God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Ukweli ni kwamba will, ipo, limited will ipo na free will pia ipo.

Kwa kutumia kanuni za uhusiano/uwiano/relativity hii ambayo tunaiona freewill kwetu bado ni limited will ukipanda katika nyanda za juu yake zaidi halafu ukaitazama.

Lakini for all intents and purpose in this existance, this reality ambayo wengine wanaita illusion hiyo limited will ni free kabisa! Kulingana na mambo tunayopaswa kuchagua huku duniani.

Kwa waliokubali kuwa watoto wa Mungu in fact hicho kitu hata hakiumi yaani kwanza ni raha iliyoje kuwekewa mipaka na unayemuamini[trust] kwamba yote anayofanya ni kwa ajili ya wema kwetu sote. Freedom yetu itazidi kuongezeka kadri tunavyokuwa karibu na Mungu. Sema kufikia freedom aliyonayo yeye[infinity freewill] itachukua umilele [takes eternity to achieve] and that is a good thing! it means we will remain His children all the way for eternity😊

Kukataa kwako Mungu asikupangie mipaka ni dalili tu ya kuwa hujamuamini. Rudisha uaminifu kama yeye alivyokuamini kuwa unaweza kufanya maamuzi sahihi katika mipaka alokuwekea kwa sasa. Muamini sasa na kadri unavyokua mnazidi kuaminiana na kupeana uhuru zaidi.

Hili jambo sio geni, waangalie wanandoa wachanga na kadri wanavyoishi wanazidi kupanua mipaka. Huo mfano[wa wanandoa] sio mtamu sana ukilinganisha na wa baba na watoto wake ambao upo more closer to perfection in representantion of Gods love to man.
 
Kusuma Mungu yupo bila kuthibitisha kivipi yupo haifanyi awepo

Thibitisha yupo kwanza hayo mengine yatafuata
 
Unajuaje kwamba hata hiyo infinity yenyewe si illussion?
Kujua kuwa ni illusion au sio illusion kwangu hainiathiri tena. In fact nilishafikia mkataa wa kuishi ninavyoishinhata kama tupo katika illusion full scale, au reality full scale.

Kuna wajinga fulani sasa hivi wanafanya kampeni ya kukufanya uchanganyikiwe na uone kuwa kuchanganyikiwa huko ni normal tu.

Mtu akikwambia reality ni tofauti katika quantum scale physics [ninazifahamu kiujumlajumla pia] na ukakubali mojakwamoja bila kutafuta namna ya kuziunganisha na uhalisia ili kuipata harmonized/syncronized reality as we know it [actually as you know it]. Unataka kukubali kuchanganyikiwa na uone ni sahihi kwa sababu tu kila kitu hakina maana wala [errting is meaningless bro]

Hapohapo uone kwamba huko kutokuwa na maana ndio kunaleta maana zaidi na unaamua kufuata hizo swaga. Jambo ambalo ni paradoxical! If everything is meaningless why and how do you find meaning[sense] in that meaninglessness!!!!. Yaani kama hakuna chenye maana the unatumia nini kuichukulia hiyo sentensi kuwa ni sahihi???

Hata kama kila kitu ni illusion basi sawa ni illusion full scale hadi hilo suala la kwamba hicho kitu ni illusion up to infinity, ambayo nayo ni illusion. Lakini wacha tuishi humo maana ndimo tulimomo na kanuni zake tupo tunaziishi. So be it.

Kimsingi ukiwa na Roho wa Mungu quantum physics itakusaidia kumjua Mungu zaidi, kuijua freewill zaidi [conscious being's observation affects reality in those scales that he considers so small - RELATIVELY/Relativity]. Ukiwa na Mungu unaweza hata kusoma kitabu cha shetani/uchawi na ukamjua Mungu. Na ukijichagua kuwa sio wa Mungu hadi misahafu utakutamo vitu viovu kinyama. We make our realities be. It is a choice - Free- will
 
Napenda sana analogy ya namna hii

Kwasababu iaanza na kwaku assume, basi wacha tu assume kuwa ni kweli Mungu yupo

Tutumie analogy hiyo hiyo ku question sifa za Mungu

Mungu huyu ni omnipotent, omnibenevolent na pia ni omniscient

Omnipotent: ana nguvu ya kuzuia maovu yasiweze kutokea

omnibenevolent: ana upendo wote na mwenye utayari wa kuzuia mabaya

Omniscient: Mwenye ujuzi wote wa kuelewa ni njia gani uovu unaweza ukapenya, na mwenye kujua ni njia gani ambayo inaweza kuzuia huo uovu

Mungu mwenye kujua njia zote ambazo dhambi na maovu yanaweza yakaja kutokea, Mungu mwenye uwezo wa kuzuia hayo yote yasiwepo, mwenye kila sababu ya kufanya hivyo angezuia maovu yasiwepo.

