Treni mpya ya SGR yenye mfumo wa Electrical Multiple Units (EMU) imeanza safari za Dar Moro Dodoma tangu tarehe 1 mwezi wa 11 2024.
Licha ya kuwa more comfortable zaidi ya zile za kawaida, treni za EMU zinafikia kasi ya juu kwa haraka zaidi.
Safari ya kwanza kutoka Dar kwenda Dodoma imechukua saa 3 tu ikilinganishwa na takribani saa 4 kwa SGR ya kawaida.
Yote haya ni mambo mazuri katika nyanja ya usafiri Tanzania na ni mambo ya kupongzwa. Ila angalizo moja hapa ni juu ya gharama kubwa za safari ya treni hizi. Inaonekana wazi kabisa usafiri huu mzuri haujakusudiwa kuwa wa kila mtanzania kwani watanzania wenye kipato cha chini hawataweza kumudu kulipa shilingi 100,000/- hadi 150,000/- kati ya Dar-Dodoma.
Kimsingi gharama hizi zilipaswa kuwa za ndege.