Gharama za treni mpya ya EMU kutoka Dar hadi Dodoma zilipaswa kuwa gharama za usafiri wa ndege

Gharama za treni mpya ya EMU kutoka Dar hadi Dodoma zilipaswa kuwa gharama za usafiri wa ndege

shilingi 100,000/- hadi 150,000/- kati ya Dar-Dodoma.
Kama kawaida kila kitu kizuri wanawaweka kauzibe ili wanufaike wao tu.
Walipokuwa wanapanga kwa upande wao hizo ni bei ndogo sana kwani wanashinda ulaya na marekani na wanalipa mamilioni kibao kwa ndege.

Unajua hii ndio shida ya viongozi wa kiafrika.
 
Gentleman, pendekezo zuri sana.

Tuwe wavumilivu kidogo kwa sasa, kwani ni mapema mno kuzungumzia chochote kuhusu hilo.

Hata hivyo mamlaka husika zimechukua pendekezo na oni hilo, na watafanya tathmini ya kina baadae na kuona linalowezekana,
ingawa kwasasa safari zitaendelea kama kawaida kwa gharama hizo hizo 🐒
Unajifanya msemaji wa TRC.
 
Dar Dom ndege huwa zinajaa pamoja na ukubwa wa nauli...

Nadhani hata hiyo treni watakuwa wamerefer bei za ndege then wakapunguza kwa asilimia kadhaa around 60-50%

Ukiacha hilo, bila shaka gharama za kiuendeshaji maana hiyo mashine inatumia umeme sio wa bure, ina wafanyakazi lukuki kwa kila safari moja (tofauti n basi)...
Hoja zako ni dhaifu mno.
 
Treni mpya ya SGR yenye mfumo wa Electrical Multiple Units (EMU) imeanza safari za Dar Moro Dodoma tangu tarehe 1 mwezi wa 11 2024.

Licha ya kuwa more comfortable zaidi ya zile za kawaida, treni za EMU zinafikia kasi ya juu kwa haraka zaidi.

Safari ya kwanza kutoka Dar kwenda Dodoma imechukua saa 3 tu ikilinganishwa na takribani saa 4 kwa SGR ya kawaida.

Yote haya ni mambo mazuri katika nyanja ya usafiri Tanzania na ni mambo ya kupongzwa. Ila angalizo moja hapa ni juu ya gharama kubwa za safari ya treni hizi. Inaonekana wazi kabisa usafiri huu mzuri haujakusudiwa kuwa wa kila mtanzania kwani watanzania wenye kipato cha chini hawataweza kumudu kulipa shilingi 100,000/- hadi 150,000/- kati ya Dar-Dodoma.

Kimsingi gharama hizi zilipaswa kuwa za ndege.
Si mlisema yule jamaa analeta maendeleo ya vitu na si watu
 
Bado hatujayaishi maono ya usafiri huu, mwenyewe alipoanzisha treni ya umeme alidhamiria ibebe mizigo kutuunganisha na nchi jirani, gharama za kubeba mizigo ya nchi zingine zingebalance gharama za kubeba abiria na ikawa nauli rafiki kwa sisi walalahoi.

Bei kubwa ya nauli inaongeza gharama zaidi za uendeshaji maana wasafiri wanakuwa wachache, hapa ndo utaona jinsi tulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri na kuamua mambo.
 
Angekuwepo mwasisi wake Hayati JPM, bei zisingekuwa hivyo.
Nafikiri hata atakayekuja 2025/2026 hatakubali hizi bei ziendelee maana atakuwa ameona maisha halisi ya wapiga kura mara baada ya kuzunguka nchi nzima.
Itoshe tu kusema, "vitu vya kurithi huwezi kuwa na uchungu navyo kama vile vitu vya kutafuta mwenyewe".
 
View attachment 3141120

Hii pia ni gharama ya Treni ya Mchongoko (EMU) kwa daraja la kawaida (Economy).

Tuache kuzungumza yale ambayo hayapo katika uhalisia ilimradi kuikosoa tuu serikali.
Watanzania ni watu wa ajabu sana. Hebu ona walivyozua taharuki kumbe hawajaamgalia hata hivyo viwango. Mkuu usingeleta huu ushahidi hapa ningeondoka na matango pori.
 
Dar Dom ndege huwa zinajaa pamoja na ukubwa wa nauli...

Nadhani hata hiyo treni watakuwa wamerefer bei za ndege then wakapunguza kwa asilimia kadhaa around 60-50%

Ukiacha hilo, bila shaka gharama za kiuendeshaji maana hiyo mashine inatumia umeme sio wa bure, ina wafanyakazi lukuki kwa kila safari moja (tofauti n basi)...
Ni kwa sababu wahusika wengi wanalipiwa na serikali na siyo kwamba ni wafanya biashara ni wale ambao hawana uchungu wa kusema nauli kubwa au ndogo
 
Sasa si unaona vitu vyenyewe vimekuwa na vululuvululu?
Hata kuviendesha mnashindwa. Mwenyewe angekuwepo angesimama na kutoa bei elekezi na ingekuwa imeisha. Kuwapa wahuni nagasi za decision making matokeo yake ndio hayo
 
Back
Top Bottom