God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Ukumbuke kabla ya hukumu ya mwisho sote tutafufuliwa na kupata miili yetu then tuhukumiwe.
 

Mm ndo maana huwa nasema kwa mujibu wa dini mungu ndo shetani mkuu
 

Daah jamaa uko na akili sana inabd uandike kitabu tutanunua
 

Daah watu mnawaza aisee mawazo ambayo sjawah kuwaza n kweli huwez kufurahia wenzio wako
Motoni …, same na hapa dunian ndg hawawez kufurah uende jela
 

Em kaa the soma thread yako kama anajua kila kitu had utakavo kufa freewill ipo wapi
 

Yaan anajua kila kitu chako kama utachange na kama hautachange hapo freewill ipo wapi
 
Mfano wa yuda unafurahisha sana.

Kwanza Bible yesu anatabiri tazama mwana wa afamu atasalitiwa.

Pili humo humo kwenye Bible unakutana mstari ole wake atakayemsaliti masia ni heri asingezaliwa kwa kisanga atakachokutana nacho.

Na je kama yuda asingemsaliti kristo tungepataje wokovu.

Ndio inakuja point hakuna jema wala baya machoni pa muumba.
 
Kwa pointi yako kama kuna kila jamii ina mungu wake sawa. But ukikonsider kwamba kuna mungu mmoja muumba wa jamii zote ata kama zina miungu yao ndipo utakapoona point yangu.
 
Yaan anajua kila kitu chako kama utachange na kama hautachange hapo freewill ipo wapi
Kujua kwa jambo kuna kuzuia nini weww kufanya unachotaka ? Shida yenu wote wanao pinga hii "free will" hawaonyeshi uhusiano wa kujua na kufanya matendo.

Katika Uislamu kuna baadhi ya makundi yalikuwa yanaitwa Jahmiyah na Jabriyah, hawa walikuwa wanajinasibu ya kuwa wao ni Waislamu, katika istilahi ya Kiislamu tunaziita "Firaq" hawa katika itikadi zao walikuwa wanasema au kuamini ya kuwa "Mwanadamu hana uhuru wa kuchagua, yaani ni kama vile ua au jani linalo au lililo pulizwa na upepo" lakini wote walio kuwa na imani hiyo hawaonyeshi popote uhusiano wa kujua na ufanyaji matendo. Hili ni tatizo la kulazimisha mambo na kutofikiria mambo kwa undani.
 
Je siku ya kuhukumiwa mimi nitakua najifahamu kua ndio mimi? (Kumbuka roho ndio inabeba taarifa zako zote/kwenye roho
Nakubaliana na wewe hakika hapa ndo pana utata. Mi nadhani hutajitambua kabisa kwa sababu hutakumbuka kabisa ya duniani. Mind inaikomind brain kufanya vitu. Na kumbukumbu zipo kwa brain zimetunzwa. Wanasayansi walishadhibitisha ubongo ndio unaotunza kumbukumbu. Ni baada ya jamaa mmoja kupoteza sehemu ya ubungo wake katika ajali, ikawa kuna vitu anakumbuka ila vingine hakumbuki kabisa.

Ila tumetoka mbali sana ni karne ya juzi tu hapa watu wa kisomo walikuwa wakidhania moyo ndo unatunza kumbukumbu.
 
fre will is illusion

Ambao mnadhania kuna free will mnijibu haya.

- wapi ulichagua kuzaliwa, unafikiri ungepewa nafasi ya kuchagua ungechagua kuzaliwa maxingira uliyopo. Why ulikuwa walia ulivyozaliwa tu

- wapi ulichagua kuwa muumini wa dini unayoabudu. Jee wazazi wako wangekuwa dini tofauti na yako uliyonayo sasa hivi, ungekuwa na dini hii unafikiri?

- kwa wale walio na magonjwa ya kurithi, hivi kuna sehemu walichagua kuwa nayo au the whole sequence of events was predetermined from moment their parents fall in love to moment they conceive.
 

Hoja zako nzito mkuu
 
Em kaa the soma thread yako kama anajua kila kitu had utakavo kufa freewill ipo wapi
Freewill ipo kwenye uhuru tuliopewa wa kufanya maamuzi ya ama kuwa wema ama wabaya.

Kwamba, Mungu hatakaa aingilie uhuru wa uamuzi wote unaoufanya mpaka utakapokufa.

Amekupa mamlaka ya kujichagulia hatma yako - uwe mwema ama mbaya.
 
Hatukupata wokovu kwa Kristu alisalitiwa na Yuda; tulipata wokovu kwa kuwa Kristu alijitoa mzimamzima bila kujibakiza hata umauti msalabani.

