Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

Kuna mambo unachanganya!!sasa uvaaji wa kwenye sehemu za starehe nao uufananishe na matukio yanayorushwa live na tv, sehemu za starehe zina sheria zake ambazo umri chini ya miaka 18 hauruhusiwi kuwa eneo hilo!!eti kwa kuwa kwenye simu zao wana picha/video za aina ngono basi wasisimamie maadili???!!inshu sio kuvaa madela,lakini vazi hilo halikuwa sahihi sana , hapo labda ungezungumzia ukubwa wa adhabu tu, ningekuelewa lakini sio hizo hoja zako .
 
Kwaiyo unamaanisha kiongozi atoe upendeleo kwa waliomchagua sababu tu walimpigia kampeni, hata kama wanakosea?
 
Mnajua maana ya live event?
Kama kwenye simu yangu kuna pilau
Ndo halali kuonesha chochote kwenye TV??
Simu zetu watoto wanatazama hizo pilau?
Kwahiyo hata video za Gwajima na amberuti zioneshwe wasafi TV?

Hiyo Event sikuifuatilia nisiwe muongo lakini kutokana video niliyoiona inaonesha hiyo Live event ilioneshwa Usiku ila sijui muda gani specific

secondly hiyo attire ya Gigy ni zile nguo zinazomatch rangi ya ngozi yake labda na hizo nakshi tu ndo zimeleta shida, Sijaona uchi kama Wa Nick minaj au coachella ya Beyonce ambayo wanafki wengi wa humu husifia kama maendeleo ya stage peformance.. kiufupi sijaona kama ni big issue ya kumatch hasara ya kuifungia media 6 months

Kingine nadhani badala ya kuwatupia lawama wasafi na kusheherekea ban yao. Hao TCRA wangeweka mifumo thabiti ya kuchuja maudhui na muda wa kurushwa maana kuna nyimbo watoto wenu wanazisikiliza saa saba mchana na zina impact kuliko hiyo "Imaginary nakedness" ya gigy
 

Hizi ndio points at least mtu unaweza kuongelea, Leo hii nyimbo nyingi zinaimba soft porns na humu zinashabikiwa kupita kiasi ila leo hao hao mashabiki wamegeuka watakatifu ghafla wa kusimamia maadili. Huu ni unafki
 
Chukua suruali yoyote anayovaa dem wako kisha mpelekee mama ako, hapo ndio utajua si kila nguo inayovaliwa barabarani basi inatakiwa na mama ako avae. Uwe na adabu
Ndo uache kutetea upumbavu. Kamvalishe mamako ile nguo kama unaona iko sawa kimaadili
 
hivi yule msanii ROSA LEE anaishi kenya vile.. πŸ™„

Wanaimba Matusi Tupu atleast East Africa Radio wanacheza Clean Versions tu za Bongo Fleva ukikuta wamecheza Dirty basi ujue hakuna DJ bali ni presenter tu.

Ukipata Muda nime attach versions mbili -Clean version ni ya EA Radio na Dirty Version ni Online(Nimeokoka Gnako)

"Nimeokoka siku hizi hatupigi ******* ,ingekuwa zamani ningepita na Zuchu,Huo usela **** " - Shetta (Clean)
""Nimeokoka siku hizi hatupigi mapuchu ,ingekuwa zamani ningepita na Zuchu,Huo usela mavi " - Shetta (Dirty)

Your browser is not able to play this audio.
Your browser is not able to play this audio.
 
HAWA BASATA HAWAJIELEWI NA SERIKALI PIA

Unafungia watu wakati mitandao ya ngono iko free nchini watu wanaangalia upuuzi,afu wanafungia Twitter

Unafungia wanasanii wa ndani wakati kuna video za nje zinaonyeshwa wakati zina watu wamevaa mavazi mbaya zaidi ya yale ya gigy na zinaruka hewani
 
Siyo kwamba akili ya kikahaba imetuvaa Sana watanzania ndo maana?. Kwann huo mchoro usiuone kama ramani ya Iran?
Mchoro unafanana na **** halafu nione ni kama ramani ya Iran, hapo nitakua naidanganya akili yangu.
 
kiuhalisia hiyo vazi ndio halina shida sana ila shida inakuja kwenye hizo bolded area kwenye matiti na hiyo hapo chini.kitendo cha hayo maeneo kukozwa kinafanya mtazamaji wa azingatie/aone kirahisi..
 
