Ndugu yangu, nashukuru kwa mawazo yako mazuri ila naomba umuulize Askofu wa Ngara Diocese kama alisharudishiwa hati yake. Kosa ni kuulizia watu waliopotea na maiti zilizookotwa kwenye viroba plus katiba huru.
Rais wetu mpendwa alikataa kutoa ruhusa mshtakiwa kumzika mama yake wakati yeye mama yake amemuuguza hapo kwake Chato kitandani.
Watu walikufa kwa shinikizo la damu baada ya baba na mwana kumfukuza kazi mbele ya kadamnasi pale kwenye daraja la kigamboni.
Je sera ipi ya chama chochote inayoruhusu watu kupotea, watu kupigwa risasi na kunyang'anywa uraia bila kesi yoyote kufunguliwa?
Wote tunaishi na kufariki mara moja hivyo hakuna atakayerudi kurekebisha ya nyuma. Sera zinatungwa na binadamu na huyo binadamu anaamua afuate sera ipi na akandamize ipi.