi vyombo vya habari. Hawakufurahia tamko la jana. Hivyo wanetafuta njia mzunguko kumkwamisha mama.
Nashauri Mh Rais hii wizara ya habari ibadilishiwe viongozi. Na zaidi, asiwape nafasi hawa wapiga fiimbi wa Jiwe
 
... tusipodhibiti...
Msemaji wa serikali ametoa ufafanuzi kwamba kilichofunguliwa ni online TV na si Magazeti. Hi kauli Msigwa anadai imetoka kwa Mhe. Rais.

Mwenyekiti wa wazazi Wa ccm ametoka adharani nakusema Mhe. Rais apangiwi kuhusu katiba mpya. Maana ya kauli hii nimsimamo wa chama kuwa hakuna katiba mpya

Lakini haya yanatufundisha Nini? Endapo utahutubia Taifa watu wakakupongeza lakini viongoz wachache wanaokula mema ya nchi wakakasurika basi tambua Tanzania si ya Watanzania Tena Bali ni nchi ya watu wachache.

Hii trend imeturejesha kwenye maumivu Yale Yale, lakini pia mkinzano huu wa kauli una athari kwenye uchumi maana Kama ndani kwa wananchi ahadi zinabadilika je kwa wageni itakuwaje? Tusipothibiti hii Hali upo uwezekano wanaoitwa wawekezaji kuja nakuhamisha rasilimali zetu kuzipokeleka huko walipotoka. Tusicheze na mind za wananchi tutaliyumbisha Taifa, tutatengeneza wapigaji na kuondoa wazalendo
 
UFAFANUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria.

Gerson Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali
Amegeuka 360°,haya bwana.
 
Kwani hayo magazeti yamekosea nini, maana mama anacholenga ni ajira za watu
 
Huyo Msigwa kaandika hapa "vyomb vya habari vilivyo fungiwa". Huyo dogo ata poteza hiyo Ofisi akiendelea kutumia mawazo na kiburi cha Abbas
FB_IMG_1617813089697.jpg
 
Na hizo online TV zilifungiwa bila vifungu vya sheria? Hadi zinafunguliwa bila vifungu
 
Uzuri wa mama yeye anafanya maamuzi tu...utasikia Abas kawa katibu kata
 
Lakini hao ndio wasemaje rasmi wa serikali, na hawawezi kusema bila ufafanuzi wa mwenye kauli, yaani rais wetu Samia. Turidhike kwamba alichagua aina ya chombo cha habari cha kufunguliwa - viji televisheni vya mkononi.

Si vyombo vyote, yaani redio, televisheni, magazeti, majarida na internet kwa ajili ya mitandao ya kijamii
Hao Abbas na Msigwa ni wapuuzi. Rais alitamka kuwa "Kuna vyombo vya habari vimefungiwa....sijui hivyo vi tv vya mkononi. Vifungulieni" Sasa wao wanaleta ujuaji ngoja waone.

Yani Rais alimaanisha vyombo vyote vya habari. Gerson na Abbas waelewe kuwa Jiwe lao halipo tena ooohooo!
 
IMG_0742.png
 
Enzi za uhai wa jiwe ungekuwa ushareply kunipoteza
Umekuwa wa bardiii
Haya rudi kijijini kwenu ukalime
Mwenge unaanza kukimbizwa,nitakupa ratiba urudi nao kama ulivyokuleta mjini.
Wewe upotezwe kwa lipi? Wakati ni utopolo tuu...! Sisi tunaendelea kupigakazi na kula raha zetu wewe endelea na utopolo wako tu.
 
Kwahio waliomsikia ni Msigwa na Abbas peke yao? Magazeti yote leo Tanzania yameripoti tofauti na Abas na huyu Msigwa. Wallah CCM ni ile ile
Tatizo bavicha mnataka mawazo yenu ndio yawe msimamo wa selikali.

Samia alisema nanukuu,
"kuna vijivyombo vya habari mlifungia hivi vi tv vya mikononi hivi, naomba vifungulieni lakini waviendeshe kwa kufuafa sheria. Na makosa yao ya kuviendesha bila kufuata sheria yaainishwe na adhabu zake"

Kama mna kumbuka hivyo vi tv vilifungiwa sababu ya usajili na si kukiuaka maadili ya utangazaji na uandishi kama ilivyo kwa magazeti yaliyofungiwa.
 
Back
Top Bottom