Godless Lema aahirisha mkutano wake na waandishi wa habari

Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.

Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.

Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.

Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.

Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.

Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.

Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Mbona anajitetea sana, Ila pamoja na hayo watu wameshamjua, Zitto alianza hivi hivi Msigwa naye alianza hivi hivi press press, halikadharika Slaa matokeo yake yanajulikana.
 
Yeye anatiliwa mashaka, mashaka juu yake bado yapo. Ni wajibu wake (hata kama sio kuita waandishi), kudhibitish mashaka juu yake kuwa sio ya kweli.
Yeye kusema amekaa lock-up mara 50, kuuwawa, kukimbia nchi haina maana hawezi kufika bei.
Wapo watu walikwenda zaidi ya hapo, na bado wakasaliti mageuzi kwa vipande vya fedha. Kumtilia mtu mashaka sio jambo baya, ni wajibu wa mtiliwa mashaka kuthibitisha usafi wake.
Well
 
Lema yuko sahihi, tatizo la Chadema ni Heche, Heche ndio mvurugaji mkubwa wa chama. Lema akiondoka CHADEMA,mikoa ya kaskazini, Moshi na Arusha Chadema watakuwa hawana support tena!
Screenshot_20260714-183814~2.png
 
Lema yuko sahihi, tatizo la Chadema ni Heche, Heche ndio mvurugaji mkubwa wa chama. Lema akiondoka CHADEMA,mikoa ya kaskazini, Moshi na Arusha Chadema watakuwa hawana support tena!
Bakini na CCM yenu. Achana na chadema. Kama Mh. Heche anavuruga chadema mliyosema mliiua zamani si ndio mngetakiwa mfurahi. Heche hanunuliki.
 
Safi sana Godbless Lema . Nakuomba sana usiyumbishwe na hawa machawa wa ccm wanaopenyeza sumu .... umekipambania chama kwa mateso makubwa sana , hata katika uongozi huu ni wewe uliyejitoa hata kwa kwenda kinyume na kaka yako Mbowe .... rudi kwenye mapambano kwa nguvu moja na ultimatum thabiti ., najua siasa za sasa ni ngumu zenye kujitoa bila malipo ila panakaribia kukucha ..... umenipa moyo sana the roll model wangu
Lema kafika bei hata Mbowe kakipambania sana chama tena ni mwanzilishi lkn alipofika bei akaondoka.

Kumbuka Mbowe alikuwa anapigiwa kampeni na chawa wa CCM ili aendelee kuwa Mkiti the same sasa anavyopongezwa Lema leo na wana CCM.
 
Heche anaiendesha Chadema, kama chama cha familia yake, amekula michango ya tone tone, na hakuna wa kumuajibisha, anaejaribu kufungua mdomo kuhoji kama lema alivyofanya, anamsulubu . Heche hafai kuwa kiongozi!
Na tutaendelea kuchanga aile as long mapambano yanaendelea. Wewe unafikiri mkewe na watoto Wanaishi vipi kama baba yupo kwenye ukombozi wa nchi?
 
Heche anaiendesha Chadema, kama chama cha familia yake, amekula michango ya tone tone, na hakuna wa kumuajibisha, anaejaribu kufungua mdomo kuhoji kama lema alivyofanya, anamsulubu . Heche hafai kuwa kiongozi!
Wivu utakuua. Ulitamani sana Godbless Lema aondoke CHADEMA. Sasa mashavu yamewashuka mbogamboga nyie
 
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.

Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.

Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.

Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.

Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.

Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.

Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
tuna kusubiria kule muda ushafika mkuu😅
 
Dhamira njema haipigi kelele wala haitangazwi bali hujitangaza yenyewe na kuthibitika kwa matendo!
 
Kw
Lema yuko sahihi, tatizo la Chadema ni Heche, Heche ndio mvurugaji mkubwa wa chama. Lema akiondoka CHADEMA,mikoa ya kaskazini, Moshi na Arusha Chadema watakuwa hawana support tena!
Kwasababu amekataa kwenda kwenye maridhiano feki? Vyama vyenu vipo vingi kwa nini msiridhiane navyo?
 
Back
Top Bottom