God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Kwa hiyo Mungu ilikuwa ni chaguo lake kuumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya au naye hakutarajia?
 
Kwa maana hiyo sio uovu
 
Kwa hiyo Mungu ilikuwa ni chaguo lake kuumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya au naye hakutarajia?
Mungu kama ilivyo baba zetu siku zote He wants the best for us; I believe Him, Things have reasons/purpose.

Nikuulize wewe je ungependa kuishi kama roboti? au ungependa kuishi kama mwanadamu?

Mh! sina namna ya kumtofautisha roboti na mwanadamu hata hivyo kulingana na unavyomchukulia mwanadamu. Pole.

Lakini we jamaa ni mbishi tu, kuna sehemu hadi ukatype kwamba hata hicho ulichokitype kilikuwa kimeshaapangwa!! seriously??
 
Nishakuambia kuhusu mfano wako wa baba kum refer Mungu ni kosa

Baba hajaumba ulimwengu ambao hata yeye kuna mambo tele hapendezewi nayo na ndio maana ni kawaida kumkuta akiwa na stress kwa namna mambo yanafanyika bila mapenzi yake na amekosa uwezo wa kuyafanya yaende kwa namna ambayo anataka yeye.

Baba hana uwezo wote wa kurekebisha kile ambacho anaona hakiko sawa
 
Kama unauliza kuhusu maoni yangu yakuhusu ulimwengu wa namna gani ambao ulikuwa best mi ningechagua ule ambao haupingani na sifa za Mungu wako

Usio weza kuruhusu maovu. Usiseme ameruhusu maovu ili kufanya watu wasio robot wakati huko mbinguni kuna maisha ambayo hayaruhusu maovu na hakuna kiumbe kinacho behave kama robot
 
Wa namna hiyo ungefanya upendo ushindikanike, upendo huja kwa hiyari na sio sheria kali.

Na nitazidi kusema kuwa hakuna kizuizi cha kinguvu kinachozuia raia wengi tu wa kimbingu wasitende maovu [kinyume na mapenzi ya Baba] bali ni wao wenyewe tu na upendo wao ndio unaowashikamanisha. Mfano Yesu angeweza kuamua kuepuka kikombe bali aliamua kuendana na mapenzi ya Baba, kutii au kuwa muislamu literally. Shetani aliamua kinyume na akatenda kinyume na iliwezekana na alikuwa mbinguni! Baadhi ya malaika pia waliwahi kushirikiana na Ibilisi. Inawezekana.

Sitaacha kutoa mifano, vitani akikamatwa raia wa kawaida au mwanajeshi wa kawaida jeshi la adui linaweza kujaribu kumtrain na kumbreak ili awe upande wao. Lakini kuna baadhi ya vyeo mwanajeshi akifikia ni bora tu ukimkamata umuue maana loyality kwa nchi yake ipo kiwango cha juu mno. Na hiyo haiondoi kuwa mwanajeshi huyo anaweza kuamua kuisaliti nchi yake. Yaani ukute mwanajeshi katika difinition ya yeye kuna jina la nchi yake kabisa atakufa kabla hajaisaliti nchi yake. Ndio watu wa mbinguni, wamejidifine kuwa wao ni sehemu ya ufalme wa Mungu hawafanyi uovu, ila wakiamua wanaweza. Ndiyo maana sisi tunasemaga tu generally mbinguni hakuna uovu

Lakini pia mambo mengi kule hakuna, magonjwa, njaa, na vitu vingi vya kidunia. Unabakia tu utii na kiburi katika maamuzi. Aliyeenda kule alishajiamulia tangu duniani kuwa atakuwa mtii sasa abadilikie nini tena akifika huko? Mbinguni hawabehave kama maroboti wanatenda kwa mapenzi yao kabisa kazi za Mungu hata kama kinadharia wangeweza kuchepuka[wengi wao].
 

