God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mpaka hapo tu huna freewill. Una limited will.

Ni kama vile unaangalia Netfix, unajiona unachagua movie kwa freewill.

Wakati hizo movies za kuchagua kuna watu wamekuchagulia, nyingine wamekubania huwezi kuziona ili uzichague.

Mwenyewe unajiona una freewill, kumbe watu wamekuwekea mipaka ya kuchagua.

Uko dukani unachagua bidhaa, unajiona una freewill, wakati kuna watu wamekuchagulia cha kuchagua wakakupangia.

Unajiona una uhuru wa kwenda kulia au kushoto kwenye njiapanda, lakini hujui kwamba huna uhuru wa kuruka juu bila usaidizi wa chombo cha kuruka, hapo hujaamua kwa freewill kwenda kulia, umeamua kwa options finyu ulizo nazo.

Hiyo si freewill, hiyo ni limited.
Ukweli ni kwamba will, ipo, limited will ipo na free will pia ipo.

Kwa kutumia kanuni za uhusiano/uwiano/relativity hii ambayo tunaiona freewill kwetu bado ni limited will ukipanda katika nyanda za juu yake zaidi halafu ukaitazama.

Lakini for all intents and purpose in this existance, this reality ambayo wengine wanaita illusion hiyo limited will ni free kabisa! Kulingana na mambo tunayopaswa kuchagua huku duniani.

Kwa waliokubali kuwa watoto wa Mungu in fact hicho kitu hata hakiumi yaani kwanza ni raha iliyoje kuwekewa mipaka na unayemuamini[trust] kwamba yote anayofanya ni kwa ajili ya wema kwetu sote. Freedom yetu itazidi kuongezeka kadri tunavyokuwa karibu na Mungu. Sema kufikia freedom aliyonayo yeye[infinity freewill] itachukua umilele [takes eternity to achieve] and that is a good thing! it means we will remain His children all the way for eternity😊

Kukataa kwako Mungu asikupangie mipaka ni dalili tu ya kuwa hujamuamini. Rudisha uaminifu kama yeye alivyokuamini kuwa unaweza kufanya maamuzi sahihi katika mipaka alokuwekea kwa sasa. Muamini sasa na kadri unavyokua mnazidi kuaminiana na kupeana uhuru zaidi.

Hili jambo sio geni, waangalie wanandoa wachanga na kadri wanavyoishi wanazidi kupanua mipaka. Huo mfano[wa wanandoa] sio mtamu sana ukilinganisha na wa baba na watoto wake ambao upo more closer to perfection in representantion of Gods love to man.
 
This one made no sense, sijaelewa sababu na matokeo yake hapo. Huoni mutual exclusivity ya kinamna fulani hapo.

Ukweli ni kwamba Mungu yupo na freewill ambayo kwa vipimo vya kijuu[sijui kichini] zaidi inaonekana kama limited ni free kabisa for all intents and purpose kwa hapa duniani.
Kusuma Mungu yupo bila kuthibitisha kivipi yupo haifanyi awepo

Thibitisha yupo kwanza hayo mengine yatafuata
 
Unajuaje kwamba hata hiyo infinity yenyewe si illussion?
Kujua kuwa ni illusion au sio illusion kwangu hainiathiri tena. In fact nilishafikia mkataa wa kuishi ninavyoishinhata kama tupo katika illusion full scale, au reality full scale.

Kuna wajinga fulani sasa hivi wanafanya kampeni ya kukufanya uchanganyikiwe na uone kuwa kuchanganyikiwa huko ni normal tu.

Mtu akikwambia reality ni tofauti katika quantum scale physics [ninazifahamu kiujumlajumla pia] na ukakubali mojakwamoja bila kutafuta namna ya kuziunganisha na uhalisia ili kuipata harmonized/syncronized reality as we know it [actually as you know it]. Unataka kukubali kuchanganyikiwa na uone ni sahihi kwa sababu tu kila kitu hakina maana wala [errting is meaningless bro]

Hapohapo uone kwamba huko kutokuwa na maana ndio kunaleta maana zaidi na unaamua kufuata hizo swaga. Jambo ambalo ni paradoxical! If everything is meaningless why and how do you find meaning[sense] in that meaninglessness!!!!. Yaani kama hakuna chenye maana the unatumia nini kuichukulia hiyo sentensi kuwa ni sahihi???

Hata kama kila kitu ni illusion basi sawa ni illusion full scale hadi hilo suala la kwamba hicho kitu ni illusion up to infinity, ambayo nayo ni illusion. Lakini wacha tuishi humo maana ndimo tulimomo na kanuni zake tupo tunaziishi. So be it.

