Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Sio kweli kuwa hospitali za Umma zipo juu kuliko Private ,watu wanakimbiaga hospitali za Private kwenda kwenye hspitali za UMMA na hii ni kutokana na gharama kuwa nafuu kwenye hospitali za Umma
 
Kuiondoa ccm madarakani sio solution. Solution hapa ni Mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao utakua mfumo rfiki wa kuhakikisha Matibabu kwa wote yanakua sawa
wamefilisi mfuko wa bima ya afya wanataka tuanze kuchaingia tena ili waje kula tena.
BIMA YA AFYA NI KAMA TOZO ZA SIMU hakuna kitu pale, hakuna kitacho badilika kwenye matibabu
 
Sio kweli kuwa hospitali za Umma zipo juu kuliko Private ,watu wanakimbiaga hospitali za Private kwenda kwenye hspitali za UMMA na hii ni kutokana na gharama kuwa nafuu kwenye hospitali za Umma

Wapi nimesema hospitali za umma bei ni kubwa kuliko private.

Tatizo ni kuwa bei hizi ni kubwa mno nje ya uhalisia. Zingatia pia bei hIzi hatuna ridhaa nazo na haijulikani ni Kwa vigezo zipi huku kodi na tozo tunalipa.
 
Sekta ya Afya inahitaji fedha kujiendesha ndio maana wananchi tunapaswa kuchangia ,je ? Gharama ya matibabu ya moyo au figo inaweza kuwa sawa na mtu anayeumwa malaria ?? Utaalamu na vifaa vinalingana ?? Tusiongee mambo kwa ushabiki tukateni Bima za Afya ,serikal kwa sasa inafanya kazi nzuri ya kuleta teknolojia pamoja na ujenzi wa mahospital ya kisasa nchi nzima ,huu wakati wa ujenzi wananch hatuna budi kuchangia ili huduma iendelee BIMA BIMA BIMAA ni muhimu ndugu zangu
 
wamefilisi mfuko wa bima ya afya wanataka tuanze kuchaingia tena ili waje kula tena.
BIMA YA AFYA NI KAMA TOZO ZA SIMU hakuna kitu pale, hakuna kitacho badilika kwenye matibabu

Hii wataifilisi tena pamoja na kuchukua zaidi kutoka kwetu.
 
Tatizo ni kuwa bei hizi ni kubwa mno nje ya uhalisia.
Embu toa mfano mmoja wa huduma kama consultation, surgery, medicine, or any medical consumables

Ambazo umelinganisha na manunuzi ukagundua hazina uhalisia
 
Hii wataifilisi tena pamoja na kuchukua zaidi kutoka kwetu.
mkuu embu fikiria kidogo kila mtu ana bima ya afya ya sh laki tatu, alafu unakwenda hospitali unaambiwa panado hakuna, we utafanya nini?
Mradi wa mwendo kasi nauli ni kubwa kuliko daladala lakini upo ICU, Bima ya afya ni upigaji tu hakuna cha kuboresha huduma
 
Mkuu hili jambo si binafsi. Kwamba ninayo bima afya hakunisimamishi kuona tunakoelekea siko kwenyewe.

Kwamba NHIF imefilisika? Nini kitazuia mfuko upi kutokufilisika?

Kwamba bei zinapangwa unilaratelly. Hii haikubaliki. Sisi kama wateja binafsi au kupitia bima tunayo haki ya kuzijua gharama halisi.

Tozo na kodi hulipi peke yako. Kwamba hospitali hizi Zina majengo, vifaa, wataalamu, madawa, mishahara nk vinavyotokana na kodi zetu, hapana!

Tusiibiane mchana mchana hivi.

Viko wapi vigezo vya bei hizi tujiridhishe?

Mfuko gani utasalimika kwenye wizi wa wazi huu?
 
Huu ndiyo ulio ukweli. Bahati mbaya ni kuwa kwa kutokujitambua wengine wanakenua kama vile hayahusu.
 
Maswali yangu yalikuwa Aya

Toa mfano mmoja wa huduma kama consultation, surgery, medicine, or any medical consumables

Ambazo umelinganisha na manunuzi ukagundua hazina uhalisia
 
Embu toa mfano mmoja wa huduma kama consultation, surgery, medicine, or any medical consumables

Ambazo umelinganisha na manunuzi ukagundua hazina uhalisia

Majina ya kibeberu hayo hayatafsiriki kuwa pesa.

Wananchi wamewekeza kupitia tozo na pesa zao zikapatikana hospitali, vifaa, majengo, dawa, machela, wafanyakazi , mishahara nk.

Kama unachojaribu kusema ni kuwa sasa utalaamu ni mali binafsi ni muda muafaka tugawane mbao za meza na misumari.

Sera mpya hii ya Bashe haikubaliki.

Tupeni bei tuzijue ikibidi tufanye maamuzi magumu:

Ujuzi, vifaa, majengo, dawa, nk.

Tatizo liko wapi?
 
Cost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.
Nililipa shs 30,000/= mapokezi tu, dawa kheri ukanunue nje ya hospitali na mgonjwa anaporuhusiwa ni balaa jingine wakati dawa zote ulinunua mwenyewe! Kwa kifupi kila unapoambiwa nenda chumba hiki au kile kuna kiingilio kama vibandaumiza.
 
Maswali yangu yalikuwa Aya

Toa mfano mmoja wa huduma kama consultation, surgery, medicine, or any medical consumables

Ambazo umelinganisha na manunuzi ukagundua hazina uhalisia

Sisi ni wateja tunaochelea kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Tumeuliza:

1. Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?
2.Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?
3. Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Majibu yako wapi?
 
Amezoea kutibiwa Aga Khan hivyo hajui majina kwa kiswahili msamehe tu, siku akija Ilala au Mwananyamala atayajua kwa kiswahili.
 
Nililipa shs 30,000/= mapokezi tu, dawa kheri ukanunue nje ya hospitali na mgonjwa anaporuhusiwa ni balaa jingine wakati dawa zote ulinunua mwenyewe! Kwa kifupi kila unapoambiwa nenda chumba hiki au kile kuna kiingilio kama vibandaumiza.
yaani hospitali afadhali kwa mganga wa kienyeji, hapo bado rushwa kwa manesi ya kuzungusha faili ,kumpa dawa mgonjwa
 
Siku ukiugua ndo utaelewa, jikatie bima mapema
 
Ndiyo maana tunauliza:

1. Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

2. Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

3. Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kulikoni kuandikia mate?
 
Hayupo anayekataa cost sharing ila break down ya gharama ni vyema vikajulikana, nani anaweka bei na vigezo gani.

Vinginevyo hapa ni ujanja ujanja tu.
Gharama zipo za aina Mbili.

Kwa Hospitali kubwa (mashirika yanayojitegemea gharama zinapangwa na bodi ya Hospitali ).

Kwa hospital za Wilaya, vituo vya Afya gharama zinapangwa na Halmashauri.

Vyanzo vya mapato ya Hospitali huwa ni Kama ifuatavyo:

  • BIMA
  • Kama huna Bima utalipa gharama zifuatazo:
  • Kumuona Daktari ( Medical consultation ).

Daktari akikuandikia vipimo ukifika Maabara utalipia.

Ukirudi kwa Daktari akikuandikia Dawa ukienda duka la Dawa utalipia.

Ikitokea UKALAZWA utalipia Kitanda kwa siku kulingana na gharama za Kituo husika.

Ukifa, ndugu zako watalioia gharama za mortuary kulingana na siku ulizokaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…