Tunapaswa kujifunza kutenda mema hapa dunini hata tukifika mbinguni tuishi milele na Mungu muumbaji huku tukiwa na mili mipyA
 
Kwanza Hakuna FREE WILL....isipokua kuna utashi..Mungu katupa utashi..utashi ni utambuzi wa jema, baya, nini cha kufanya, nini nisifanye na matokeo yake ni nini....Hicho ndo Mungu katupatia...yaani ametupa uwezo wa kughamua matokeo ya matendo tunayofanya...Tunafundikshwa amri kumi za Mungu na maelekezo mengine kibao, hizi ni amri....ni maelekezo, tunapaswa kufanya na tusipotekeleza tutaadhibiwa...Mfano ukiwa barabarani unaendesha..ukikuta alama za zebra unapaswa kusimama...dereva anayesimama kwenye zebra anakua kafanya kwa free will au sababu anajua ni sheria na akipita atapewa adhabu, lkn pia hapohapo kuna madereva wengi tunapita tu Zebra..hatupunguzi au kusimama kidogo...je tunakua hatujui matokeo yake kuwa kuna 30,000 au??Utashi ni kutambua kuwa kupita kwenye zebra bila kupunguza si sawa sababu unaweza kusababisha ajali kwa wavukaji etc...kuamua kwenda au kusimama ni maamuzi binafsi...huku ukijua nini matokeo yake....

Suala la moto au mbingu pia tunalichukulis kibinadamu sana....Roho ya mwanadamu ni mali ya huko ilikotoka ....Roho zetu zimeumbwa zirudi kwa mmiliki wake...supernatural being/Mungu....(Kumbuka Binadamu tuna sehemu tatu-MTU WA NJE-Mwili huu, Mtu wa Ndani-Soul-Mtu wa Ndani zaidi-Spirit...)..Ukifa mwili wako na soul zinaperish..lakini spirit yako inaondoka....inaungana na energy ilikotoka...HAPO sasa ndo suala la Mbingu na Moto linakuja....Kama ulifanya makosa....Roho yako haitaruhusiwa kurudi kwenye ukamilisho wake..kufika inakopaswa kuwa.....kumbuka hii ni pigo kubwa sana..ni kama vile uwe na kiu kali halafi hupewi maji..au kama pande mbili za sumaku zinavovutana na upande unaovutwa uwekewe kizingiti....Huu ndo moto ..

Mbingu ni kinyume chake....roho inaenda kwenye ukamilifu, inafika kwa Mungu...etc..

Ninaamini tutawatambua ndugu zetu wote....Mungu ni upendo na hana chuki....kama aliweza kukunganisha na mtu kimwili hawezi kuwa katili na kuwanyima hiyi furaha mliyoianzisha duniani....Hivyo tutajuana, tutatambuana, tutaenjoy LKN katika hali nyingine.....na raha ambazo haziwezi linganishwa na raha za dunia hizi...
 
Mungu au shetani siyo majina ni dhana tu (concept) kama ilivyo ubaya, wema, upendo, chuki n.k

Kimsingi ni cheo kama ilivyo kwa rais, mfalme, malkia n.k

Tatizo linapoanzia ni nani anastahili kupewa hivyo vyeo.

The good news is that wote wanaochangia huu uzi na wengine watakaoendelea kuchangia wote wako sahihi.
Hii ni kwasababu you can only express what you know.
And what you know is the collection of whatever you have ever learned (formally and informally) and held it as true.

Things gets weird when you go a little deeper to find the source of all our accumulated knowledge.

Knowledge inapatikana kwenye maandishi kama vitabu, majarida n.k. pia kwenye mafundisho na mapokeo/simulizi mbalimbali.

Kama ni vitabu, swali nani aliviandika na alikuwa ana lengo gani. Vitabu vyote viwe vya dini au vya sayansi, historia, hadithi n.k kuna lengo lililokusudiwa na mwandishi/waandishi.

Hii ndiyo sababu ya kuwa na philosophy zinazokinzana au kushabihiana na kutofautiana. Ndiyo sababu ya kuwa na imani au dini zinazotofautiana kimtizamo na kimapokeo.

Kwa sababu hiyo kila mtu yuko sahihi kwenye mtazamo wake. Na katika hili hakuna mungu wala shetani.

Niseme tu there is a supreme intelligence at the centre of the universe who has set universal laws that execute themselves regardless of whether we believe in god or satan.

Let me stop here before I get myself lost.
 
Kama upendo huja kwa hiari na sio sheria kali kwanini kuna adhabu ya moto?

Watu wanafanya mema sio kwa kupenda ni kwasababu ya kuogopa moto, sasa hiyo hiari hapo iko wapi?
 
Mungu amemuumba mtu na free will kwa lengo la kumwonyesha ukweli wa mambo ulivyo au utakavyokuwa katika hayo mambo anayochagua au atakayochagua.

Uchaguzi wetu ndio hatima yetu. Kama tunachagua ubaya kwa mfano, hivyo ndivyo hatima yetu inakuwa. Lakini Mungu anaweza kuingilia.

