KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu kwa Hiyo ni sahihi kwa hizo gharama? pato la mwananchi kwa mwaka ni kiasi gani? je wananchi wanaweza Kumudu hizo Gharama?
Nashukuru kwa kuhoji

Serikali inalipia gharama za elimu nchini, ili kumwezesha kila mtu aweze kusoma. Ndio maana shule za serikali unalipa.elfu 20, lakini serikali inachangia sehemu kubwa

Vivyo hivyo kwa gharama za kujifungua. Ili kupunguza mzigo wa uzazi. Tanzania inelegant miongozo kibao ya mama wajawazito over the years ikiwa pamoja na kugharamia asilimia kubwa ya hizo gharama.

Nilivyosema kuwa states ni gharama kujifungua sikumaanisha nililinganisha na Tanzania. Nilimanisha ni moja ya nchi ambayo wanalipa 100% which was burden kwa wananchi wake. Alipokuja Obama akaleta Obama care kuwapunguzia wasioweza. Gharama ya kujifungua states ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko anywhere else. Hii inatokana kuwa wamewekeza advanced services kwenye matibabu

Nchi nyingi duniani zina mipango tofauti, kuna nchi zina upungufu wa watu ikitegemea kwamba mama akinifingua mtoto anagharamiwa na serikali mpaka 5 years, hapo ndipo ataachuwa mzazi

Kama hujaelewa naweza kukuelewesh vizuri nikipata kifungua kinywa ndio kwanza naamka
 
Wakuu Kwema? Bila shaka muko salama.

Mwezi uliopita Nilikuwa Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, Baada ya mke wangu Kuhamishiwa hapo baaada ya Kupewa Rufaa kutoka Kituo cha Afya ambapo alienda Kujifungua.

Kitu ambacho Nimeona Gharama za pale ni kubwa sana ni kama Hospitali za Watu Binafsi au Taasisi za Dini n.k

Wakati anapokelewa Pale Emergence nilitakiwa Kulipia Laki moja Fedha Taslimu ambayo wanaita ni ya Accomadation na haina maelezo mengine tena unapewa Control number ulipie ndio aanze Kuhudumiwa.

Baada ya Hapo alijifungua salama watoto wawili Mapacha alikaa siku ya Ijumaa hadi Jumatatu yaani Siku tatu Tu nikapewa Bill ya 1.35 yaani (Milioni moja laki tatu na elfu thelathini na tano) Nikasita kulipa nikaenda kwa wahasibu Kugombana nao Kidogo nikitaka Ufafanuzi japo Ilishindikana.

Baadae niliuliza Nikaambiwa Ghrama ya Kulala kwa Siku ni 50,000 lakini gharama ya Kujifungua ni 750,000. Niliambiwa Hiyo ssera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.

Nilipambana nikalipia kiasi nikatoka.

Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wake pale hadi fedha ipatikane.

Kwa kweli jambo hili linaumiza sana watanzania wa hali ya Chini ambao Kimsingi wanaamini Hospitali za Umma zinazoendeshwa naKupata Ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi za wananchi gharama zake ziwe rafiki ili kila mwananchi aweze Kumudu ila imekuwa ni Tofauti.

Soma Pia:Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza

WIZARA YA Afya Aid Inatakiwa ilitazame hili na wawaweke wananchi wazi kwamba ile ni Hospitali ya Kulipia .

Ushahidi wa Nyaraka zote nianzo Mods musifute mukitaka ushahidi wa Receipt na Bill nitawapa
Jina lenyew ushasema hospitali ya taifa
si tunaendaga tu vituo vya afya ni bure tuu kama akijifungua kawaida kama utatozwa hela haizidi
Mhh Mean while me nili jipanga kwa zaid ya 500k wakat wife ana karibia kujifungua .nikawa surprised naambiwa nilipie 30k ya kitanda tu mengine bure ,kwakua alijifungua kawaida ..

