MANAKE MKARI
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 299
- 240
What are you talking about? Vile vingi sio viwanja...ni mashamba. Mbweni na Bunju kumepimwa properly lakini sio Goba. Salasala pia kuna eneo limepimwa na kweli kuko njema kweli kweli
Hakuna mpangilio wa majengo wala mitaa, eneo likishakuwa na mpangilio hovyo hata liwe na nyumba kali kiasi gani, linabaki hovyo tu.Sinza haina tofauti na Magomeni, ishapitwa na wakati, Goba ni habari nyingine, inapendeza sana kutokana na vilima kuna sehemu karibu na Mbezi Juu kuna mandhari nzuri sana unaliona jiji na lote na city centre na bahari kwa pamoja,pia barabara kuu za kuingia na kutoka Goba zinapendeza sana
Goba itafunika vibaya sana kutokana na madhari yake ya vilima....na hili limeshadhiri kutokana na kasi yake ya ujenzi wa nyumba nyingi za hadhi ya juu...
Watu wanaangalia madhari ya eneo, ukisubiri eneo kupangwa utakuwa umechelewa.....Kitu ambacho wengi hatukubali ni kuwa wa Tz wanaangalia vitu vingi zaidi ya eneo "kupangwa".
Mkuu pande za mbezi itakua habari nyingine imagine hapo hujazungumzia barabara za makabe,msumi nazo zikiunganishwa.Kuna eneo nasikia wametengewa na ruti mpya za magari ya abiria zitaanzishwa za kuanzia na kuishia hapo.
Nimesikia eneo linaitwa Saisai. Kwa habari nyepesi pia kuna ujenzi wa barabara kiwango cha lami kuunganisha Goba-Matosa-Kimara na Goba-Matosa-Temboni (Mbezi).
Kwenda Mbezi Luis, Mbezi Beach, na Kwenda Madale na Tegeta tayari kiwango cha lami.
Mzee karibu na madale piaMkuu pande za mbezi itakua habari nyingine imagine hapo hujazungumzia barabara za makabe,msumi nazo zikiunganishwa.
Machinga wajengewe huko mana wateja wapo
Moja ya suluhu ya watu kuacha kujenga kiholela ni kuacha kukata viwanja vya high density baadala yake viwanja vyote katika nchi viwe Low density...Kuanzishwe vyeo vya mabwana ardhi wa kata ambao wanaripoti ardhi wilayani na kazi yao kuhakikisha ujenzi unafuata taratibu na ramani za mipango miji zinafuatwa..
Mkuu mbona kama unafoka hivi[emoji3]Ushauri mzuri sana huu ili huko mbeleni kuepuka
Kuchafua miji. Leo sinza, magomeni, tabata, tandika, mwananyamala, mbagala, ni sawa na kipilipili cha nywele za mtu asie pitisha chanuo kichwani.
Inatia aibu sana pale upo kwenye ndege unatua DSM. hiyo DSM yenyewe sasa,[emoji23][emoji23][emoji23] ukianza kuangalia maeneo ya jirani ya Yombo, Kiwalani, Temeke, huko kote kote ni takataka.
Nyumba hazina mpangilio, ukanaribishwa Dar na nyumba zina mabati yenye kutu, yameshikiliwa na vipande vya mawe kwenye mapaa... zimekaa kulia kushoto juu chini , hakuna mpangilio and no green zone kabisaa. Ni aibu kwa city center kuwa ya ovyo
Nenda Mwanza uone kule milimani vijumba vilivyo utadhani uko milima ya GalilayaEneo kama goba ingekua kwa wenzetu huko dunia ya kwanza pangekua pa kuvutia sana kwa jinsi ambavyo kungepangiliwa na ile mandhari yake ya vilima
Ila ss ni hapa bongo ukipita pale kuna mchanganyiko wa kila kitu [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Kwa mara ya kwanza nakanyaga ardhi ya Tabata, mandela road ni vumbi tupu.Tabata itabaki juu
Kule juu nchi za wenzetu huko kungekua ni sehemu ya kuvutia sanaNenda Mwanza uone kule milimani vijumba vilivyo utadhani uko milima ya Galilaya
Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app