Kumbe; hata kama asingesalitiwa na Yuda bado Wayahudi wangemkamata tu, walishajipanga.

Kama waliweza kumsulubisha bila kuwa na ushahidi wa kweli, wangeshindwa vipi kumkamata bila hata ya usaliti wa Yuda?

Hata Maandiko yaliyotimizwa na usaliti wa Yuda bado hayakumtaja Yuda kama msaliti.

Kwahiyo, Yuda aliamua mwenyewe kwa uhuru wake kuwa msaliti. Hakupangiwa wala kulazimishwa na yeyote.
 
We live in the universe of 'duality'

Good|bad, juu|chini, kulia|kushoto, ukweli|uongo
MUNGU | SHETANI

Ili ulimwengu uwe balanced ilibidi MUNGU amuumbe shetani
Kwa hiyo Mungu alidhamiria kabisa kumuumba Shetani ili kuleta balance, sasa kwa nini shetani alaumiwe wakati kumbe yeye aliumbwa ahamasishe ubaya ili alete balance?
Hiyo simulizi ya haki, kweli na huruma inapatikana wapi kwenye biblia (au kitabu kingine cha dini) ili nami nikaisome kabla sijajibu hoja...

Kuna tofauti Kati ya dhambi na nakosa.Ukifanya dhambi MUNGU hawezi kukuona maana ni mtakatikfu ,ndy maana Adam alipokula tunda, MUNGU hakumuona Adam ndy maana akauliza "Adam uko wapi"
Mbona wakati wana wa Israel walipikuwa wanatenda hiyo iitwayo dhambi alikuwa anaona na alikuwa akikasirika sana?
Vipi kuhusu Daudi kuzini na mke wa mwanajeshi wake na utamu ukamkolea akaamua asuke mpango wa kumuua huyo mjeshi ili amchukue kabisa mke wa huyo jamaa mbona alimuona hadi akamtuma nabii kwenda kumweleza ni jinsi gani yeye (Mungu) amekasirika...?
Mnona kaini alipomuua nduguye Abeli alimuona?
 
Safi sana, safi sana umereinforce point moja ilikuwa inapelekea watu kumuona Mungu isivyo. Kumuona kama vile yeye ndio anaye'dictate' hali zetu huku duniani. Wakati kumbe ni matokeo ya chaguzi zetu wenyewe ndiyo tunajiumbia dunia zetu.

Mtu akisoma kwa bidii na akaelewa kinamna fulani yeye mwenyewe mwisho wake atapata ufaulu fulani sambamba na alivyofanyafanya. Yaani ni kama automatically hivi.

Pia hata kuishi baadaye katika ufalme wa mbingu au ufalme wa shetani inawezekana hakuna kiumbe kutoka nje kinachokuja kukuambia wewe nenda huku au nenda kule. La!. Itakuwa ni mtu mwenyewe tu mfano akijifanya mbinafsi mwovu mwishoni atachaguachagua hadi kujikuta na washirika wenzie wenye tabia hizo baada ya kufa. Ukizungukwa na watu wabinafsi na waovu mara nyingi inamaanisha 'hell' hata kama upo wapi. Fikiria wewe uwe tajiri sehemu iliyozagaa 'ma-panya road' je utafaidi?

Lakini pia fikiria mfano ukafanya fikira na maamuzi yako ya kijamaa/communal ukapenda ushirikiano na upendo usio wa kibinafsi, upendo wa kimungu. Halafu mwishoni ukajitengenezea uhusiano wa karibu na marafiki wa namna hiyo mkajikuta wote baada ya kufa mpo katika dunia yenye watu wenye utashi huru/freewill lakini wote mna maamuzi ya kiupendo kwa kila mmoja wenu. Ndugu yangu hiyo mojakwa moja ndiyo tafsiri ya kuuishi ufalme wa mbinguni. Fikiria labda mazingira ambapo hata nyumba yako imebomolewa na upepo ukiwa haupo upo safarini, utarudi na utakuta vyombo vyako vi salama [tena hata kukuta wamekurekebishia wanakijiji!] Na siku nyingine ikimtokea mwingine wewe na wanakijiji wenzio mtashirikiana kumjengea 'victim mpya'. So kazi zitaendelea, hakuna kupumzika mbinguni wala jehanamu, lakini kwa mbinguni zitaleta raha mno kuzishiriki maana ni za upendo.