NOTE
ilikua kituo cha afya nazani ndo bure aki jifungua kawaida na 150k operation. Uko Hospitall za Rufaa ni kukandwa tu
Upo sahihi mkuu
 
Nashukuru kwa kuhoji

Serikali inalipia gharama za elimu nchini, ili kumwezesha kila mtu aweze kusoma. Ndio maana shule za serikali unalipa.elfu 20, lakini serikali inachangia sehemu kubwa

Vivyo hivyo kwa gharama za kujifungua. Ili kupunguza mzigo wa uzazi. Tanzania inelegant miongozo kibao ya mama wajawazito over the years ikiwa pamoja na kugharamia asilimia kubwa ya hizo gharama.

Nilivyosema kuwa states ni gharama kujifungua sikumaanisha nililinganisha na Tanzania. Nilimanisha ni moja ya nchi ambayo wanalipa 100% which was burden kwa wananchi wake. Alipokuja Obama akaleta Obama care kuwapunguzia wasioweza. Gharama ya kujifungua states ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko anywhere else. Hii inatokana kuwa wamewekeza advanced services kwenye matibabu

Nchi nyingi duniani zina mipango tofauti, kuna nchi zina upungufu wa watu ikitegemea kwamba mama akinifingua mtoto anagharamiwa na serikali mpaka 5 years, hapo ndipo ataachuwa mzazi

Kama hujaelewa naweza kukuelewesh vizuri nikipata kifungua kinywa ndio kwanza naamka
Nimekuelewa Mkuu
 
Jina lenyew ushasema hospitali ya taifa
si tunaendaga tu vituo vya afya ni bure tuu kama akijifungua kawaida kama utatozwa hela haizidi afu 50 tena kuwe kumetokea shida wakati wa kujifungua
walimhamishia Huko Mkuu. Kwani Hospitali ya Taifa sio sehemu ya Hospitali za Umma?
 
Umepigwa parefu sana hapo kujifungua hospital za serikali ni bure kabisa ,sio za serikali tu hata zenye ubia na serikali.Utalipia kitanda,au kama kuna upasuaji mkubwa au mdogo,pia kama kuna chakula
Aisee nilikuta watu wengi sanawanadaiwa kule na wameshindwa kutoka wameshikiliwa zaidi ya mwezi na hili ndio linaloumiza zaidi
 
yaani nilipe hospitali ya umma laki saba mke wangu kujifungua, kwa kipi? hata private hawapo hivyo.
Nchi hii mkuu imeshakuwa kama ni ya tabaka fulani hivi. na ukigoma kulipia ujue hawatamuachia. kuna watu wana miezi wapo kule tu hawawezi kutoka wala hawana uwezo wa kulipia
 
Nadhani hapo ndipo wengi walipaswa kuhoji, alienda kama mgonjwa wa private au public?.

Maana kama ni public, mbona watu wanatibiwa na hizo bima tu?, kama kuna dawa iko nje ya mpango wa bima utaambiwa, utapewa control number na utalipia au uandikiwa kisha ukanunue nje.
Kabisa, ukiwa na Bima haisumbui
 
Mhh Mean while me nili jipanga kwa zaid ya 500k wakat wife ana karibia kujifungua .nikawa surprised naambiwa nilipie 30k ya kitanda tu mengine bure ,kwakua alijifungua kawaida ..

NOTE
ilikua kituo cha afya nazani ndo bure aki jifungua kawaida na 150k operation. Uko Hospitall za Rufaa ni kukandwa tu
hatukupenda kwenda Huko Mkuu sisi tulipewa Rufaa maana Kimara HC walisema hawana vifaa hivyo wakampeleka Huko.
 
Sera ya Afya ya 2007 inaelekeza kuwa Matibabu ya Mama Mjamzito na Watoto chini ya Miaka 5 ni bure.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa anatambua kuwa zipo baadhi ya Hospitali za Umma zinazotoza wananchi fedha na kuzitaka kuacha mara moja huku Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitakiwa kusimamia jambo hilo.

Dkt. Mollel hakusema kuwa hakuna Hospitali isiyotoza watu kwa ajili ya kupata huduma hiyo kama ilivyoandikwa hapo juu.
 
Back
Top Bottom