SEHEMU YA SABA:=....
basi baada ya kuzama soko la kilombero nilinunua viatu na nguo za kutosha.
nilikaa kitaa kwa miezi huku nikiwa nakula bata mara triple A,silk club na ma wingu kila weekend,katika kukaa kwangu mtaani kuna demu alikuwa student nilikuwa natoka naye bahati mbaya alipata ujauzito,msala ulikuwa mkubwa sana ikanibidi nikimbie kitaa.
Nikaenda mgodini kupigika tena,dingi akapambana na wazazi wa yule binti,wakakubaliana kuwa nimchukue binti yao ila faini nilitozwa pia.
Basi binti akaenda kuishi kwenye zile room 2 maana zingine nilipangisha akawa mke wangu,mimi nikiwa machimboni..
Nikaendelea na msoto wa kila siku,mawe yakawa magumu kutoka,hali ikazidi kuwa mbaya,siku nimejilaza kwenye udongo nikiwa nimechafuka hatari,mzee akanipigia simu na kuniambia kuna mtu kapenda shamba langu yupo tayari kulinunua.
Basi nikafunga safari kurudi arusha,kufika wife tumbo tayari kubwa na zimebaki siku chache ili ajifungue na ukicheki sina kitu,na wapangaji washanipa kodi siwadai.
Nikaona bora niliuze,kumbe mtej mwenyewe alikuwa geor davie wa ngurumo ya upaka,tukafikia makubaliano ya kuuza akanipa million 17,maana shamba lilikuwa barabarani na anataka kufungua kanisa,kipindi hicho bado hajawa maarafu kama alivyosasa.
Basi nikapokea pesa,nikaona niachane na uchimbaji madini ile kazi inamsoto sana na nihatari sana,nikaona niachane nayo.
Nikafungua account bank nikatia million 15,wife tayari siku zimewadia akajifungua mapacha wawili wote wanaume.
Itaendeleeeea..................