Gilead Teri: Sera za Uchumi za Rais Samia Zavutia Uwekezaji wa Trilioni 20 ($7.7b). Amfananisha na Deng Xiaoping Baba wa Uchumi wa China

Gilead Teri: Sera za Uchumi za Rais Samia Zavutia Uwekezaji wa Trilioni 20 ($7.7b). Amfananisha na Deng Xiaoping Baba wa Uchumi wa China

Nchi ambayo hata viti vya kukalia walimu ni shida watu wanasema sera zake kiuchumi zinaendana na China?
20240126_205851.jpg
 
Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania TIC bwana Gerald Teri amesema sera Bora na nzuri za Uchumi na Biashara zilizoasisiwa na Rais Samia zimefanikisha kuvutia uwekezaji wa mtaji (FDI) wenye thamani ya $7.7 bln Kwa mwaka 2024.

Bwana Teri amesema Hilo ni ongezeko la zaidi ya mara 3 kutoka Shilingi Trilioni 5( $2b) mwaka 2022 Hadi Trilioni 20 ($7.7b) mwaka 2024.

Pia soma Bajeti ya Serikali mwaka 2025/26 Itakuwa Trilioni 55.03. Sawa na ongezeko la Trilioni 20 Ndani ya miaka 4*1/2 ya Rais Samia.

Bwana Teri amefananisha ukuaji huu wa Uchumi na kipindi Cha Uongozi wa Rais Deng ambae anajulikana kama baba wa Uchumi wa China Mpya kwani mnamo mwaka 1992 ,China chini ya Deng Xiaoping ikipata ongezeko kubwa la uwekezaji na ujuaji wa Uchumi wa zaidi ya mara 3.👇👇

My Take: Hakika Samia ndio Deng Xiaoping wa Tanzania na amekuwa rafiki mkubwa wa biashara na uwekezaji.

Tunampa maua yake angalia hai na anaona.👇👇

Pia soma Dollar yaanza kushuka kwa kasi

Ngoja waje wafuasi wa chama fulani waje kubisha yaan wao kila kitu ni kubisha sijui wana nn
 
Tatizo kubwa la sisi watanzania ni kutojikubali. Ifike wakati tujipongeze kwenye maeneo tunayofanya vizuri na tujikosoe na kujirekebisha kwenye maeneo tunayofanya vibaya. Tusisifie kila kitu wala tusisilibe kila kitu
Tunaweza kujidharau ila kwa kipindi hiki tunafanya vizuri kuwazidi majirani zetu. Ila tusisahau kwa rasilimali, nguvu kazi na uoto na hali ya hewa tuliyonayo tunaweza kufanya vzr zaidi. Shime vijana tuamka tuchakarike bado tumelala mnooo, wengi tunastuka tukifika miaka 30 ama 40 wakati ilibidi kuanzia 18-25 vichwa viko moto
 
Naona kama Jamaa Gilod Teri ni kama anasuka namba ivi, hio miradi tunayoaminishwa ipo na ni mpya , ipo wapi? Wameajiri nani? Maaana wakifanya intavyuu wanaonesha tu miradi ya zamani toka enzi za mkapa, sijui lakini hawa majamaa wanaongea kingereza kingi ni wa kuwaangalia kwa makini.. juzi zito kampiga swali ambalo kila mtu anajiuliza ila hajalijibu. Jamaa yuko smart ila hii nchi ngumu mno haina majibu mepesi mepesi 🤣majuzi tu mabalozi wote waliandika barua kwamba wawekezaji wao wanasumbuliwa na tra asa purpose ya tic ni nini
 
Attachments

  • IMG_2112.jpeg
    IMG_2112.jpeg
    1.2 MB · Views: 4
Naona kama Jamaa Gilod Teri ni kama anasuka namba ivi, hio miradi tunayoaminishwa ipo na ni mpya , ipo wapi? Wameajiri nani? Maaana wakifanya intavyuu wanaonesha tu miradi ya zamani toka enzi za mkapa, sijui lakini hawa majamaa wanaongea kingereza kingi ni wa kuwaangalia kwa makini.. juzi zito kampiga swali ambalo kila mtu anajiuliza ila hajalijibu. Jamaa yuko smart ila hii nchi ngumu mno haina majibu mepesi mepesi 🤣majuzi tu mabalozi wote waliandika barua kwamba wawekezaji wao wanasumbuliwa na tra asa purpose ya tic ni nini
Wewe upo Mkoa gani kwanza nikutajie miradi ya huko?

By the way Iko Kila Mkoa japo Mingi ipo Dar,Pwani,Arusha,Dom,Tanga na Mwanza.

Mwisho Gilead alijibu Hilo swali fuatilia conversation hizo na Kwa ushahidi akamwambia Zito awe anapakua bulletin ya Kila robo inaonesha mtawangiko wa miradi.

Usichokijua ni kwamba hata gorofa Mpya inayoanzia mil.500 ni sehemu ya miradi maana mnaweza kuwa mumekariri kwamba miradi ni viwanda tuu nk
 
Back
Top Bottom