Kimsingi ukiwa na Roho wa Mungu quantum physics itakusaidia kumjua Mungu zaidi, kuijua freewill zaidi [conscious being's observation affects reality in those scales that he considers so small - RELATIVELY/Relativity]. Ukiwa na Mungu unaweza hata kusoma kitabu cha shetani/uchawi na ukamjua Mungu. Na ukijichagua kuwa sio wa Mungu hadi misahafu utakutamo vitu viovu kinyama. We make our realities be. It is a choice - Free- will
Time ni illussion, to a photon that travels at the speed of light, time does not exist.

Cause and effect is an illussion.

In quantum physics, it is possible to have effects before causes and causes after effects in a crazily cyclical way.

Nimepost links hapo juu.

Sasa kama hata time na cause and effects ni illussions, how could free will be true?
 
Nadhani nilikuwa naelekea kusinzia pia, ila wazo la jumla ilikuwa ni: ikiwa ninao uthibitisho wa baadhi ya sifa hivyo basi nitachukulia kitu ninachokifikiria ndiyo hicho hadi pale nitakapokithibitisha kikamilifu. Au mpango mzima utaabort ikiwa nitapata sifa itakayothibitisha kinyume na ninachowaza.

Mfano kama nikinunua kioo nikakata kwa hilo jiwe - nitathibitisha ni almasi [assume ni gold standard]
Nikiona almasi imepitisha umeme hata kabla sijaikatia kioo basi nitajua- sio almasi. Eaasy.

Ila mind you kuwa kwake almasi au kutokuwa almasi hakubadilishi kuwa ni kitu cha thamani maana kina kazi ninayoiona ni nzuri kabisa kwangu. Kama wewe ni mmoja wa wasioweza kuvalue kitu hadi kithaminishwe kwa pesa ndio utapata tabu kunielewa.
Napenda sana analogy ya namna hii

Kwasababu iaanza na kwaku assume, basi wacha tu assume kuwa ni kweli Mungu yupo

Tutumie analogy hiyo hiyo ku question sifa za Mungu

Mungu huyu ni omnipotent, omnibenevolent na pia ni omniscient

Omnipotent: ana nguvu ya kuzuia maovu yasiweze kutokea

omnibenevolent: ana upendo wote na mwenye utayari wa kuzuia mabaya

Omniscient: Mwenye ujuzi wote wa kuelewa ni njia gani uovu unaweza ukapenya, na mwenye kujua ni njia gani ambayo inaweza kuzuia huo uovu

Mungu mwenye kujua njia zote ambazo dhambi na maovu yanaweza yakaja kutokea, Mungu mwenye uwezo wa kuzuia hayo yote yasiwepo, mwenye kila sababu ya kufanya hivyo angezuia maovu yasiwepo.

Kama kungekua na Mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na muweza wa yote basi uovu usingekuwepo

Uovu upo. Hiyo inamaanisha hauwezi kuwa na vyote viwili kwa mpigo (contradiction) yani kuwepo na uovu halafu at the same time kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote

Uovu unathibitisha Mungu huyo hayupo
 
Kusuma Mungu yupo bila kuthibitisha kivipi yupo haifanyi awepo

Thibitisha yupo kwanza hayo mengine yatafuata
Almost yote ninayoyaona na ninayoyashuhudia yanaendana na Mungu yupo, maisha yangu yooooote nitaendelea kuthibitisha.

Amini[trust] kwanza kilichopo halafu ndio tuendelee wote kumtafuta Mungu. Ndio kazi yetu hapa duniani mzee
 
Naam, wala hujakosea, ikiwa tu, utajibu maswali yangu ntaelewa sasa yamekuingia ntasogea mbele.

Nimekwambia wewe upo kibishi siyo kiusomi. Huna haja ya kuelewa. Mara nyingi hata Kiranga humu anakuuliza maswali unashndwa kuyajibu wakati majibu yake yote yapo kwenye Qur'an, wazi kabisa.

Unashindwa kuelewa na kukubali kuwa Qur'an ndiyo "guidance" aliyopewa Mtume Muhammad pekee kupambana na Wasioamini Mungu. Na humo ndani yake kuna visa vingi sana vya mitume wa kabla yake binaletwa kama ilm kwake na kwetu tunapokutana na wasio na dini, wanojiita Wakristo, Wanaojiita Wayahudi, na wale kama wewe ambao wanaamini maneno ya watu na hekaya za kutungwa.

Unashindwa kuielewa Salat ndani ya Qur'an kwa kuwa tu, umejitia loki kichwani mwako.

Narudia...

Umeelewa salat, usizozijuwa wewe, kuwa xzpo kwenyeQur'an, zimeanzia wapi? Kama ilivyoelezwa kwenye Qur'an? Nilikuwekea ushahidi wa Qur'an. Unaukubali unaukataa?

Unaelewa nyakati za salat zote zipo kwenye Qur'an? Nilikuwekea ushahidi wa Qur'an, unaukubali au unaukataa.

