Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Dharura ni wizi kwenye malipo haya hayo hayapaswi kusubiri.

Tutahitaji kupata break down ya malipo haya.

Tunafahamu ni nia yenu tusijue break down hIzi. Kumbe ni kwa sababu ya maslahi binafsi.

Manesi 20 registrars 8 health attendants 4 ... Ili mhalalishe bei kubwa siyo?

Mwogopeni japo mola basi? Watanzania hawa huko vijijini na hata mijini ni maskini mno!
Sawa boss
 
Dharura ni wizi kwenye malipo haya hayo hayapaswi kusubiri.

Tutahitaji kupata break down ya malipo haya.

Tunafahamu ni nia yenu tusijue break down hIzi. Kumbe ni kwa sababu ya maslahi binafsi.

Manesi 20 registrars 8 health attendants 4 ... Ili mhalalishe bei kubwa siyo? Mbona hatuwaoni hao kwenye sessions hIzi za dialysis?

Staff hewa ...

Mwogopeni japo mola basi? Watanzania hawa huko vijijini na hata mijini ni maskini mno!
Sawa boss, ifanyie kazi mapema ili tupate nafuu. Usisahau kutujulisha utakayoyakuta huko. Na ya huko duniani kwingineko.
 
Mjadara mzuri huu.

Tips.
1.Wananchi/clients wanahitaji mchanganuo wa huduma na gharama zake.
2.Kuna concept kwa wananchi kuwa hospital na vituo vya Afya vya umma vinaendeshwa na Govt 100%..... kwa hili inabidi watu waelewe kuwa si kweli kuwa Govt inagharimia 100% cost za uendeshaji ... kuna percentage imeachwa kwa mtumiaji kuchangia. Na jukumu la kupanga bei limekaimishwa kwa bodi za uendeshaji wa vituo/hospital so wao ndio wanapanga bei ya hudumu ambazo mgonjwa atachajiwa ili ku-compliment kiasi kilichotolewa na serikali ili kukamilisha mzunguko mzima wa matibabu... hapa utakutana na pesa ya kufungua file, kitanda n. k

3.kuna baadhi ya gharama za uendeshaji zinategemea mapato ya kituo/hospital chenyewe eg. umeme, maji, posho za overtime na extra duty, on call allowances , Ulinzi, Usafi ...hapa si ajabu kituo cha kawaida kabisa kinahitaji 60M ku-cover hizo cost, so watu waelewe tanesco na mamlaka za maji zinatoza pesa as usual.

4.kuhusu itemization.. hili liko kwenye miongozo/maandishi kama wao wanavyopenda kusema .. BUT nani ana muda wa kuanza kumfafanulia clients item moja moja ...so huduma zimekuwa fixed kwenye mfumo wa package ... na kila package na bei yake(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).

5.Kuhusu Gharama kuwa juu ... inabidi tufanye comperative ... unasema gharama iko juu ukilinganisha na wapi? kwa ukanda wetu sisi ndio tunatoa huduma cheap sana.... kama refference point ni uchumi wa watumiaji (mimi nikiwemo) hapo huwezi kuturidhisha wotee.

WHO IS RESPONSIBLE.

again .. mwananchi eg mwanzilishi wa maada anatakiwa aihoji mamlaka(mhimili uliojichimbia zaidi) kuhusu gharama hizi na itemazation.

CRAZY OPINION FROM MY COLLEGUE.
Turudi sera ya nyuma kidogo ... huduma za Afya na Elimu ziachiwe Govt tuuu na ziwe buree ... private sector abakie huko kwingine ... hii haitatuhitaji BIMA wala mbwembwe nyiingi .. kwanza wahudumu hawatakuwa na choices za kukimbia kimbia mara yuko kituoni kwake muda kidogo yuko private ... hakutakuwa na upotevu wa bidhaa za Afya .. hata akiiba cormodity atapeleka wapi?

Kongole mleta mada .. but kuwa flexible wa Tz hatuko serious hivyo .. tunasubir Afe tukachange msibani at the time hatukuweza kuchangia gharama ya Tiba.
Nakubaliana nawe, lakini crazy opinion ya serikali kufany kila kitu wakati kuna wilaya hapa mjini 75% ya vituo vya afya ni binafsi. Tutahitaji muda na maandalizi.
 
Kasome vizuri Conset form uliyosaini ina mambo mengi ya msingi.

Pia nimesema kuna aina na kiasi cha makosa na adhabu. Duala lilikuwa ni kuwasilisha tatizo la msingi na kushughulikiwa kulingana na shida halisi.

