God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Nakubaliana na wewe,
Kabisa
 
Hii kitu nilikuwa natafakari Sana, isome yote,


kama Mungu anajua mwisho wa dunia katika mtiririko wote, ni dhahiri kuwa atakuwa anajua pia mwanzo na mwisho wa kila mwanadamu katika mtiririko wote…


ikiwa na maana kuwa anajua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa, ni yupi ataingia mbinguni na ni yupi hataingia mbinguni siku ya mwisho…


Na kama anayajua hayo ni dhahiri kuwa ni yeye huyo huyo ndiye anayechagua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa..Kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema “Hakuna awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenipeleka (Yohana 6:44)”.


Kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndiye anayemvuta mtu kwa MUNGU na sio mtu mwenyewe anayejipeleka kwa Mungu.
 
Hapa nafikiria Kila mwanadamu ana lessons zake lazima apitie .
 
Kwanini Mungu aliumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya kufanyika?
Kwa sababu ya upendo kaka.

Mungu anatupenda sisi na ndiyo maana ameruhusu tuweze kufanya maamuzi kulingana na mapenzi yetu. Ametuamini tuna uwezo wa kufanua maamuzi mema na anatupenda.

Maamuzi hayo muda mwingine yanakuwa ni yenye makosa [mabaya] na ndiyo maana husamehe na kutupatia muda wa rehema kuyaelewa kupitia matokeo yake na mwishoni kuyatubu[change of mind] hayo makosa.

Ikiwa angeweka kusiwezekane kufanyika kitu kinyume na mapenzi yake basi tungesema anatumia tu uwezo/power yake na sio upendo. Lakini kwa kutusikiliza sisi matakwa yetu anatupa mfano wa matumizi mazuri ya nguvu/uwezo/ujuzi/power.

Power is best expressed through LOVE

Kufanya mtu afe ghafla baada ya kuwaza kutenda dhambi sio upendo ni uwezo/power. Kufanya mtu afanye unachotaka tu hata kama hapendi [yaani hata kama unaamini ni kizuri kwake] bado sio upendo ni uwezo.

Wazazi hutumia uwezo kwa watoto wadogo maana bado hawajauamini utashi wao upo na ujinga mwingi. Ila watoto wakikua upendo ndiyo hutawala maana utashi umeshabalansi.

Mungu ametutrain kupitia mitume na manabii na hadi sasa ameshatuamini. Tusimuangushe
 
Kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndiye anayemvuta mtu kwa MUNGU na sio mtu mwenyewe anayejipeleka kwa Mungu.
Sahihi kuwa Roho wa Mungu ndiye anayevuta watu waende kwa Mungu.

Pia ni ukweli kwamba Mungu hana upendeleo

Hivyo Roho wa Mungu anawavuta watu wote wenye akili timamu kwa Mungu.

Wenye kukubali wanaitikia, wenye kukataa wanaitikia.

Mvuto upo kwa kila mtu, baada ya kuja Masihi sheria ya Mungu iliandika katika kila moyo. Inabaki utashi wako tu kukubali au kukataa!
 
Safi kabisa ,
 
Kijana mpaka najiuliza kwanini hujibu swlai langu ? Swali langu linakutaka wewe uonyeshe mafungamano kati ya kupangiwa jambo, Mola kujua na uhuru wako wa kufanya hayo mambo.

Mola amekuoangia jambo fulani, Mola anajua jambo fulani ila hajakushurutisha wewe ufanye jambo hilo, ndiyo maana ukapewa utashi na akili, na uwezo kufanya jambo na kutolifanya.
 
Wewe unapofanya mambo yako kwa uhuru inamaanisha sisi wengine hatupo huru?

Mungu anatumia uhuru wake kufanya mema, sisi nasi tunatumia uhuru wetu kadiri tupendavyo.

