God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Huenda mungu hakumuumba shetani
Siyo huenda, hiyo ni fact.

Mungu hakumuumba shetani, alimuumba Lucifer. Kila alichokiumba Mungu ni chema (Mwanzo 1:31).

Shetani ni matokeo ya uchaguzi wa Lucifer kutokuendelea kuwa mwema.
 
Mungu akijua utaenda kushoto, hapo una uchaguzi wa kufanya unachotaka ukaenda kulia?

Kama huna option hiyo utasemaje una uhuru wa kufanya unachotaka wakati choice ilishakuwa fixed kabla hata hujazaliwa?

View attachment 2242516
Hatujalazimishwa kutenda au kuchagua kile anachokijua au anachokiwaza Mungu.

La sivyo, kusingekuwa na uovu maana Mungu ni mwema na anatuwazia mema (Yeremia 29:11)

Mungu kujua utaenda kulia au kushoto hakukulazimishi wewe uende kule ajuako yeye.

Una maamuzi ya kwenda popote.
 

Mi sina Mengi ila nitakujibu kwa kutumia movie ya Matrix

Underson: If you Already know ,How am i going to make a choice?

Oracle: You didnt come here to make a choice, You have already made it!!…
you came here to understand why you made it””…..

KwakiasiFulani inajibu kitu
 
But sovereign man and Sovereign God are mutually exclusive.
Not really.

We were created in the image and likeness of God.

Just as how God is sovereign, so we are. This is the reason for the existence of our free will.

We were created sovereign.
 
Nilitaka kuweka sawa kwamba Mungu hakutupa utashi usio na mipaka. Mnara wa Babeli, Gharika ya Nuhu, Sodoma na Gomora, Kifo cha Herode, Yona na Ninawi ni mifano michache kuwa mwanadamu hakupewa uhuru wa kufanya chochote bali kuna mipaka!
Hakuna mipaka, kuna matokeo ya uamuzi wetu.
 
Ukishakuwa na hofu juu ya adhabu fulani uliyoahidiwa kupewa endapo hutafanya yale uliyoamrishwa ufanye utasemaje uko huru?

Kama upendo huja kwa hiari kwanini Mungu hakuweka mfumo huru ambao watu wangemuabudu kwa hiari yao bila kulazimishwa kumpenda kwa kuogopa moto?

Pana free will mpaka hapo?
 
Kuchagua masomo ya sayansi kwako kunaweza kuonekana kama umefanya uamuzi huo kwa utashi wako lakini kihalisia ulikwisha amuliwa uje uchague sayansi na haukua na uchaguzi mwingine
 
Ungepangiwa usingekuwa na mamlaka ya kufanya uchaguzi. The very moment unakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi, hapohapo dhana ya kupangiwa inaondoka.
Hakuna mtu ambaye yuko free kufanya maamuzi

Wewe ulishapangiwa mpala fate yako, kila kinachotokea kwako sio bahati mbaya kwasababu ulikwisha andikiwa.

Huna option ya kubadilisha chochote, sasa hiyo free will iko wapi?

Mungu akishakuona wewe ni wamotoni, kupitia free will yako unaweza kuwa na option ya kwenda peponi?

Hiyo ndio tunasema Mungu alimuumba mtu akiwa tayari ni muovu, muovu ambaye Mungu alijua kuwa atakuja kuua mtoto asiye na hatia

Lakini bado Mungu akamuacha mtu huyo aje aue mtoto huyo asiye na hatia

Najua utasema amemuavha mtu huyo aje afanye hivyo kwasababu amepewa free will na Mungu hawezi kuingilia free will ya mtu

Lakini unazungumziaje free will ya mtoto anayekwenda kuuliwa?

Kwa namna gani hiyo mtoto ameweza kutumia freewill kati ya kuchagua kuuliwa na huyo muovu au lah?

Kama ubaya unaweza kufanyika bila agreements ya free will kutoka pande mbili basi ni wazi hatuna hiyo free will
 
Unakuwaje na uhuru wa kuchagua kama tayari umeshapangiwa?

Unaambiwa chagua jibu sahihi kati ya yafuatayo;
Rais wa kwanza wa Tanzania ni:
(a) Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Hapo unachagua nini sasa?
Mwalimu ambaye anajua majibu utayoenda kuchagua kabla hajakupa mtihani, anasababu yeyote ya kukupa huo mtihani?

Anakupa mtihani ili ajue nini?

Akishajua kuwa topic hii hujaelewa na kwamba hata ukipewa mtihani hutafaulu, anaweza kukupa mtihani kwa kutegemea tofauti na alivyoona?
 
Nakumbuka uliwahi kunimind kutumia mfano wa baba na mtoto lakini sidhani kama nitaacha. Nitaachaje sasa wakati hata Yesu mwenyewe alipenda kutumia mfanano wa namna iyo hiyo? Mimi kama mfuasi wake nitaendelea kuiga mfano wake.

Wakati ambapo Baba hajamuamini kikamilifu mwanae anaruhusiwa kutumia vitisho. Kusema hajamuamini nadhani ni makosa, tuseme amemuamini kuwa anaweza kuwa mtu mzuri. Ila kwa wakati huo bado hajaamini uwezo wa akili yake kufanya maamuzi sahihi. Anajua fika kwamba mwanae bado hana ujuzi sahihi tayari bali mtoto ako na ujinga mwingi. Atamtisha, atamchapa atamlazimisha kutii baadhi ya vitu. Na hii ni sehemu ya uzoefu utakaomjenga kuweza kuaminika baadaye kadri elimu/ujuzi/uzoefu wake unavyokua.