Anza kwa kujibu hayo, hakuna mipaka ya kukufundisha, mpaka utapoyajibu hayo ntaendelea. Usiiogope Qur'an. Kuiogopa Qur'an ni ushetani, mashtani yanapoisikia Qur'an ndiyo huikimbia, kama unavyoikimbia wewe kwa maswali simpo ya akida.

Haya ondoa ufinyu wako, uyajibu hayo ili niendelee kukutoa minyororo uliyojizonga nayo kwenye ubongo wako.

Anzia hapa;" La yamlikuna minhu khitaba".
Ndiyo maana nakwambia hivi unazeeka vibaya, uliweka hizo aya na mimi nikakuongezea aya nyingine kuhusu nguzo hiyo. Sasa usirudie jambo ambalo liko wazi.

Swali langu rahisi sana, nenda katika ule uzi utuonyeshe namna ya kusali na kutoa zaka katika Qur'aan. Hili mpaka unakufa.

Naomba uniambie ni maswali gani hayo ambayo nimeshindwa kumjibu na majibu yake yapi kwenye Qur'aan, ili nipate faida.
 
Napenda sana analogy ya namna hii

Kwasababu iaanza na kwaku assume, basi wacha tu assume kuwa ni kweli Mungu yupo

Tutumie analogy hiyo hiyo ku question sifa za Mungu

Mungu huyu ni omnipotent, omnibenevolent na pia ni omniscient

Omnipotent: ana nguvu ya kuzuia maovu yasiweze kutokea

omnibenevolent: ana upendo wote na mwenye utayari wa kuzuia mabaya

Omniscient: Mwenye ujuzi wote wa kuelewa ni njia gani uovu unaweza ukapenya, na mwenye kujua ni njia gani ambayo inaweza kuzuia huo uovu

Mungu mwenye kujua njia zote ambazo dhambi na maovu yanaweza yakaja kutokea, Mungu mwenye uwezo wa kuzuia hayo yote yasiwepo, mwenye kila sababu ya kufanya hivyo angezuia maovu yasiwepo.

Kama kungekua na Mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na muweza wa yote basi uovu usingekuwepo

Uovu upo. Hiyo inamaanisha hauwezi kuwa na vyote viwili kwa mpigo (contradiction) yani kuwepo na uovu halafu at the same time kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote

Uovu unathibitisha Mungu huyo hayupo
Anhaa, umepata taabu kwa sababu moja tu ya kuweka kama Mungu ako anachukia uovu yaani angeweza angeufuta tu usiwepo kwa waja wake. Wrong.

Kwa kuanzia tujue kwamba mpaka sasa concept/taswira/picha ya Mungu tuliyofikia ni upendo na uwezo usio na kikomo, na ujuzi usio na kikomo. Ukicontrast na sie, mimi na wewe tuna ukomo katika hayo mambo yote.

Unapokaa wewe na Kiranga halafu mkajiona kuwa mna akili sana naujuzi wote kiasi kwamba mnajua kuwa uovu ni mbaya for all intents and purpose mkaona mko sahihi kuliko Mungu mnajidanganya. Yeye anajua zaidi.

Mimi na nyie wote ni watoto, katika utoto wetu tunaweza kukubaliana kabisa kwamba viboko havifai, na baba anapaswa kutupatia kila kitu, na atupe sasa hivi [no delay] tukaona ni sahihi tunajidanganya. Ndiyo naweza nikaungana na nyie kwamba uovu ni kitu kibaya kwa mwisho wa utashi wetukwa sasa. Lakini nikifikiri hata hili suala la muda, kutuwekea kwamba tunaexperience mambo fulani kulingana na muda kadri tunavyokua naamini yu sahihi. I trust HIM

Maswali yenu yanaonesha hampendi kukua, hampendi hata kuishi sasa as a result. Maana yake maisha yanajumuisha kila siku kukua na kupata experience mpya na kupambana na vichangamoto vidogovidogo vinavyotaka kutusambaratisha. Sasa imagine unatokea na kila kitu then unaishi ili iweje. Kwa kweli kuweka muda ni akili kuu ya Mwenyewe. Mungu fundi😊💪, asante sana.
 
Almost yote ninayoyaona na ninayoyashuhudia yanaendana na Mungu yupo, maisha yangu yooooote nitaendelea kuthibitisha.

Amini[trust] kwanza kilichopo halafu ndio tuendelee wote kumtafuta Mungu. Ndio kazi yetu hapa duniani mzee
Anecdotal fallacy inatumika kupumbaza nguvu ya hoja lakini kwa bahati mbaya hoja za namna hiyo hazijawahi kuwa na hitimisho lililotokana na uthibitisho wala uchunguzi

Mtu anaye amua kuangukia kuamini kwenye "Anecdotal fallacy "(personal experience) kwa ku present mifano michache (ambayo nayo hiyo hawezi kuithibitisha kuwa imesababishwa na hicho chanzo anachotaka kukithibitisha)

Kwenye ishu hii ubongo umeamua kuchagua vitu simple ili usijchoshe kwa kukusanya kusanya vi stori vya hapa na pale kuliko uthibitisho unaopimika au logical arguments ambazo ni complex ambazo zinahitaji ufikiriaji wa kina.
 