Kama kungekua na Mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na muweza wa yote basi uovu usingekuwepo

Uovu upo. Hiyo inamaanisha hauwezi kuwa na vyote viwili kwa mpigo (contradiction) yani kuwepo na uovu halafu at the same time kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote

Uovu unathibitisha Mungu huyo hayupo
 
Kusuma Mungu yupo bila kuthibitisha kivipi yupo haifanyi awepo

Thibitisha yupo kwanza hayo mengine yatafuata
Almost yote ninayoyaona na ninayoyashuhudia yanaendana na Mungu yupo, maisha yangu yooooote nitaendelea kuthibitisha.

Amini[trust] kwanza kilichopo halafu ndio tuendelee wote kumtafuta Mungu. Ndio kazi yetu hapa duniani mzee
 
Ndiyo maana nakwambia hivi unazeeka vibaya, uliweka hizo aya na mimi nikakuongezea aya nyingine kuhusu nguzo hiyo. Sasa usirudie jambo ambalo liko wazi.

Swali langu rahisi sana, nenda katika ule uzi utuonyeshe namna ya kusali na kutoa zaka katika Qur'aan. Hili mpaka unakufa.

Naomba uniambie ni maswali gani hayo ambayo nimeshindwa kumjibu na majibu yake yapi kwenye Qur'aan, ili nipate faida.
 
Anhaa, umepata taabu kwa sababu moja tu ya kuweka kama Mungu ako anachukia uovu yaani angeweza angeufuta tu usiwepo kwa waja wake. Wrong.

Kwa kuanzia tujue kwamba mpaka sasa concept/taswira/picha ya Mungu tuliyofikia ni upendo na uwezo usio na kikomo, na ujuzi usio na kikomo. Ukicontrast na sie, mimi na wewe tuna ukomo katika hayo mambo yote.

Unapokaa wewe na Kiranga halafu mkajiona kuwa mna akili sana naujuzi wote kiasi kwamba mnajua kuwa uovu ni mbaya for all intents and purpose mkaona mko sahihi kuliko Mungu mnajidanganya. Yeye anajua zaidi.

Mimi na nyie wote ni watoto, katika utoto wetu tunaweza kukubaliana kabisa kwamba viboko havifai, na baba anapaswa kutupatia kila kitu, na atupe sasa hivi [no delay] tukaona ni sahihi tunajidanganya. Ndiyo naweza nikaungana na nyie kwamba uovu ni kitu kibaya kwa mwisho wa utashi wetukwa sasa. Lakini nikifikiri hata hili suala la muda, kutuwekea kwamba tunaexperience mambo fulani kulingana na muda kadri tunavyokua naamini yu sahihi. I trust HIM

Maswali yenu yanaonesha hampendi kukua, hampendi hata kuishi sasa as a result. Maana yake maisha yanajumuisha kila siku kukua na kupata experience mpya na kupambana na vichangamoto vidogovidogo vinavyotaka kutusambaratisha. Sasa imagine unatokea na kila kitu then unaishi ili iweje. Kwa kweli kuweka muda ni akili kuu ya Mwenyewe. Mungu fundi😊💪, asante sana.
 
Almost yote ninayoyaona na ninayoyashuhudia yanaendana na Mungu yupo, maisha yangu yooooote nitaendelea kuthibitisha.

Amini[trust] kwanza kilichopo halafu ndio tuendelee wote kumtafuta Mungu. Ndio kazi yetu hapa duniani mzee
Anecdotal fallacy inatumika kupumbaza nguvu ya hoja lakini kwa bahati mbaya hoja za namna hiyo hazijawahi kuwa na hitimisho lililotokana na uthibitisho wala uchunguzi

Mtu anaye amua kuangukia kuamini kwenye "Anecdotal fallacy "(personal experience) kwa ku present mifano michache (ambayo nayo hiyo hawezi kuithibitisha kuwa imesababishwa na hicho chanzo anachotaka kukithibitisha)

Kwenye ishu hii ubongo umeamua kuchagua vitu simple ili usijchoshe kwa kukusanya kusanya vi stori vya hapa na pale kuliko uthibitisho unaopimika au logical arguments ambazo ni complex ambazo zinahitaji ufikiriaji wa kina.
 