Lakini si tunawaangalia kupitia local channels !!?? Au hazipigwi kwenye vipindi !!?? Mbona havifungiwi!??
Kwani mkuu Muislamu safi akialikwa kwenye Sherehe ya kipaimara ndio unakuwa Uhalali wa yeye kushiriki mkuu wa meza!?

Wacha tuone ushetani wao, na sisi tuwaoneshe utofauti watoto wetu ..kubwa unaweza kuwa msanii unavaa vitenge na utatokelezea.. sio lazima uanike uchi ndio ung'ae..

Sasa wakiamua wanataka kujianika.. wanapanda tu kwa Trump... Mimi najiuliza mbona wsanii wa Malaysia hawakai uchi!? Je UAE!? Oman, Iran, Kuwait!? Kwanini na wao wasisaule kabisa....maana kuendelea wamendelea kuliko sisi mbali sana...

Nadhani kama tunaiga tuige vya maana, sio kuiga tuu hata ujinga... Msanii mwenye elimu na anaamini kwenye kipaji hawezi kutembea uchi... Ni insecure non artiste kama huyu dada enda up doing stupid things...

Yule mwenzake alijijua akaenda kupika.. sasa hivi heshima yake iko, sio.lazima avue jukwaani na kujidhalilisha na kuwadhalilisha wanawake ndio apate ugali. Ukiwa bora kwenye chako sio lazima uwe extra.

Na watoto wetu lazima waone..na shortcomings wazijue wakiamua kuacha njia unayowafunza nayo..basi hilo ni juu yao.
 
Mni Nadhani TCRA Kwa kushirikiana na BASATA wangeweka SARE/UNIFORM maalum kwa ajili ya Perfomance zote za majukwaani, Kama (POLICE au WANAFUNZI)
Nadhani hii itasaiidia kukomesha hii dhahma
 
Wewe ukiwa na Binti yako.. (would you be comfortable na uvaaji huu!?)

If not then hayo si maadili. Hiyo picha kwangu mimi sio tu mbaya ila yuko uchi kabisa... Na hiyo ni kwa watanzania asilimia 65+ tunaoishi vijijini...
Usisingizie kijijini hebu angalia ngoma zetu za asili za huko kijijini wanavyovaa ni vibaya zaidi ya hivyo. Hata hivyo nakubaliana na wewe kua lazima maadili yasimamiwe ila ukitoa adhabu lazima uwe na justification ambayo katika hii scenario ni ya kutafuta na tochi huku adhabu ikiwa kubwa sana.
 
tena wamemkosea sana, kitumbua chenyewe kilisha expire kwa kugawa gawa hovyo anataka kulichafua taifa letu. TCRA ni bora mmfungie na huyo GIGGY kifungo cha maisha asifanye show yoyote.
 
Nashukuru at least tunakubaliana..

Changamoto ya sheria na kanuni ni swala kubwa kuliko TCRA wenyewe.. hivi vitu viko kwa sasa wanasimamia utekelezaji.

Kama sheria na kanuni haziko fair lazima turudi kwenye drawing board.. Hii mambo sio ya kujiamulia tuu..

Na shida yetu watz sheria zinapotungwa utasikia wekeni sheria kali ili tuwanyooshe wahalifu.. tukifika kwenye kutekeleza utasikia jamani ila sheria ni kali sana..as if wakati wa uandaaji Watu wanakuwa wamejifungia ndani..

Tumewapa sheria Hizi miaka karibu mitano sasa.. tuwaachie wazisimamie.. kama kuna umuhimu wa kupunguza adhabu kwa kosa la namna hivi basi tuandae utaratibu wa mapitio ya sheria na kanuni zake.
 
dunia gani nyie? Mnataka wasanii wavae madela na mashuka
πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“
 
Nguo inaonyesha mifano ya utamu we unasema kuwa haina shida utamu nauona kabisa tena wameweka na vile vimavuzi we jamaa sijui unatetea nini hapa.
Kwa kweli hata mimi sifahamu nini kinatetewa. I think he needs glasses to think that he thinks there is nothing wrong is ridiculous to say the least.
 
Timu domo mnatokwa mapovu wakati mnaona kabisa gigy alikosea.

Mnapenda kukumbatia cheap whores waliojivika uanamuziki kisa hawana malipo makubwa kama wanamuziki wa kike wastaraabu
 

Hii nguo haifai na Siyo sawa na nguo za Ma Bar etc, Hakuna mtu anavaa hivi mtaani au popote publically....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…