Anhaa, umepata taabu kwa sababu moja tu ya kuweka kama Mungu ako anachukia uovu yaani angeweza angeufuta tu usiwepo kwa waja wake. Wrong.

Kwa kuanzia tujue kwamba mpaka sasa concept/taswira/picha ya Mungu tuliyofikia ni upendo na uwezo usio na kikomo, na ujuzi usio na kikomo. Ukicontrast na sie, mimi na wewe tuna ukomo katika hayo mambo yote.

Unapokaa wewe na Kiranga halafu mkajiona kuwa mna akili sana naujuzi wote kiasi kwamba mnajua kuwa uovu ni mbaya for all intents and purpose mkaona mko sahihi kuliko Mungu mnajidanganya. Yeye anajua zaidi.

Mimi na nyie wote ni watoto, katika utoto wetu tunaweza kukubaliana kabisa kwamba viboko havifai, na baba anapaswa kutupatia kila kitu, na atupe sasa hivi [no delay] tukaona ni sahihi tunajidanganya. Ndiyo naweza nikaungana na nyie kwamba uovu ni kitu kibaya kwa mwisho wa utashi wetukwa sasa. Lakini nikifikiri hata hili suala la muda, kutuwekea kwamba tunaexperience mambo fulani kulingana na muda kadri tunavyokua naamini yu sahihi. I trust HIM

Maswali yenu yanaonesha hampendi kukua, hampendi hata kuishi sasa as a result. Maana yake maisha yanajumuisha kila siku kukua na kupata experience mpya na kupambana na vichangamoto vidogovidogo vinavyotaka kutusambaratisha. Sasa imagine unatokea na kila kitu then unaishi ili iweje. Kwa kweli kuweka muda ni akili kuu ya Mwenyewe. Mungu fundi😊💪, asante sana.
Katika hoja yangu, swala la Mungu kuchukia uovu hilo ni jambo la baadaye

Nasema ni jambo la baadaye kwasababu hoja ime base kabla hata ya uovu kuanza kutokea, hoja ime base katika sifa zake ambazo zina pingana na uovu.

Ukilazimisha uovu na Mungu vichangamane, hapo utakuwa unaikubali pembe tatu duara ya Kiranga
 
Hii mada huwezi kuijadili Bila kugusia maarifa kutoka ktk Dini,nitachangia Kwa Imani ya Dini yangu ya kiislamu sio lazima ukubaliane nayo Ila ni kupanua uelewa wako Tu.
Ktk Uislamu Malaika hawamuasi Mungu kamwe Kwa kuwa wameumbwa hivyo,wao ni watiifu na wanatekeleza maagizo ya Mola wao,baada ya Adam kuumbwa,Mwenyezi Mungu aliwaambia Malaika wamsujidie Adamu kama sijida ya utii na si Ile ya ibada kwakuwa ni Mungu pekee ndo anasujudiwa.

Sasa Malaika wote walimsujudia Adam isipokuwa Ibilisi,na Ibilisi hakuwa Malaika Bali ni miongoni mwa Majini,kwahiyo Kwa Imani ya kiislamu Malaika hawana free will,Ila Majini na wanadamu Wana free will.

Nije sasa je Mungu hajui kuwa mwanadamu atafanya makosa au atafanya mazuri?
Mungu anajua mwisho wa kila kiumbe chake utakuwaje,si kwamba amepanga iwe hivyo Ila anajua kesho yetu itakuwaje,na kama angepanga Fulani aingie Motoni na Fulani aingie peponi basi hakuwa na haja ya kuleta mitume wake na vitabu vyake kwakuwa visingesaidia kitu kwakuwa tayar ilishapangwa hivyo.

Na kuonyesha kuwa bado Mungu anatupenda na kutaka kuingia peponi,anatupa nafasi ya kutubu makosa yetu kama alivyopokea toba ya Baba yetu Adamu,na yeye ndie aliyemfundisha Adamu maneno hayo ya kutubu,lkn Ibilisi Kwa kiburi chake hakuomba toba ndo akahukumiwa upotofu,na hii maana yake nini,ina maana Ibilisi asingekuja kamwe kuwa mwema na ndo maana ataingia Motoni.

Na Mungu anasema hata mdhulumu mtu hata kama kafanya jema dogo kama chembe ya hadari atalipwa malipo yake na akifanya ubaya vilevile,je kama amekitambulisha hivyo iweje Leo aje amhukumu mwanadamu aingie Motoni wakati huo huo awe tayar amesababishia mwanadamu kuwa hivyo? Jibu hapana Kwa kujua kwake Fulani atakuwa peponi na Fulani atakuwa Motoni haimaanishi ameyasababisha hayo Ila anajua matendo yetu ya kila mmoja yatakuwaje.