Katika hoja yangu, swala la Mungu kuchukia uovu hilo ni jambo la baadaye

Nasema ni jambo la baadaye kwasababu hoja ime base kabla hata ya uovu kuanza kutokea, hoja ime base katika sifa zake ambazo zina pingana na uovu.

Ukilazimisha uovu na Mungu vichangamane, hapo utakuwa unaikubali pembe tatu duara ya Kiranga
 
Hii mada huwezi kuijadili Bila kugusia maarifa kutoka ktk Dini,nitachangia Kwa Imani ya Dini yangu ya kiislamu sio lazima ukubaliane nayo Ila ni kupanua uelewa wako Tu.
Ktk Uislamu Malaika hawamuasi Mungu kamwe Kwa kuwa wameumbwa hivyo,wao ni watiifu na wanatekeleza maagizo ya Mola wao,baada ya Adam kuumbwa,Mwenyezi Mungu aliwaambia Malaika wamsujidie Adamu kama sijida ya utii na si Ile ya ibada kwakuwa ni Mungu pekee ndo anasujudiwa.

Sasa Malaika wote walimsujudia Adam isipokuwa Ibilisi,na Ibilisi hakuwa Malaika Bali ni miongoni mwa Majini,kwahiyo Kwa Imani ya kiislamu Malaika hawana free will,Ila Majini na wanadamu Wana free will.

Nije sasa je Mungu hajui kuwa mwanadamu atafanya makosa au atafanya mazuri?
Mungu anajua mwisho wa kila kiumbe chake utakuwaje,si kwamba amepanga iwe hivyo Ila anajua kesho yetu itakuwaje,na kama angepanga Fulani aingie Motoni na Fulani aingie peponi basi hakuwa na haja ya kuleta mitume wake na vitabu vyake kwakuwa visingesaidia kitu kwakuwa tayar ilishapangwa hivyo.

Na kuonyesha kuwa bado Mungu anatupenda na kutaka kuingia peponi,anatupa nafasi ya kutubu makosa yetu kama alivyopokea toba ya Baba yetu Adamu,na yeye ndie aliyemfundisha Adamu maneno hayo ya kutubu,lkn Ibilisi Kwa kiburi chake hakuomba toba ndo akahukumiwa upotofu,na hii maana yake nini,ina maana Ibilisi asingekuja kamwe kuwa mwema na ndo maana ataingia Motoni.

Na Mungu anasema hata mdhulumu mtu hata kama kafanya jema dogo kama chembe ya hadari atalipwa malipo yake na akifanya ubaya vilevile,je kama amekitambulisha hivyo iweje Leo aje amhukumu mwanadamu aingie Motoni wakati huo huo awe tayar amesababishia mwanadamu kuwa hivyo? Jibu hapana Kwa kujua kwake Fulani atakuwa peponi na Fulani atakuwa Motoni haimaanishi ameyasababisha hayo Ila anajua matendo yetu ya kila mmoja yatakuwaje.

Nakumbusha tena hii ni Kwa Imani ya Dini yangu sio lazima uikubali,kwahiyo tusitukanane wala kuchafuana,kama hukubaliano nayo Kausha.

Nitaendelea....
 
Mr unaweza kuhisi kuwa nitatishika kwa kuniambia kuwa kitu fulani ni fallacy. Ningetikisika kama ningekuwa kile kipindi ambapo bado naamini kuwa uhalisia ni mmoja tu ila sio sasa.

Hata kama bado naamini katika objective reality, ninaelewa pia inajumuisha uhalisi na uhalali wa personal relative reality. Kwa hiyo kitu kuwa anecdotal au personal wala haitanifanya nione kuwa ni uongo. La.

After all experience yako ni kitu personal, reality ni kitu personal na hata Mungu unahusiana naye personally. Hakuna haja ya kulazimisha objectivity ilhali kila mmoja anayo freewill yake. Baadhi ya mambo basic tunashare ila mengi yao ni personal experience which depend on who do you think you are. Most things arent what they simply are, but most of them are the way you choose to be, the way you are and that is just the way it is.
 
Kila kilichoumbwa na na Mungu ni chema, kuna vitu unavielewa hivyo hata sasa hivi na kuna vitu utaendelea kuvielewa kadri unavyokua katika imani. Usichukulie kuwa evolution ya uelewa wako imekamilika na final. I hope unaikubali evolution?

