Godless Lema aahirisha mkutano wake na waandishi wa habari

Godless Lema aahirisha mkutano wake na waandishi wa habari

Kakosea sana. Ajiandae kutimuliwa CHADEMA. Hiyo press conference aliyoahirisha ndo ingemsaidia kutofukuzwa.
 
Heche anaiendesha Chadema, kama chama cha familia yake, amekula michango ya tone tone, na hakuna wa kumuajibisha, anaejaribu kufungua mdomo kuhoji kama lema alivyofanya, anamsulubu . Heche hafai kuwa kiongozi!
Chai, propaganda, uongo wa Mbogamboga 🚮
 
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.

Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.

Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.

Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.

Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.

Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.

Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Good move
 
Nafikiri kama umesikiliza hotuba ya Heche na ya Mnyika utaelewa kuwa Chadema haiendeshwi na hao wanaharakati uchwara, na ni Lemma tu aliteleza baada ya kuanza kujibishana na yule chizi fresh Sativa.
Lakini Kuna baadhi ya viongozi ndani ya chadema wanawatumia hao wanaharakati kwamasilahi yao ndani ya hicho chama.
Lema ameanza kushambuliwa baada ya kuhoji matumizi ya michango ya tonetone kitu kinacho onesha kuwa wanufaika wa hizo tonetone ndo walio wa tuma hao wanaharakati kumshambulia Lema.
Hili la yeye kutoa rambirambi Kwa Samia limejichomeka tu kijuujuu tu lakini mizizi wa fitina ni matumizi ya tonetone.
 
Back
Top Bottom