Nakumbusha tena hii ni Kwa Imani ya Dini yangu sio lazima uikubali,kwahiyo tusitukanane wala kuchafuana,kama hukubaliano nayo Kausha.

Nitaendelea....
 
Anecdotal fallacy inatumika kupumbaza nguvu ya hoja lakini kwa bahati mbaya hoja za namna hiyo hazijawahi kuwa na hitimisho lililotokana na uthibitisho wala uchunguzi

Mtu anaye amua kuangukia kuamini kwenye "Anecdotal fallacy "(personal experience) kwa ku present mifano michache (ambayo nayo hiyo hawezi kuithibitisha kuwa imesababishwa na hicho chanzo anachotaka kukithibitisha)

Kwenye ishu hii ubongo umeamua kuchagua vitu simple ili usijchoshe kwa kukusanya kusanya vi stori vya hapa na pale kuliko uthibitisho unaopimika au logical arguments ambazo ni complex ambazo zinahitaji ufikiriaji wa kina.
Mr unaweza kuhisi kuwa nitatishika kwa kuniambia kuwa kitu fulani ni fallacy. Ningetikisika kama ningekuwa kile kipindi ambapo bado naamini kuwa uhalisia ni mmoja tu ila sio sasa.

Hata kama bado naamini katika objective reality, ninaelewa pia inajumuisha uhalisi na uhalali wa personal relative reality. Kwa hiyo kitu kuwa anecdotal au personal wala haitanifanya nione kuwa ni uongo. La.

After all experience yako ni kitu personal, reality ni kitu personal na hata Mungu unahusiana naye personally. Hakuna haja ya kulazimisha objectivity ilhali kila mmoja anayo freewill yake. Baadhi ya mambo basic tunashare ila mengi yao ni personal experience which depend on who do you think you are. Most things arent what they simply are, but most of them are the way you choose to be, the way you are and that is just the way it is.
 
Katika hoja yangu, swala la Mungu kuchukia uovu hilo ni jambo la baadaye

Nasema ni jambo la baadaye kwasababu hoja ime base kabla hata ya uovu kuanza kutokea, hoja ime base katika sifa zake ambazo zina pingana na uovu.

Ukilazimisha uovu na Mungu vichangamane, hapo utakuwa unaikubali pembe tatu duara ya Kiranga
Kila kilichoumbwa na na Mungu ni chema, kuna vitu unavielewa hivyo hata sasa hivi na kuna vitu utaendelea kuvielewa kadri unavyokua katika imani. Usichukulie kuwa evolution ya uelewa wako imekamilika na final. I hope unaikubali evolution?

Anecdote nyingine hii pokea: ni kwamba mimi niliumia sana kwa wakati ule nimejua alternative ya ukweli kwamba Mungu hayupo, tena mara nirudi kwenye kujua kuwa Mungu yupo. Napata tabu kuswitch kati ya hizo reality/illusion mbili kichwa kinauma na sipendi kukosea. Nikajilaumu ni kwa nini nimejifunza alternative mbili ona sasa zinanitesa. Kumbuka hapo mwanzo nilikuwa kama wewe kuamini kuwa reality ni moja tu so wakati naamini nilijua ukweli pekee ni katika kuamini Mungu, Na wakati siamini nilijua kabisa kuwa ukweli ni hayupo na suala la yupo ni uongo. Kimbembe ni nilipogundua uhalisi wa mawazo hayo mawili😥. Kumbe bhana ndio vizuri ili nichague kweli na sio kiotomati kwa kutojua [appeal to ignorance]. And that is a good thing.

Hadi inafika wakati nakubali kwamba kumbe hizi ni 'kweli' mbili ambazo mtu binafsi anaweza kuamua na kuchukua mojawapo na akabakia ni mwenye akili timamu na akapokea sambamba na ukweli anaoupigania. Na kujua kuwa ninao uwezo wa kuchagua yeyote ndio nikapona na furaha ikarudi maradufu.

Kwa kufanya uchaguzi wangu [free-will] nilifurahi mno maana nimekuwa na power/uwezo na nipo na jukumu/responsible na uamuzi wangu. So liberating, the feeling was so liberating. Hapo ndipo nilipoachana na imani potofu kwamba kuna ukweli mmoja tu kwa kila mtu - objective reality. La. Bali kuna expanded objective reality inayojumuisha hadi hizo subjective realities😲. Ukweli ni kwamba reality yako [subjective reality] ndiyo inayorule maisha na kifo.

