Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

SEHEMU YA KUMI:=......
Basi hali kwangu ikawa mbaya kinoma,nikawa sina chochote zaidi ya pumzi ya mwenyenzi MUNGU,watu walijua huyu tutamzika kesho,ilifika point of no return back ndugu msomaji.
Usione machizi na vichaa mtaani ukawacheka na kuwadharau hakuna kitu kibaya kama depression hii kitu ndo inauwa watu siku hizi,mtu akiwa na depression kujiua ni fasta sana.

Nilishawahi jaribu kujiua mara 4 lakini ikashindikana,nilishameza valium vidongo 14 nakunywa chupa 4 za banana ili nife lakini nilikuja kuhamka baada ya siku 3,nilishawahi kujinyonga lakini kamba zikawa zinakatika,MUNGU muache aitwe MUNGU 🙏🙏🙏🙏 Kama watu hawamuamini waache na roho zao.

Nilikuwa mtumiaji mbaya wa valium,mwili ulikuwa chaka la shetani,hakuna kitu kibaya kama kuji katia tamaa.

Basi maisha ya kawa hayana thamani kwangu zaidi ya kufa tu.
Kuna siku nimekaa mto sanawary ndo nilikuwa naoga huko maana nyumbani nilikimbia,kuna mawazo yakanijia kipondi nikiwa mtoto nishawahi kuwasikia watu wakisema kuwa ela za madini hazidumu zina majini,basi nikajua chochote nilichokipata kwa madini kimeteketea aisee nililia kinyama.

Nikaoga na kufua nguo zangu vinzuri,ili kuwa siku ya j4,kuna wazo lika nijia la kuenda redio safina,sijawahi kwenda ila nikasema lazima nifike kweli nikatembea kwa miguu kwanzia ilboru mpaka mbauda mahali redio safina ilipo.
Sikuwa na nauli hata Mia,ikanibidi nipige kwata..

Nilifika safina nimechoka hatari pia nasikia nnjaa la kufa tu,kuna wa mama. Iliwakuta wanauza ndizi pale nnjee nikawaomba hata ndizi moja,waliponiona hali yangu ilivyo vibaya wakanipa ndizi 4..

Nilikula zile nikashushia na maji ya bomba..

Itaendeleeeeea.
 
Chai
 
Chai
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA:=...
BAADA YA KULA ZILE NDIZI NA KUNYWA MAJI NILIJIKONGOJA MPAKA NDANI,KUNA MAMA ALINIFUATA AKANIULIZA UNASHIDA GANI??
NIKAMUAMBIA NAMTAKA MCHUNGAJI TUU,
MAMA AKAENDA OFFICINE NAKUMUITA MCHUNGAJI,BAADA YA KUJA NIKAMUELEZEA MATATIZO YANGU YOTE.

MCHUNGAJI AKANIOMBEA AISEE NILITAPIKA VITU VYA AJABU SANA,VEUSI KAMA MKAA,BAADA YA KUTAPIKA VILE VITU FAHAMU IKANIRUDIA YA UBINADAMU TENA.

MCHUNGAJI AKANIPA BIBLIA NA NAULI YA KURUDI HOME,HUWEZI KUAMINI NILIRUDI ZANGU KWETU AMBAPO NILIKIMBIA ZAIDI YA MIAKA 2,MAMA ALIFURAHI SANA KUNIONA MARA ALISHANIKATIA TAMAA YA KUNIONA TENA.

WAKAJA NDUGU NA MAJIRANI WAKARIBU KUNIPA POLE,AISEE KUMBE VILE VITU NILIVYOTAPIKA KANISANI NILILISHWA NA WACHAWI NDIVYO VILIVYOHARIBU MAISHA YANGU..

HIYO ILIKUWA 2018..
HUYU MUNGU MUACHE HAITWE MUNGU TUU
DAIMA NITAMUABUDU YEYE PEKEE YAKE..

BASI NIKAANZA MWANZO MPYA KAMA NDO NIMETOKA KUZALIWA,HUWEZI AMINI NIKATAFUTWA NA MSHIKAJI WANGU ANAYEFANYA KAZI YA KUPANDISHA WAZUNGU MLIMA KILIMANJARO,AKANIAMBIA KUNA KAZI YA TOUR GUIDE YA MLIMA KILIMANJARO ,AKANIAMBIA ANANIPA MIEZI KADHAA YA KURUDISHA AFYA TENA..

BASI NIKAANZA KULA NA KUFANYA MAZOEZI
ILIFANYA MAZOEZI KAMA CHAKULA,BAADA YA WEEK KADHAA AFYA IKAANZA KURUDI,NIKAENDA KWA BIBI NGARAMTONI KUKAA HUKO AKAWA ANANIPIKIA LOSHOROO NA VYAKULA VYA ASILI NILIKAA KULE KWA MWENZI 1 HIVI.

AISEE AFYA IKARUDI KAMA MWANZO TENA NIKAPENDEZA MFANO HAKUNA..
JAMAA AKANIPA KAZI YA KUWA GUIDE MLIMA KILIMANJARO,KAZI ZIKAWA NYINGI SANA TIPS KIBAO PESA IKAANZA KUINGIA TENA.

NIKASIMAMISHA ROOM ZANGU 2 CHAPU,WIFE NIKAMRUDISHA NYUMBANI NA WATOTO WATU HAWAKUAMINI KAMA NI MIMI MAANA NIMEPENDEZA KIFUA KIMETANUKA MISULI KAMA YOTE YANI NIKAWA HANDSOME WA MAANA.

MUNGU AKANIPA JAMBO KUBWA SANA..
UNATAKA KUJUA NI JAMBO GANII???

ITAENDELEEEA......
 
nice
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI:=...
INAENDELEEEEA...

MUNGU AKANIPA JAMBO KUBWA SANA,KUNA SIKU NIMERUDI KUTOKA MOSHI ILE NAFIKA TU KWANGU NIKAPOKEA SIMU KWA RAFIKI YANGU ANAYEFANYA KAZI MOJA YA KAMPUNI KUBWA SANA YA UTALII ARUSHA,AKANIAMBIA KUNA WAZUNGU WANATOKA NORWAY WAPO 12 KWAHIYO WANAHITAJI MTU WAKUWAZUNGUSHA ARUSHA YOTE MA MBUGA ZA WANYAMA ZOTE MAANA WANAFANYA RESEARCH,NAKUCHUKUA DOCUMENTARY.

ILA WANATAKA DEREVA ASIYE NA KAMPUNI YEYOTE ILE.PIA WANAHITAJI PROFESSIONAL TOUR GUIDE,PIA WANATOA ELA YA KUKODISHA COASTER KWA MIEZI 2.

JAMAA AKANIUNGANISHA KWAO,BASI NIKAENDA KUWAPOKEA KIA JAMAA WALIKUJA NA VITU VYOTE VYA PRODUCTION.

NIKAWATAFUTIA HOTELI NZURI
KILA KITU KILIKUWA CHINI YANGU..


ITAENDELEEEEA....
NIMEANDIKA KWA KIFUPI MAANA NOW NAPELEKA WAGENI WANAENDA KULA
 
Duu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…