Godbless Lema: Vijana wote mnaoendesha bodaboda, miaka 20 ijayo wote mtakuwa mmekufa

Godbless Lema akiwa Mwanza amesema “Ukiona dereva bodaboda ameongezeka ujue ni umasikini umeongezeka, hakuna kazi ya mateso, ufukara na umasikini.

"Vijana mnaoendesha bodaboda hivi sasa, miaka 20 ijayo wote mtakuwa mmekufa, mtaumwa vifua, viuno, migongo na wengine mtakuwa vipofu kutokana na upepo.”
 
Kwani uwongo???

Mfano,uwe unakaa gongo la mboto na kila siku uwe una piga trip za kuja moroco,hutamaliza miezi 3,6 lazima utakutana na jambo,kama siyo ajali ya kukuletea kilema basi kifo

Ova
Acheni kuperekeshwa na siasa za kinafki.

Ingekuwa mtu unakufa kirahisi hivyo watu tusingekuwa tunazama maduarani huku mvua zinanyesha.
 
Lema hataki tena siasa za kura ya mtu sasa kaamua kuwapa hasira muitoe CCM madarakani.

Hawezi kueleweka ila anachokifanya ni siasa za Marx, ni mbaya kwa mtawala sababu anakuchonganisha na tabaka la wafanyakazi.

Nawaza hivyo.
Unawaza upumbavu. Anawachonganisha wapiga kura na chama chake. Kaamua kuisaidia CCM kujipatia kura zote za bodaboda..
 
Godbless Lema akiwa Mwanza amesema “Ukiona dereva bodaboda ameongezeka ujue ni umasikini umeongezeka, hakuna kazi ya mateso, ufukara na umasikini.

"Vijana mnaoendesha bodaboda hivi sasa, miaka 20 ijayo wote mtakuwa mmekufa, mtaumwa vifua, viuno, migongo na wengine mtakuwa vipofu kutokana na upepo.”
Ukweli mchungu sana
 
Lema limbukeni tu asome historia tunakopitia sisi hata nchi zilizoendelea zilipitia hatua zote tunazopitia
 
Vipi kuhusu makuli viwandani, wanaozama migodini wao hawatapata matatizo ya vifua, migongo na viuno?

Lema anataka wote tukakae bungeni tupige meza eeeh!
Anataka wote tukimbilie Canada labda
 
Kwani uwongo???

Mfano,uwe unakaa gongo la mboto na kila siku uwe una piga trip za kuja moroco,hutamaliza miezi 3,6 lazima utakutana na jambo,kama siyo ajali ya kukuletea kilema basi kifo

Ova
Ajali haina kinga hata nyumbani kwako unaweza kuwasha pikipiki ikakusababishia ajali, acha ushamba wewe
 
Bodaboda sio kazi ni taabu nashida...
Wanasema eti kazigani huli mpaka ukaliwe nyuma!!!
Bora niwe fundi ujenzi,seremala nk
 
Back
Top Bottom