Tetesi: Godbless Lema huenda akawa Katibu Mkuu ajaye wa CHADEMA

Lisu wa 2020 ni tofauti na wa sasa kwa sababu anampinga mama Abdul?
 

1. Lisu
2.Heche
3. Lisu

Pagumu aisee! Wote wakurupukaji
 
Akiwa Lema itapendeza sana
 
Mpiga ramli piga vzri na Bado hujasema lissu forever
 
Baada ya kupatikana kwa mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye ni Tundu Lisu na John Heche sasa ni dhahiri Godbless Lema ndiye atakaye chaguliwa kuwa Katibu mkuu kukamilisha sekretarieti ya chama hicho.

Ikumbukwe kuwa Lema ni kambi Lisu na ndiye aliyekuwa msimamizi wa kura za Lisu kwenye uchaguzi wa kupatikana kwa mwenyekiti wa chama hicho

Inaonyesha timu Lisu walishajipanga mapema kuwa Lisu agombee uwenyekiti, Heche makamu mwenyekiti wakishinda Lema atateuliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho

Hivyo kuna kila dalili Lema kutangazwa kuwa ndiye katibu mkuu wa chama hicho kabla ya mkutano wao mkuu kwisha ili kukamilisha safu yao ya uongozi

Hapo watakuwa wametimiza utatu wao mtakatifu Lisu, Heche na Lema ndio maana Lema hakutia nia ya kuomba umakamu na kuomba wenyekiti wa kanda kwa makusudi kabisa kwa kuwa alishahaidiwa nafasi ya katibu mkuu

Comasava Lisu na Heche
 
sava tre` bien merci
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…