Nikiri kwamba mimi sikutazama live show ya Giggy Money iliyorushwa na Wasafi TV ambayo TCRA hawakuipenda.
Lakini kupitia platforms tofauti za
social network nimeweza kuona picha ya Giggy akiwa kwenye vazi fulani hivi inayojadiliwa sana kwamba ndiyo alikuwa amevaa wakati wa show (picha ipo chini hapa).
Binafsi sijaona tatizo na vazi lile. Vazi limebuniwa vizuri linaonesha maungo ya Giggy vizuri kabisa. Shida iko wapi?
Mbona ndiyo hayo mavazi nayaona bichi, kwenye
swimming events na maahindano ya mamiss. Bila kusahau huko kwenye mabaa, mitaani n.k. Sasa ninyi TCRA mnalinda maadili ya watazama TV tu?
Mko dunia gani nyie? Mnataka wasanii wavae madela na mashuka?
Halafu huu unafiki tutauacha lini watanzania? Hivi kweli tukipekuwa simu zenu ninyi mnaodai kukerwa na picha za Giggy hatutakuta picha za "pilau"?
Ninyi mnaojitia kukirihishwa na picha za Giggy ndiyo ninyi wenye nyumba ndogo na michepuko kama yote. Hayo ni maadili? Lkn mkisimama majukwaani mwajitia wasafi kama malaika.
Kama kweli tunataka kulinda maadili basi tuzuie uchafu kila idara, ofisi, sehemu za starehe, vyombo vya usafiri na kwingineko. Katika hili kuna kitu hakiko sawa.