Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

Kumbe nay bure, hamna kitu hapa ni mwendo wa Jiwe. kazi tunayo haki ya mungu!
Kwani wewe ulikuwa na matumaini gani kwa Rais Samia? Ulifikiri tz daima watarejea na udaku wao tena?
 
Hiyo ndiyo hoja na ajenda nzito na muhimu kwa kuanzia - katiba mpya. Ufafanuzi umetolewa, tukubaliane nao. Hata rais mwenyewe amewahi kufafanua makosa ya matamshi yake pale alipotamka mara kadhaa "bunge la katiba" badala ya bunge la bajeti.

Mpaka akasema: "hivi nina maradhi gani na katiba? Tusahau kwanza!"
Binafsi naona sisi kama taifa tunajadili vihoja vyepesi sana, hizo online tv a.k.a youtube channels l, vifurushi vya data, CV za waliopewa dhamana n.k ni hoja ndogo sana...
 
Kwani si tumekubaliana tunataka Raisi awe anasikiliza ushauri,sasa ndo wasaidizi wake wamemshauri afungulie TV Mtandao🤣🤣🤣,mimi siwaelewi kabisa au unataka awe kama jiwe🤣🤣,inaitwa meza moto tema moto🤣🤣🤣
 
Sawa kabisa!
Kamfichia aibu subordinate wake, for sure soon atatoa tena tamko la kufungulia vyombo vya habari kifasaha zaidi ingawa tamko lake kwangu mimi niliona limelenga vyombo vyote na Online TVs zilikuwa mfano. Aliposema Vi TV na ile Vifunguliwe...
 
UFAFANUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria.

Gerson Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali
Kama atafungulia TV tu na kuacha vyombo vingine atakuwa Hana akili ya kujiongeza. Lengo la Rais ni kukwepa lawama kuwa anazuia uhuru wa Habari, uhuru wa Habari sio TV tu.
 
Hao Abbas na Msigwa ni wapuuzi. Rais alitamka kuwa "Kuna vyombo vya habari vimefungiwa....sijui hivyo vi tv vya mkononi. Vifungulieni" Sasa wao wanaleta ujuaji ngoja waone.

Yani Rais alimaanisha vyombo vyote vya habari. Gerson na Abbas waelewe kuwa Jiwe lao halipo tena ooohooo!
Msigwa ni msemaji wa selikali, yani ni mdomo wa Samia na selikali yote sasa wewe unapinga kipi
 
Ufafanuzi unaotelewa na msemaji wa serikali hauwezi kuwa wake lazima atakua amewasiliana na mtoa kauli ilikujiridhisha.
Sasa mkimlaumu mtoa taarifa mtakua mnalaumu asiehusika kabisa yeye ni mjumbe tu sio muamuzi.

Vyama vya siasa jIkiteni kwenye kudai katiba mpya mintarafu tume huru ya uchaguzi lasihivyo baada ya uchaguzi 2025 tutasikia malalamiko yaleyale wakati sasa mmejikita kwenye kusifia na kuzungumza hoja zisizo na msingi.
 
Baada ya tamko la katibu mkuu wizara ya habari maelezo furaha za watanzania zimezimika ghafula kama mshumaa
Watanzani kimya!! kama vile wamemwagiwa maji baridi hawaamini kilichotokea mpaka sasa hivi
Kwa kiswali cha mjini tunasema watanzania wapenda uhuru wa habari na uhuru wa biashara wamepigwa bao la dakika za nyongeza
Watanzania kabla hata hawaanza kufaidi furaha ya uhuru wa habari na uhuru wa kafanya biashara kwa uhuru wamepigwa bao dakika ya nyongeza wamebaki wamepigwa na butwaa!! Hawajui wafanye nini
Watanzani walibeti vibaya wakaanza kushangilia mapema kabla mechi ya uhuru wa habari haijaisha
 
Hajawahi kuwa na akili yule jamaa kimsingi alikua anaelekezwa tu na marehemu babaake magu sio kama anajua hata anachokifanya ni nini , uliona wapi kanjanja anapewa usemaji wa Serikali lazima aonee watu tu hasa wale waliokua makanjanja wenzie ili aonekane sasa yuko juu, stupid kabisa
 
Ngoja niwape mfano wenzenu walivyofanya

Mh. Mwigulu Nchemba ameonesha kuelewa haraka Mh. RAais SSH anataka nini. Kuna swali aliaulizwa kimtego na mwandisi wa habari kuhusu msimamo wa serikali kwenye TASK FORCE ya TRA. Mh. Nchemba alijibu very technical kuwa Wizara inaenda kukaa kufanya marekebisho ili kwendana na muongozo uliotoleea na Mh. Rais. Nampa credit sana Waziri aliongea positive na kuonesha uhakika wa utekelezaji.

Twende wizara ya habari sasa. Mh. Rais kasema vyombo vya habari vifunguliwe Katibu wa Wizara ndugu Abbas anaanza kuwepo specification, msemaji wa serikali day 1 anasema kama agizo la Rais day 2 anaunga mkono ya Abbas. Nilitegemea Innocent aje na usawazisho nae anakuja na approach za ujinga ujinga.

Wizara ya habari Mnamuhujumu Rais.
Au mnaona wivu watu wanavyomuunga mkono au mnajiona untouchables

Waziri nilitegemea wewe uweke sawa kuwa wiki ijayo au tarehe fulani utakatana vyombo vyote vilivyofungiwa mpeane maelekezo ili safari hii wasifanye makosa.

Kwa staili hii Mnamuhujumu Rais wetu mpendwa
 
Mh Samia tulishamuonya bila kutimua hawa mamluki wa jiwe akawaacha wakajipanga atang'olewa yeye , ni lazima angejiuliza kwanini wote waliokuwa wanamuunga mkono jiwe wana nyumba Chato ? yaani kwanini walijenga nyumba za kufikia Chato ili hali si kwao ?
 
Back
Top Bottom