Ni Mungu ametupa huo uwezo wa kujichagulia reality ambayo sisi binafsi ndio tunaona inafaa. Anatupenda kweli na kuyaruhusu mawazo yetu yatujenge sisi na yatujengee future au no future thereof. Reality unayoiona ndiyo inakuwa reality yote with respect to you.

Braza unaishi dunia yako uliyoipenda zaidi na mimi ninaishi dunia yangu ninayoipenda zaidi. Unao uhuru wa kuchagua kuishi popote uamuzi ni wako - FreeWill.
 
Mr unaweza kuhisi kuwa nitatishika kwa kuniambia kuwa kitu fulani ni fallacy. Ningetikisika kama ningekuwa kile kipindi ambapo bado naamini kuwa uhalisia ni mmoja tu ila sio sasa.

Hata kama bado naamini katika objective reality, ninaelewa pia inajumuisha uhalisi na uhalali wa personal relative reality. Kwa hiyo kitu kuwa anecdotal au personal wala haitanifanya nione kuwa ni uongo. La.

After all experience yako ni kitu personal, reality ni kitu personal na hata Mungu unahusiana naye personally. Hakuna haja ya kulazimisha objectivity ilhali kila mmoja anayo freewill yake. Baadhi ya mambo basic tunashare ila mengi yao ni personal experience which depend on who do you think you are. Most things arent what they simply are, but most of them are the way you choose to be, the way you are and that is just the way it is.
Wapi nimekutisha?

Mi nachallenge hoja yako uliyoipitishia mlango wa nyuma kinyemela na namna isivyo faa kusimama kama uthibitisho kwa kukosa vigezo vya msingi we unakuja kusema nakutisha
 
Kila kilichoumbwa na na Mungu ni chema, kuna vitu unavielewa hivyo hata sasa hivi na kuna vitu utaendelea kuvielewa kadri unavyokua katika imani. Usichukulie kuwa evolution ya uelewa wako imekamilika na final. I hope unaikubali evolution?

Anecdote nyingine hii pokea: ni kwamba mimi niliumia sana kwa wakati ule nimejua alternative ya ukweli kwamba Mungu hayupo, tena mara nirudi kwenye kujua kuwa Mungu yupo. Napata tabu kuswitch kati ya hizo reality/illusion mbili kichwa kinauma na sipendi kukosea. Nikajilaumu ni kwa nini nimejifunza alternative mbili ona sasa zinanitesa. Kumbuka hapo mwanzo nilikuwa kama wewe kuamini kuwa reality ni moja tu so wakati naamini nilijua ukweli pekee ni katika kuamini Mungu, Na wakati siamini nilijua kabisa kuwa ukweli ni hayupo na suala la yupo ni uongo. Kimbembe ni nilipogundua uhalisi wa mawazo hayo mawili😥. Kumbe bhana ndio vizuri ili nichague kweli na sio kiotomati kwa kutojua [appeal to ignorance]. And that is a good thing.

Hadi inafika wakati nakubali kwamba kumbe hizi ni 'kweli' mbili ambazo mtu binafsi anaweza kuamua na kuchukua mojawapo na akabakia ni mwenye akili timamu na akapokea sambamba na ukweli anaoupigania. Na kujua kuwa ninao uwezo wa kuchagua yeyote ndio nikapona na furaha ikarudi maradufu.

Kwa kufanya uchaguzi wangu [free-will] nilifurahi mno maana nimekuwa na power/uwezo na nipo na jukumu/responsible na uamuzi wangu. So liberating, the feeling was so liberating. Hapo ndipo nilipoachana na imani potofu kwamba kuna ukweli mmoja tu kwa kila mtu - objective reality. La. Bali kuna expanded objective reality inayojumuisha hadi hizo subjective realities😲. Ukweli ni kwamba reality yako [subjective reality] ndiyo inayorule maisha na kifo.

Ni Mungu ametupa huo uwezo wa kujichagulia reality ambayo sisi binafsi ndio tunaona inafaa. Anatupenda kweli na kuyaruhusu mawazo yetu yatujenge sisi na yatujengee future au no future thereof. Reality unayoiona ndiyo inakuwa reality yote with respect to you.

Braza unaishi dunia yako uliyoipenda zaidi na mimi ninaishi dunia yangu ninayoipenda zaidi. Unao uhuru wa kuchagua kuishi popote uamuzi ni wako - FreeWill.
Unashindwa kuelewa

Mimi nimehoji uwezekano wa Mungu kuumba ulimwengu ambao hauruhusu uovu ilikuwa ni logic kwasababu ya sifa zake

Ukianambia aliumba vitu vyema unakuwa hujaelewa mantiki ya hoja yangu. Kwasababu hoja imeanzia awali ambapo hivyo vitu vyema havijaumbwa, Mungu alikuwa na option ya kuumba ulimwengu usioweza kuruhusu mabaya

Usinambie aliumba vitu vikiwa vyema and brah brah brah, wakati angeumba ulimwengu ambao kwa namna yeyote uovu hauwezekaniki hayo mabaya yasingeweza kutokea

Sababu za kuumba ulimwengu huo usio ruhusu mabaya alikuwa nazo

Alikuwa na ujuzi wote wa kujua ni sehemu gani ambayo mauovu yanaweza kupenya, na kwa ujuzi huo akaweza kujua ni mbinu gani ya kuweza kudhibiti uovu usiwezekane

Kwanini alishindwa kufanya hivyo?
 