Kwa hiyo hata kama Scars alivyopendekeza kuwa na mbinguni napo tutaendelea na kuhustle kinamna fulani afahamu utofauti mkubwa uliopo kati ya; watu wanaohustle kati ya mijitu mibinafsi, na wanaohustle kati ya watu waupendo kuna utofauti mkubwa sana mfano wa hell and heaven figuratively and literally too! Kila mtu kutokana na namna anyoiona sahihi anajielekeza anakokupenda mwenyewe. Mungu anajua kuwa njia ya upendo ni nzuri, ila mwanadamu akimsisitizia kwamba njia ya ubinafsi ndio yenyewe sasa. Akajitia u-much-know basi Mungu humruhusu aendage huko maana ndiko atakakofaidi kwa mujibu wake yeye mwanadamu. Huo ni upendo mkuu sana!

Upendo ni pale unao uwezo na utashi kufanya lolote, lakini unaamua kutumia uwezo huo kwa uamuzi huru wako kuyafanya matakwa/mapenzi ya yule unayempenda. Mungu anatupenda sana mazee
 
Mkuu pole kwa swali kubwa hilo
Kipindi nipo shule nilikuwa na rafiki yangu niliwahi muuliza swali hili na swali jingne la kufikirisha sana ambalo nmekuja pata majibu yake baadabya kusoma mwanzo mpaka ufunuo mara ya kwanza na kurudia tena. Pia kupata wasaha wa kusikiliza mitizamo ya waru mbali mbali na kuunganisha na biblia na visa vya wana wa Mungu mbal mbali.

Mkuu Mungu alipotuumba alijua hatma ya kila mmoja na alitoa karama kwa kila alio wake. Unaweza niuliza mbona wengne ni walevi hawana hata lolote? Karama na talanta nying tulizopewa tumeruhusu ziibiwe ama kuharibiwa na wachafuzi hasa hao wachawi na washirikina.

Ila kilamtu Mungu kampa kipawa chake. Swala zima la hatma yetu ni kuwa Mungu katupa uwezo wa kutambua mema na mabayana kaleta wajumbe wake waje kutuhubiria kuhusu uwepo wake na nn asichotaka toka kwetu pia nn anataka.

Freewill ndo inabaki kwetu wenyewee kuwa tushike yale yake anayosema na wajumbe wake wanatushuhudia kufanya au tupotoke na twende upotevuni. Baadhi ya mambo lazma yatokee ili utukufu wa Mungu udhihirike.
 
Kwa pointi yako kama kuna kila jamii ina mungu wake sawa. But ukikonsider kwamba kuna mungu mmoja muumba wa jamii zote ata kama zina miungu yao ndipo utakapoona point yangu.
Hapana.

Hoja yangu ni kuwa, wema (goodness) ama uovu (evilness) wa kitu unapimwa kwa ku-refer mafundisho na maelekezo ya Mungu kwa jambo husika.

Kitu kuwa sahihi (right) au kikosefu (wrong) inategemea tu na interpretation ya jamii husika. Tunaita maadili.

Siyo kila kitu kilicho sahihi ni chema ama si kila kilicho na makosa kwa jamii husika ni kiovu, nitakupa mfano.

Kwa jamii nyingi za Wazungu sasa hivi ushoga ni kitu sahihi (kwa mtazamo wa jamii zao); lakini je, ushoga ni kitu chema mbele ya Mungu? Hapana, ushoga ni uovu, ni dhambi.

Mfano wa pili; wanawake kuvaa suruali kwa jamii zetu za Kiafrika hutafsiriwa kama makosa. Lakini, ni amri gani ya Mungu inavunjwa wakivaa suruali?

Summarily; japokuwa ushoga ni kitu sahihi (right) kwa jamii nyingi za Wazungu lakini ni kitu kiovu mbele ya Mungu. Japo wanawake kuvaa suruali ni makosa kwa jamii nyingi za Kiafrika lakini siyo kitu kiovu mbele ya Mungu.

Mungu ni mmoja na ndio maana kitu chema ni chema tu kwa jamii zote na kiovu ni kiovu tu kwa jamii zote.

Kitu kuwa sahihi au kosa mbele ya jamii husika hakihusiani moja kwa moja na interpretation ya jamii husika kuwa njema ama ovu.

Si maadili yote ni mema, mengine ni maovu.

I humbly rest my case.
 
Hapana, dhana ya freewill ni uthibitisho wa uwezo wa Mungu (omnipotence); kwamba ana nguvu na mamlaka yote ya kufanya chochote, hata kutupa uhuru kamili wa kujiamulia hatma zetu.
Twende taratibu..
Mungu anajua yote, sivyo.?
Hii inamaanisha kuwa ana uwezo wa kuona yote kabla hata hayo yote hayajaanza kutokea.

Kabla mimi sijazaliwa alishajua kuwa mimi nitakuwaje kwa kuwa yeye ajua yote, then huo utashi huru nautoa wapi wakati mimi naishi kile ambacho kilionekana kabla ya hata mimi kuwapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…