Anecdote nyingine hii pokea: ni kwamba mimi niliumia sana kwa wakati ule nimejua alternative ya ukweli kwamba Mungu hayupo, tena mara nirudi kwenye kujua kuwa Mungu yupo. Napata tabu kuswitch kati ya hizo reality/illusion mbili kichwa kinauma na sipendi kukosea. Nikajilaumu ni kwa nini nimejifunza alternative mbili ona sasa zinanitesa. Kumbuka hapo mwanzo nilikuwa kama wewe kuamini kuwa reality ni moja tu so wakati naamini nilijua ukweli pekee ni katika kuamini Mungu, Na wakati siamini nilijua kabisa kuwa ukweli ni hayupo na suala la yupo ni uongo. Kimbembe ni nilipogundua uhalisi wa mawazo hayo mawili😥. Kumbe bhana ndio vizuri ili nichague kweli na sio kiotomati kwa kutojua [appeal to ignorance]. And that is a good thing.

Hadi inafika wakati nakubali kwamba kumbe hizi ni 'kweli' mbili ambazo mtu binafsi anaweza kuamua na kuchukua mojawapo na akabakia ni mwenye akili timamu na akapokea sambamba na ukweli anaoupigania. Na kujua kuwa ninao uwezo wa kuchagua yeyote ndio nikapona na furaha ikarudi maradufu.

Kwa kufanya uchaguzi wangu [free-will] nilifurahi mno maana nimekuwa na power/uwezo na nipo na jukumu/responsible na uamuzi wangu. So liberating, the feeling was so liberating. Hapo ndipo nilipoachana na imani potofu kwamba kuna ukweli mmoja tu kwa kila mtu - objective reality. La. Bali kuna expanded objective reality inayojumuisha hadi hizo subjective realities😲. Ukweli ni kwamba reality yako [subjective reality] ndiyo inayorule maisha na kifo.

Ni Mungu ametupa huo uwezo wa kujichagulia reality ambayo sisi binafsi ndio tunaona inafaa. Anatupenda kweli na kuyaruhusu mawazo yetu yatujenge sisi na yatujengee future au no future thereof. Reality unayoiona ndiyo inakuwa reality yote with respect to you.

Braza unaishi dunia yako uliyoipenda zaidi na mimi ninaishi dunia yangu ninayoipenda zaidi. Unao uhuru wa kuchagua kuishi popote uamuzi ni wako - FreeWill.
 
Wapi nimekutisha?

Mi nachallenge hoja yako uliyoipitishia mlango wa nyuma kinyemela na namna isivyo faa kusimama kama uthibitisho kwa kukosa vigezo vya msingi we unakuja kusema nakutisha
 
Unashindwa kuelewa

Mimi nimehoji uwezekano wa Mungu kuumba ulimwengu ambao hauruhusu uovu ilikuwa ni logic kwasababu ya sifa zake

Ukianambia aliumba vitu vyema unakuwa hujaelewa mantiki ya hoja yangu. Kwasababu hoja imeanzia awali ambapo hivyo vitu vyema havijaumbwa, Mungu alikuwa na option ya kuumba ulimwengu usioweza kuruhusu mabaya

Usinambie aliumba vitu vikiwa vyema and brah brah brah, wakati angeumba ulimwengu ambao kwa namna yeyote uovu hauwezekaniki hayo mabaya yasingeweza kutokea

Sababu za kuumba ulimwengu huo usio ruhusu mabaya alikuwa nazo

Alikuwa na ujuzi wote wa kujua ni sehemu gani ambayo mauovu yanaweza kupenya, na kwa ujuzi huo akaweza kujua ni mbinu gani ya kuweza kudhibiti uovu usiwezekane

Kwanini alishindwa kufanya hivyo?
 
Umezungumza
Umezungumza hadithi ambayo haijapata kutokea
 
Ukisema nyumba ni lazima iwe na mjenzi, kitu hakiwezi kutokea chenyewe tu, hapo umekataa uwezekano wa Mungu kuwepo.

Kwa sababu hata Mungu naye atahitaji muumba wake, hawezi kuwepo tu.

Kwa kanuni ileile.
 
Hujafikiri kwamba kuna uwezekano pia wa kumtengeneza character ambaye hayupo kabisa?
 
Huwezi kusema una limited will halafu ukasema una free will.

Hapo ni sawa na kumwmbia mtu anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as ni rangi nyeusi, halafu ukasema umempa uhuru wa kuchagua gari la rangi yoyote.
 
Unachanganya mambo, nani kasema everything is meaningless?

Maana ni nini?

Mungu unaweza kuthibitisha yupo na si hadithi za watu tu za uongo?
 
Kumbe hujanipata pointi yangu....... pointi yangu ni kwamba kila kitu ni chema, kiko na kusudi jema.

Huo unaoita uovu ni mbaya na haufai ----- ni kitu chema! yote memaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…