Goba - Mbezi kuwa zaidi ya Sinza, Tabata

Watu ni kweli wanajenga kwa kasi, ila mipango miji ni mibovu kwa kweli. Ingekuwa na mipango miji ya kueleweka ingekuwa poa sana. Sasa sijui ni kwa sababu ya miinuko mingi au kupangilia mitaa ni janga sugu?!
 
Unafurahia Nini eneo Nyumba hazijapangwa.


Watanzania tembeeni hata hapo Namibia muone maana ya mji kuwa mzuri
 
Dar es salaam yote ni slam tu...kifupi jiji la Dar es salaam lote ni kama Tandika tu...

Kuna kipindi Tabata ilisifiwa, dah hiyo tabata sasa huko ndani vichochoro balaa.. sehemu nyingine hata magari hampishani, watu waSinza nao walikuwa wanajiona wamemaliiza kwenye vile vichochoro wanaita wenyewe mitaa, Sinza vibarabara na vidimbwi vya maji kila kona sijui walivyominyana vile wanatofauti gani na sisi wa Tandika, Tandale na Manzese huku..

Goba nayo sehemu nyingi imeanza kuwa na vichochoro na magari kupishana ni issue, watu wameanza kuminyana balaa...
 
Moja ya suluhu ya watu kuacha kujenga kiholela ni kuacha kukata viwanja vya high density baadala yake viwanja vyote katika nchi viwe Low density...Kuanzishwe vyeo vya mabwana ardhi wa kata ambao wanaripoti ardhi wilayani na kazi yao kuhakikisha ujenzi unafuata taratibu na ramani za mipango miji zinafuatwa..
 
Bongo high density ndio kila kitu
 
Ushauri Mzuri sana huu.
 
Siyo rahisi sana.Kama Kimara na Mbezi siyo sawa na Tandale then Goba itakuwa vizuri
Kimara ina nini kipya? Mbona haina mvuto kabisa? Goba maeneo yake yapo vizuri. Ila hakuja pangiliwa kabisa. Na ipo siku itasababisha unadhifu wake uwe kwenye mgogoro
 
Kimara ina nini kipya? Mbona haina mvuto kabisa? Goba maeneo yake yapo vizuri. Ila hakuja pangiliwa kabisa. Na ipo siku itasababisha unadhifu wake uwe kwenye mgogoro

Kimara na Goba ni tofauti sana.Hata bei ya viwanja inaonyesha hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…