Mjadara mzuri huu.
Tips.
1.Wananchi/clients wanahitaji mchanganuo wa huduma na gharama zake.
2.Kuna concept kwa wananchi kuwa hospital na vituo vya Afya vya umma vinaendeshwa na Govt 100%..... kwa hili inabidi watu waelewe kuwa si kweli kuwa Govt inagharimia 100% cost za uendeshaji ... kuna percentage imeachwa kwa mtumiaji kuchangia. Na jukumu la kupanga bei limekaimishwa kwa bodi za uendeshaji wa vituo/hospital so wao ndio wanapanga bei ya hudumu ambazo mgonjwa atachajiwa ili ku-compliment kiasi kilichotolewa na serikali ili kukamilisha mzunguko mzima wa matibabu... hapa utakutana na pesa ya kufungua file, kitanda n. k
3.kuna baadhi ya gharama za uendeshaji zinategemea mapato ya kituo/hospital chenyewe eg. umeme, maji, posho za overtime na extra duty, on call allowances , Ulinzi, Usafi ...hapa si ajabu kituo cha kawaida kabisa kinahitaji 60M ku-cover hizo cost, so watu waelewe tanesco na mamlaka za maji zinatoza pesa as usual.
4.kuhusu itemization.. hili liko kwenye miongozo/maandishi kama wao wanavyopenda kusema .. BUT nani ana muda wa kuanza kumfafanulia clients item moja moja ...so huduma zimekuwa fixed kwenye mfumo wa package ... na kila package na bei yake(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).
5.Kuhusu Gharama kuwa juu ... inabidi tufanye comperative ... unasema gharama iko juu ukilinganisha na wapi? kwa ukanda wetu sisi ndio tunatoa huduma cheap sana.... kama refference point ni uchumi wa watumiaji (mimi nikiwemo) hapo huwezi kuturidhisha wotee.
WHO IS RESPONSIBLE.
again .. mwananchi eg mwanzilishi wa maada anatakiwa aihoji mamlaka(mhimili uliojichimbia zaidi) kuhusu gharama hizi na itemazation.
CRAZY OPINION FROM MY COLLEGUE.
Turudi sera ya nyuma kidogo ... huduma za Afya na Elimu ziachiwe Govt tuuu na ziwe buree ... private sector abakie huko kwingine ... hii haitatuhitaji BIMA wala mbwembwe nyiingi .. kwanza wahudumu hawatakuwa na choices za kukimbia kimbia mara yuko kituoni kwake muda kidogo yuko private ... hakutakuwa na upotevu wa bidhaa za Afya .. hata akiiba cormodity atapeleka wapi?
Kongole mleta mada .. but kuwa flexible wa Tz hatuko serious hivyo .. tunasubir Afe tukachange msibani at the time hatukuweza kuchangia gharama ya Tiba.