Huku hatuna details, ila makosa yapo.
Ok uhuni wenu tumeujua siwez kuruhusu mgonjwa wangu au mimi kutibiwa kweny hizo hospitali uchwara za serikali

Surgery ndogo tu mnasababisha shida kwenye figo.

Halafu gharama za ujinga wenu na uzembe wenu mnatubebesha sisi
 
Sawa boss, ifanyie kazi mapema ili tupate nafuu. Usisahau kutujulisha utakayoyakuta huko. Na ya huko duniani kwingineko.
Hatutafanyia gizani kama mnakofanyia nyie.

Itakuwa mchana kweupe na hadharani kama humu jukwaani.

Tuna nini cha kuficha inapokuja suala la haki?

Tunahitaji katiba mpya. Kwa hakika katiba mpya lakini na hili ni dharura kweli kweli.

Kwa hakika pamoja na katiba mpya hili nalo ni la kumulika na tunajua wanufaika ninyi na hili ni wezi wachache tu.

Nisiache kukwambia tunapata inputs nyingi tu tokea mahospitalini huko kwa wafanyakazi wasioridhika na hali hIzi.

Ninaamini tuko upande sahihi. Upande wa haki na pia ulio upande wa wengi.
 
Ok uhuni wenu tumeujua siwez kuruhusu mgonjwa wangu au mimi kutibiwa kweny hizo hospitali uchwara za serikali

Surgery ndogo tu mnasababisha shida kwenye figo.

Halafu gharama za ujinga wenu na uzembe wenu mnatubebesha sisi
Pole boss, kuna wakati hazitakuwa uchwara nasi hatutakuwa wajinga.
 
Hatutafanyia gizani kama mnakofanyia nyie.

Itakuwa mchana kweupe na hadharani kama humu jukwaani.

Tuna nini cha kuficha inapokuja suala la haki?

Tunahitaji katiba mpya. Kwa hakika katiba mpya lakini na hili ni dharura kweli kweli.

Kwa hakika pamoja na katiba mpya hili nalo ni la kumulika na tunajua wanufaika ninyi na hili ni wezi wachache tu.

Nisiache kumwambia tunapata inputs nyingi tu tokea mahospitalini huko kwa wafanyakazi wasioridhika na hali hIzi.

Ninaamini tuko upande sahihi. Upande wa haki na pia ulio upande wa wengi.
Sawa, wishing you all the best.
 
Ok uhuni wenu tumeujua siwez kuruhusu mgonjwa wangu au mimi kutibiwa kweny hizo hospitali uchwara za serikali

Surgery ndogo tu mnasababisha shida kwenye figo.

Halafu gharama za ujinga wenu na uzembe wenu mnatubebesha sisi
Unakimbilia kijiweni siyo? mbona hujasolve tatizo coz wale wale uliowakimbia asubuhi ndio watakukuta jioni huko na njaa itakuwa imekuuma sana.
 
We are all human best wishes ni kitu kizuri. Kufanikiwa kwako ni kwangu na yule plae.
Ingekuwa kufanikiwa kwangu, na yule ni kwako tusingeshirikiana kupata gharama sahihi za huduma hIzi?
 
Ingekuwa kufanikiwa kwangu ni kwako tusingeshirikiana kupata gharama sahihi za huduma hIzi?
Gharama zipo mheshimiwa pata kwa kila sehemu, ukifika kituo cha afya kama notice board haina hiyo kitu muulize mkuu wa kituo. Ingawa hawezi kuweka zote kwani ni nyingi. Hivyo, mwambie akusaidie soft copy au hard copy zake.

Tusonge mbele hilo si tatizo.

Ila ujue zitatofautiana kulingana na level ya kituo na eneo kituo kilipo.
 
Tuweke kumbukumbu sawa sawa:

"Tunachohitaji ni break down ya gharama ya huduma moja moja kwenye hospitali za umma."

Kwa maana nyingine:

"Kujua gharama za consumables kwa kila huduma kuhalalisha bei anayotozwa mgonjwa kwa huduma husika."

Tunajua kuwa serikali imewekeza vilivyo kwenye hospitali hIzi na pia hulipa mishahara ya wafanyakazi na hutoa bajeti Kila mwaka kwa ajili ya dawa, stationeries, magari nk.

Tunajua pia kuwa pesa wanazolipa wateja huishia serikalini.

Wasiwasi wetu ni kuwa bei zinazotozwa ni kubwa mno kwa watu au mfuko wowote wa bima kutokufilisika.