Kila kitu, chochote chanzo chao ni Mungu; hivyo kila kitu ni kitakatifu. Katika ukweli huu ndio pia ukweli wa free will kwa binadamu.
 
Unauhakika gn kuwa yuda yupo tumboni kashatengenezwa kuwa msaliti +? Lete ushahidi wa maandiko matakatifu sio dhana za kufikirika
 
Nini maana ya freewill?
 
Kama upendo huja kwa hiari na sio sheria kali kwanini kuna adhabu ya moto?

Watu wanafanya mema sio kwa kupenda ni kwasababu ya kuogopa moto, sasa hiyo hiari hapo iko wapi?
Tuna hatua kadhaa za hisia zinazotawala katika kumjua Mungu;

Hatua ya hofu ya Mungu au uoga wa mabaya yanayoweza kukupata kama kifo na jehanamu humsaidia mtu auache ujinga aanze kumtafuta Mungu. [Uoga huwafaa wote wasiotaka kutumia akili vizuri, mfano watoto kwa baba - ila wakikua mbinu hii haifai]

Akishampata anaanza kumjua na kadri anavyomjua hofu inampungua wakati imani 'trust' ikiongezeka.

Trust ikikomaa inazaa hisia za upendo na kujitolea 'dedicated' kwa kutenda kazi za Mungu kunakuwa ni matokeo. [Watu waliokomaa, trust na love na service ndizo zinawashikamanisha]

Watu wengi tu leo tupo hatua ya kumpenda Mungu na kujitolea kwake hata kama labda hakuna mambo ya moto. Hata kama hakuna mambo ya miujiza. Tumemuamini Mungu na tunampenda na tunamtumikia. Binafsi hata kama hakuna maisha baada ya haya nimekubali kuwa katika hayahaya maisha nitajitahidi kuyaishi vizuri uweponi mwake.

In fact tushawahi kukaa na mzee mmoja tukajadili uwezekano wa hiki tulichonacho ndicho chenyewe tukagundua hata zile ahadi za mbingu mpya na nchi mpya zinaweza kutimizwa hapahapa na maisha yakawa ufalme wa Mungu! sio lazima wote tufe;

Mfano 1. kila mmoja akafuata dhamiri na Roho Mtakatifu [sheria ya Mungu iliyoandikwa mioyoni mwetu], 2. akafanya kazi anayoipenda na 3. matunda yake akayafaidi na familia na jamii, 4. jamii zote zikaacha kujifunza vita badala yake nguvu zikaelekezwa kwenye uzalishaji mali matrekta[kufua panga zetu ziwe plau] 5. upendo kiujumla ukatawala. Sifa za ki utawala wa Mungu
Au 1. Kila mmoja akaongozwa na ubinafsi hata kama dhamiri inamsuta, 2. Kila mmoja akafanya kazi kitumwa na bado asilipwe stahiki [tabu tupu] 3. unyonyaji 4. Tukaendelea kuwekeza katika tafiti za silaha kalikali za kinyuklia, silaha etc 5. kiujumla chuki ikatawala. Sifa za ki utawala wa shetani
 
Mungu hajampangia yeyote kitu chochote.

Kila kitu kinatokea kwa sababu ya uamuzi ulioufanya ambao utapelekea uamuzi mwingine.

Kwa mfano; Ukiamua kuchukua masomo ya sayansi yatakuja kusababisha uchague course ya aina fulani ambayo nayo itapelekea uishi maisha tofauti kabisa na let's say ungeamua kuchagua masomo ya sayansi.

Lakini sababu zote hizo ni matokeo tu ya uamuzi unaoamua kuufanya. Hakuna anayekupangia.
 
Ungepangiwa usingekuwa na mamlaka ya kufanya uchaguzi. The very moment unakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi, hapohapo dhana ya kupangiwa inaondoka.
 
Unatumia ubaya kufanya mazuri yaonekane mazuri

Kwani haiwezekani kuwa na freewill yenye kuchagua mazuri pekee?
Unakuwaje na uhuru wa kuchagua kama tayari umeshapangiwa?

Unaambiwa chagua jibu sahihi kati ya yafuatayo;
Rais wa kwanza wa Tanzania ni:
(a) Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Hapo unachagua nini sasa?
 
Rudia kuisoma, nimekuwekea na kwa Kiswahili.
 
Hakuna chochote kilipangwa. Maamuzi yako ndiyo yanakuletea mpango mzima wa hatma yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…