Kila mmoja anashinda mechi zake.
Nakufuatalia na nakuelewa mkuu, Kongole sana. Sasa kwanin uwezo wa kuamua kati ya mtu na mtu unatofautiana, yaan utakuta mtu mmoja ana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko mwingine, huon hapa Mungu aliweka bias kweny kufanya maamuzi sahihi na ambayo sio sahihi kwa kutofautisha uwezo wetu wa kufikiri? Huon hawa aliowapa uwezo mkubwa wa kufikiri unawakandamiza walio wa uwezo mdogo wa kufikiri? Kwanin Mungu hakuumba watu wote tuwa na utashi, akili na ufahamu sawa?
 
Uwezo wa kufanya uovu na ubaya amenipa Mungu, sio? Mimi kufanya uovu ni matokeo ya kushindwa kufanya mema kutokana na vichocheo vya ubaya kuzidi ndani yangu, sasa nani aliniumba hivi? Kwanin aruhusu vichocheo vya ubaya kuzid wema ndani yangu? Utasema mim ndo nimechagua, Kwanin nimechagua ni kwasababu ya udhaifu uliopo ndani yangu ambao Mungu ameniumbia nao, kwanin aniwekee mtego huu?
 
You are using evil to produce good huh?

Alishindwa kuwa na upendo ambao ungefanya yafanyike mazuri bila ubaya?

Umejenga hoja ya mabaya kwa kuangalia maamuzi, vipi na yale mabaya ynayofanyika bila maamuzi ya watu kama matetemeko, yanayouwa hadi watoto wadio na hatia?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio wezekana hayo yote kutokea?
 
Swali, kama Mungu alijua huyu ninayemuumba ataenda moton, na moton ataenda kwa kuchagua yeye mwenyew lakin uchaguzi wake ndo huo aende moton, sasa kwanin aniumbe nikateseke wakat yeye anajua kabisa naenda moton maana anajua mwsho wangu kabla ya mwanzo?
 
Nishakujibu

Hakuna cha utashi what seems to be utashi is just an illusion though you may experience a freedom lakini in reality everything has been predetermined and you have no freewill to choose otherwise
 
Watu waliokwisha amini kuwa kuna mambo ya kiroho hawatishwi na dhoruba za kimwili kwa kiwango unachotishwa wewe nikwambie. Wanayo Imani na amani pia.

Labda wewe utachukulia mtu kufa katika tetemeko ni jambo baya kuliko vyote kwa kuwa umeamini hapa duniani ndiyo kila kitu. Na uhai huu ndio kila kitu. Sio hivyo.

Kwa kuwa Mungu anapenda tuuexperience upendo na utashi kama tu yeye alivyo ndiyo maana katuumbia huu ulimwengu. Na kingine hapangiwi kaamua kaona huu ni mzuri kwetu kwa upendo kabisa
 
The same kwa mtu asiye amini Mungu hawezi tishwa na habari za jehanamu

Ila hapa tunajadili yale ambayo yanaleta madhara kwa watu wote hata wasio amini habari za roho

Mtu asiyeamini na anayeamini wote hawapendi kukutwa na mabaya kama hayo

Ingekuwa mabaya hayo sio tishio basi tusingeona hata wanaoamini katika roho wakifanya jitihada za kuhangaika namna ya kuepuka hayo mabaya kwasababu washajua kua hata wakipatwa na hayo mabaya watakua na extra time huko mbeleni.

Kwa hiyo swali langu bado hujajibu

Ikiwa mabaya yapo kwasababu ya uamuzi wa mtu, ilikuwaje Mungu akashindwa kuumba ulimwengu ambao viumbe wangeweza kuchagua yaliyo mema (kama ufafunuzi wako wa freewill unaohusisha mema pekee)

Kwanini Mungu hakuumba ulimwngu huo?

Na pia sio kweli kuwa kila baya linalifanyika linatokana na maamuzi yetu, mafuriko, natural calamities kwa ujumla wake husababisha maafa makubwa massively

Kivipi mabaya hayo yameweza kutokea licha ya kwamba hayajatokea kupitia maamuzi yetu?
 