Lakini akikua ndio utamuacha ajiamulie. Unaamini sasa anao ujuzi wa kutosha na uzoefu unaofaa anaweza kuamua kufanya vema kwa upendo na kuyafaidi matokeo yake!

Ndiyo Mungu anajua kila kitu, na anajua hadi kwamba hii ndio njia nzuri zaidi ya kupitia sisi wanaye ili tuyafurahie maisha mazuri. Wewe mwenye ujuzi pungufu ndio umeshindwa kun'gamua hilo.

Hata tukirudi kwenye mifano usiyoipenda: Kumpatia mwanao starehe moja kwa moja ni kumuharibu. Hata ukijidanganya kwamba mwanangu hana haja ya kujifunza kushughulika sana kisa mimi babaake tayari nina mali nitamrithisha kampuni, bado humtendei haki. Utashangaa hapati njaa, wala kiu ya pesa ila anapata vigonjwa vya kijinga mara depression. Hafurahii mali yake I mean mali yako vizuri. Lakini kama ungempa mazingira ya kuitafuta mali na kuexperience upatikanaji wake atakuwa na furaha kinyama, maana ameipata mali yake sio kopi ya mali ya baba. Labda na Mungu anatupa nafasi ya kuutafuta utakatifu ili tutakapouexperience tuufaudu kinyama.

Hata ukiitazama biblia kuna evolution ya jinsi watu wanamchukulia Mungu kuanzia kimsingi jitu lenye nguvu la kutisha kwenda li jaji lenye haki kamili hadi hapa mwishoni kuwa baba mwenye upendo na rehema na neema😊
 
Hakuna mipaka, kuna matokeo ya uamuzi wetu.
Mipaka ipo. Ndio maana wote waliovuka mipaka Mungu aliingilia kati. Mfano mmojawapo ni Yona. Hakutaka kwenda kuhubiri Ninawi, kwa utashi wake akaamua kwenda Tarshishi. Mungu angeweza kumwacha afanye kwa utashi wake ili avune matokeo ya ubishi wake. Lakini akaingilia kati akampa kichapo mpaka akakubali kwenda Ninawi kinyume na utashi wake.

Mungu haku abdicate mamlaka yake. Mamlaka yake yako juu sana ya utashi wetu.

Matokeo ya uamuzi wetu ni sahihi, tunavuna tulichopanda.
 
Not really.
Please explain how a sovereign man can exist with a Sovereign God.
Who rules over who? They can't be equals or else God will not be really a God or man a man. If God rules over man then man isn't sovereign. And if man rules over God how can He be God?

Please explain how it works!

Note the definition:
sovereignty
noun

sov·er·eign·ty | \ ˈsä-v(ə-)rən-tē , -vərn-tē also ˈsə- \
variants: or less commonly sovranty
plural sovereignties also sovranties

Definition of sovereignty
1a: supreme power especially over a body politic
b: freedom from external control : AUTONOMY
c: controlling influence
2: one that is sovereign especially : an autonomous state
3: obsolete : supreme excellence or an example of it


We were created in the image and likeness of God.
True but we were not created gods.

Just as how God is sovereign, so we are.
No man is sovereign! If you debate that, I will be waiting for an answer to the first point/

This is the reason for the existence of our free will.
We have free will because God allowed us to choose things.
He have power to override our choices any times He wishes!

We were created sovereign.
No, we were not! If you debate it, prove it (see point 1)
 
Huyo baba anakuwa na uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kiasi ashindwe namna ya kufanya mwanae aende katika mienendo anayoitaka?
 
Huyo baba anakuwa na uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kiasi ashindwe namna ya kufanya mwanae aende katika mienendo anayoitaka?
Hata kama angekuwa na huo uwezo wote na ujuzi wote hiyo sio njia ya kuiexpress power/uwezo wake.

Mungu anatufundisha kuwa 'power is best expressed through love' otherwise hakuna anayefaidi sana iwe upande wa mtawala au mtawaliwa.

Au ndugu yangu Scars wewe binafsi unapenda sana kuwa karoboti kakuendeshwa. Je hujiamini kuwa unaweza kufanya maamuzi sahihi kwa hiyo unaona ni bora tu kama kuna anayejua zaidi yako akuendeshage tu. Je huupendi ubinadamu wako?
 
Baba anakosea, sio mara zote anaweza kuwa sahihi

Baba ni kiumbe duni, hana upendo wote kwani ni mara ngapi katika jamii tumeshuhudia ukatiri wa wazazi kwa watoto?

Mfano wako wa baba hauna nguvu katika kutetea hoja kuhusu Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote
 
Sifikirii kama kuna mfano mzuri zaidi ya huo.
 
Sifikirii kama kuna mfano mzuri zaidi ya huo.
Ni kweli hakuna mfano zaidi ya huo kwasababu hakuna namna utaelezea swala la kitu chenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kikasirishwe na matendo yanayofanywa na kiumbe ambacho kipo chini ya uwezo wake bila contradiction
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…