Umezungumza
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Umezungumza hadithi ambayo haijapata kutokea
 
Kashindwa kuthibitisha madai yake na anajaribu ku fabricate uthibitisho hata kwa njia zisizo za halali ili tu kumfanya huyo Mungu wakufikirika aonekane yupo

Mtu anakuambia anathibitisha Mungu yupo kwa self evident truth, anaanza kwa kukuambia self evident truth ni ukweli ambao hauhitaji uthibitisho yani ukiambiwa tu we kubali kuwa ni kweli

Anasema nyumba lazima iwe na mjenzi, hiyo ni self evident truth kwasababu haiwezekani nyumba ikajijenga na kwamba kuhoji kuhusu kivipi isijijenge itakuwa ni ujinga

Halafu anakuambia hivyo hivyo na kwa Mungu, ulimwengu upo na lazima uwe umeumbwa na hiyo ni self evident truth

Hivyo Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu

Rhetorician hapo kafanya makosa mengi katika hoja yake ya kwanza na kuihusisha na mfano wake wa pili

Nyumba tunajua zinajengwa na wajenzi wapo, vifaa vya ujenzi vipo, makampuni ya ujenzi yapo, material ya ujenzi yapo unaweza ukaangalia ukajua haya material yana zalishwa na kampuni gani, na vyote hivyo vinathibitishika. Mtu akisema nyumba imejengwa hiyo ni logic trivial hata kama humjui fundi utakubali kupitia sababu hizo hapo juu

Sasa nani alishawahi kuthibitisha Mungu yupo ili tujue kweli aliumba ulimwengu?

Kampuni gani la ujenzi linajishughulisha na uumbaji wa ulimwengu ili hata tusipomjua muumbaji ni nani tutumie logic trivial kukubali?

Nani alishawahi kushuhudia ulimwengu unavyoumbwa kiasi tuone swala la uumbaji ni logic?

Kuna ulimwengu mwingine uliowahi kushuhudiwa ukiumbwa ili tutumie logic hiyo hiyo kusema huu pia una muumbaji japo hatujui nani?
Ukisema nyumba ni lazima iwe na mjenzi, kitu hakiwezi kutokea chenyewe tu, hapo umekataa uwezekano wa Mungu kuwepo.

Kwa sababu hata Mungu naye atahitaji muumba wake, hawezi kuwepo tu.

Kwa kanuni ileile.
 
Kabisa hata mie nilicontemplate ikiwa ningekuwa exposed na muungu mwingine na mwana wa mungu mwingine au dini nyingine etc uchaguzi bado ningekuwa nao au vipi?.

Upo uwezekano wa kumchukua character halafu ukamvua ubinafsi wake wote ukabakiza tu zile values anazozirepresent na ukatoboa.

Mfano nimejitungia kanuni kuwa kitu kilicho sahihi ni kile ambacho ni 'Of God and For mankind' baada ya hapo sina shida ya kuwajua majina hata watakaonihubiria.

Maneno yasemwe na Mtume, nabii, mwana, mchungaji, muhuni, mpinga Mungu mwenye jina lolote yakiendana na kanuni hiyo ni maneno sahihi. Kwa hiyo nitachagua sifa sahihi za Mungu hata kama amewakilishwa na jina jingine. Uzuri sheria ya Mungu ipo ndani mwetu.

Maneno yasikupe tabu, sura zisikupe tabu hapa tunaongelea thamani/values tu. Mfano mhuni mmoja akafuata kikamilifu kanuni ya 'Dont f**k with me, I wont f**k with you' unadhani hataishi mbinguni huyu mwamba? Sijui lakini huenda..
Hujafikiri kwamba kuna uwezekano pia wa kumtengeneza character ambaye hayupo kabisa?
 
Ukweli ni kwamba will, ipo, limited will ipo na free will pia ipo.

Kwa kutumia kanuni za uhusiano/uwiano/relativity hii ambayo tunaiona freewill kwetu bado ni limited will ukipanda katika nyanda za juu yake zaidi halafu ukaitazama.

Lakini for all intents and purpose in this existance, this reality ambayo wengine wanaita illusion hiyo limited will ni free kabisa! Kulingana na mambo tunayopaswa kuchagua huku duniani.