Na pia sio kweli kuwa kila baya linalifanyika linatokana na maamuzi yetu, mafuriko, natural calamities kwa ujumla wake husababisha maafa makubwa massively

Kivipi mabaya hayo yameweza kutokea licha ya kwamba hayajatokea kupitia maamuzi yetu?
Ndio sio kweli kutokana na kwamba tupo wengi na maamuzi yanafanuwa na watu wengi sio wewe binafsi pekee. Kukiwa na upendo na mshikamano hata hayo unayoyaita mabaya ya asili sio ya kusikitikiwa kihivyo. Ndiyo maana nikakuambia ili tupate experience mbalimbali kulingana na maamuzi yetu tujirudi kisha tutubu [tubadili fikra zetu].

Wanajeshi wanaokabiliana na adui huwa na furaha ya ajabu hata kama wenzao wanakufa. Ni feeling fulani nzuri sana kujua kuwa kuishi kwako na kufa kwako na kwa wengine ni katika upendo kwa wote. Hata majanga na kifo yana tafsiri tofauti jamii za kidunia zikiunganishwa na kuongezewa upendo katika kupambana na 'common enemy'

Kufurahi pamoja, kusikitika pamoja ni furaha hata kama sio raha. Endelea kushangaa na kulabel vitu kuwa vibaaaaya. Kama hutaki kuuona uzuri ndiyo. Tunasema kusudi la yote hayo ni jema hata kama wewe kwa wakati huo huelewi.

Mfano huu mfano niliupata kwa concept ya Mcqueenen alisema watu walipogundua moto ndio wakaweza kupika na kusapoti bongo kubwa zaidi kwa kuwa chakula kilichopikwa kinatokeza nishati zaidi.

Sasa ukichukulia labda sehemu kupigwa na baridi kali ni kitu kiovu, sehemu ikapigwa na baridi kali ukasema ni baya limetokea. Kumbe ndani yake kuna kusudi la kuwafundisha watu watafute moto na walishe chakula bora bongo zao. Watakaokataa kutumia akili kutumia moto automatically watakufa watapotea kwa ubishi wao. Ila waliobaki wataishi katika dunia iliyojaa watu wanaopenda kutumia bongo zao zaidi.

Au ukichukulia kuliwa na simba ni kitu kiovu bila maamuzi ya mliwa. Lakini angalia raha atakazozipata mtu atakayeweza kujenga mfumo wa asibugudhiwe na simba tena. Nyumba imara. Matumizi ya moto. Kutokutembea tena maporini na kubugudhi viumbe!

The earth is a training ground. Strengteningnground. Ukibaki na hiyo notion yako ya kutaka Mungu atufanyie kila kitu kisa ana uwezo ukaitafsiri kuwa na wewe uwafanyie kila kitu wanao kisa una uwezo jiandae kupata kizazi cha hovyo. Kuwakinga watoto na dhoruba ndogondogo hata zile za kuwajenga hayo ni mapenzi at best na sio upendo. Na inawatesa baadhi yao hawataweza kuexperience raha jata kama wataishi rahani maana hawaijui shida.

Unajua sifuri ndiyo inaanza na moja ni ya pili? -Songa
 

Safi Sana
 
Utetezi wako ume contains logical fallacy kama attempt yaku fabricate hoja ionekane factual

Mabaya yanayotokea bila kuamuliwa na mtu umetumia red herring fallacy kuyafanya yasionekane mabaya na kwamba ni mambo ya kawaida yasiyopaswa kuwa considered kama mabaya

Matetemeko, vimbunga, tsunami, nk. hayo ni mabaya ambayo yanafanyika bila watu kuamua yafanyike

Ikiwa kila baya linalotendeka hutokana na maamuzi ya watu, mfano mtu kamsababishia mwenzake kufa hilo tunaweza kuliweka katika matokeo ya uamuzi wa mtu

Lakini vipi kwa matsunami yanayoua maelfu na kuacha watu wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na watu wao wapendwa wakiwemo watoto wasio na hatia?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya kama hayo hayawezi kutokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…