Ni nia yetu kuona mifuko hii haitumiki vibaya na wajanja wachache.

Kufanyika kwa "independent audit" kujua kama kuna upungufu wa bajeti, ni kwa kiasi gani na namna gani ifidiwe, bila shaka itakuwa ni njia sahihi zaidi ya kupata haki kwa wote.

Ifahamike kuwa haupo uhalali wa kuibebesha mizigo isiyostahili mifuko ya bima za afya au awaye yote anayelipia gharama hIzi.
 
Bajeti ya matibabu ya 10m/- kwa mwanafamilia kwenye nchi yenye tozo na kodi zote zilizopo nchini haiwezekani.

Hali kadhalika hakuna bima ya Afya itaacha kufilisika Kwa bei hizo.

Zingatia msingi wa hoja:

Bei ni kwa kigezo cha ugonjwa, ujuzi, dawa, vifaa au majengo?

Bila kusahau kuwa wawekezaji kwenye vyote hivyo ni sisi wananchi.
Inategemea anaumwa nini kama kalazwa ICU hospital ya umma ni laki tano kwa siku bado dawa hospital binafsi zingine inafika hadi milioni mbili kwa siku.
 
Tuweke kumbukumbu sawa sawa:

"Tunachohitaji ni break down gharama moja moja kwenye hospitali za umma."

Kwa maana nyingine:

"Kujua gharama za consumables kwa kila huduma kuhalalisha bei anayotozwa mgonjwa kwa huduma husika."

Tunajua kuwa serikali imewekeza vilivyo kwenye hospitali hIzi na pia hulipa mishahara ya wafanyakazi na hutoa bajeti Kila mwaka kwa ajili ya dawa, stationeries, magari nk.

Tunajua pia kuwa pesa wanazolipa wateja huishia serikalini.

Wasiwasi wetu ni kuwa bei zinazotozwa ni kubwa mno kwa watu au mfuko wowote wa bima kutokufilisika.

Ni nia yetu kuona mifuko hii haitumiki vibaya na wajanja wachache.

Kufanyika kwa "independent audit" kujua kama kuna upungufu wa bajeti, kwa kiasi gani na namna gani ufidiwe, bila shaka itakuwa ni njia sahihi zaidi ya kupata haki kwa wote.

Ifahamike kuwa haupo uhalali wa kuibebesha mizigo isiyostahili mifuko ya bima za afya au awaye yote anayelipia gharama hIzi.
Title na hadidu za rejea za andiko zimetimia twende kazi sasa.
 
Inategemea anaumwa nini kama kalazwa ICU hospital ya umma ni laki tano kwa siku bado dawa hospital binafsi zingine inafika hadi milioni mbili kwa siku.

Mkuu hIzi bei hazitoki Kwa Mungu bali zinapangwa hapa hapa na watu kama sisi.

Kwanini bei hIzi ziwe kubwa hivi kwenye hospitali za umma?

Zingatia kwenye hospitali hizo wadau ni sisi kupitia kodi na tozo mbalimbali.

Wafanyakazi wanalipwa mishahara na serikali na pia Kuna allocation ya bajeti Kila mwaka.

Kwanini ICU ni laki 5 kwa siku Kwa mtu? Kwenye laki 5 tufahamishane kimoja kimoja isiwe mbuzi kwenye gunia.

Huo ndiyo msingi wa hoja mkuu.
 
Inategemea anaumwa nini kama kalazwa ICU hospital ya umma ni laki tano kwa siku bado dawa hospital binafsi zingine inafika hadi milioni mbili kwa siku.
Watu hawaelewi haya mambo, kuna hospitali ukikaa ICU siku tatu 10,000,000/= imeisha. Ndo maana tumeomba msingi wa kusema gharama kufuru huko serikalini tuelimishane. Kuna mheshimiwa atafanya data collection na alete mrejesho ili tuanzie hapo.

Ngoja tisubiri mrejesho..
 
Title na hadidu za rejea za andiko zimetimia twende kazi sasa.

Ni vizuri kuwa tuko.pamoja kwenye kwamba hatupingi bima wala kulipia matibabu kwenye hospitali za umma.

Tunapinga ujanja ujanja.

Mjini wanasema "bongo nyoso."

Panq harufu kubwa ya upigaji.

"Tuungane kuwakataa wahuni. Wahuni SI watu wazuri."

Bahati mbaya wahuni wanaweza kuwa wapo Hadi ikulu.
 
Back
Top Bottom