Kwa waliokubali kuwa watoto wa Mungu in fact hicho kitu hata hakiumi yaani kwanza ni raha iliyoje kuwekewa mipaka na unayemuamini[trust] kwamba yote anayofanya ni kwa ajili ya wema kwetu sote. Freedom yetu itazidi kuongezeka kadri tunavyokuwa karibu na Mungu. Sema kufikia freedom aliyonayo yeye[infinity freewill] itachukua umilele [takes eternity to achieve] and that is a good thing! it means we will remain His children all the way for eternity😊

Kukataa kwako Mungu asikupangie mipaka ni dalili tu ya kuwa hujamuamini. Rudisha uaminifu kama yeye alivyokuamini kuwa unaweza kufanya maamuzi sahihi katika mipaka alokuwekea kwa sasa. Muamini sasa na kadri unavyokua mnazidi kuaminiana na kupeana uhuru zaidi.

Hili jambo sio geni, waangalie wanandoa wachanga na kadri wanavyoishi wanazidi kupanua mipaka. Huo mfano[wa wanandoa] sio mtamu sana ukilinganisha na wa baba na watoto wake ambao upo more closer to perfection in representantion of Gods love to man.
Huwezi kusema una limited will halafu ukasema una free will.

Hapo ni sawa na kumwmbia mtu anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as ni rangi nyeusi, halafu ukasema umempa uhuru wa kuchagua gari la rangi yoyote.
 
Kujua kuwa ni illusion au sio illusion kwangu hainiathiri tena. In fact nilishafikia mkataa wa kuishi ninavyoishinhata kama tupo katika illusion full scale, au reality full scale.

Kuna wajinga fulani sasa hivi wanafanya kampeni ya kukufanya uchanganyikiwe na uone kuwa kuchanganyikiwa huko ni normal tu.

Mtu akikwambia reality ni tofauti katika quantum scale physics [ninazifahamu kiujumlajumla pia] na ukakubali mojakwamoja bila kutafuta namna ya kuziunganisha na uhalisia ili kuipata harmonized/syncronized reality as we know it [actually as you know it]. Unataka kukubali kuchanganyikiwa na uone ni sahihi kwa sababu tu kila kitu hakina maana wala [errting is meaningless bro]

Hapohapo uone kwamba huko kutokuwa na maana ndio kunaleta maana zaidi na unaamua kufuata hizo swaga. Jambo ambalo ni paradoxical! If everything is meaningless why and how do you find meaning[sense] in that meaninglessness!!!!. Yaani kama hakuna chenye maana the unatumia nini kuichukulia hiyo sentensi kuwa ni sahihi???

Hata kama kila kitu ni illusion basi sawa ni illusion full scale hadi hilo suala la kwamba hicho kitu ni illusion up to infinity, ambayo nayo ni illusion. Lakini wacha tuishi humo maana ndimo tulimomo na kanuni zake tupo tunaziishi. So be it.

Kimsingi ukiwa na Roho wa Mungu quantum physics itakusaidia kumjua Mungu zaidi, kuijua freewill zaidi [conscious being's observation affects reality in those scales that he considers so small - RELATIVELY/Relativity]. Ukiwa na Mungu unaweza hata kusoma kitabu cha shetani/uchawi na ukamjua Mungu. Na ukijichagua kuwa sio wa Mungu hadi misahafu utakutamo vitu viovu kinyama. We make our realities be. It is a choice - Free- will
Unachanganya mambo, nani kasema everything is meaningless?

Maana ni nini?

Mungu unaweza kuthibitisha yupo na si hadithi za watu tu za uongo?
 
Unashindwa kuelewa

Mimi nimehoji uwezekano wa Mungu kuumba ulimwengu ambao hauruhusu uovu ilikuwa ni logic kwasababu ya sifa zake

Ukianambia aliumba vitu vyema unakuwa hujaelewa mantiki ya hoja yangu. Kwasababu hoja imeanzia awali ambapo hivyo vitu vyema havijaumbwa, Mungu alikuwa na option ya kuumba ulimwengu usioweza kuruhusu mabaya

Usinambie aliumba vitu vikiwa vyema and brah brah brah, wakati angeumba ulimwengu ambao kwa namna yeyote uovu hauwezekaniki hayo mabaya yasingeweza kutokea

Sababu za kuumba ulimwengu huo usio ruhusu mabaya alikuwa nazo

Alikuwa na ujuzi wote wa kujua ni sehemu gani ambayo mauovu yanaweza kupenya, na kwa ujuzi huo akaweza kujua ni mbinu gani ya kuweza kudhibiti uovu usiwezekane

Kwanini alishindwa kufanya hivyo?
Kumbe hujanipata pointi yangu....... pointi yangu ni kwamba kila kitu ni chema, kiko na kusudi jema.

Huo unaoita uovu ni mbaya na haufai ----- ni kitu chema! yote memaa
 
Back
Top Bottom