God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mimi nimetokana na uumbaji wa mamlaka iliyo kuu, ambaye ni Mungu Mkuu muumba wa ulimwengu na vitu vyote viujazavyo.
kwa namna ulimwengu ulivyopangiliwa na kwa jinsi mimi mwanadamu nilivyoumbwa kwa jinsi ya ajabu ambayo ni ya kimiujiza nikakuthibitishia kwamba kuna mamlaka kuu iliyofanya haya ambayo ndo inaitwa Mungu.
Cha kushangaza unakuja na mifano irrelevant kuhusianisha hili swala na mtoto wa miezi 6 hawezi kuzaa mtu wa miaka 30 na sijui square root ya 2 haiwezi kuwa 10.......
kifupi you have refuted uwepo wa Mungu bila uthibitisho wowote. Na nikikwambia ueleze wewe umetokana na uweza upi na uthibitishe hilo kama unavyotaka mimi nithibitishe uwepo wa Mungu, unarukaruka kama mahindi yaliyo kwenye kikaango.
Mfano irrelevant wakati mimi ndiye nimekueleza swali lako irrelevant?

Umekubali kwamba naweza kujua kwamba jibu hili si sahihi bila kujua jibu sahihi?
 
Binafsi nime

shukuru kwa ubishi wao maana nimejifunza mengi na kurekebisha mengi kiasi kwamba kama nitaamua kuandika upya mada inayohusiana na freewill basi nitaiandika kwa ufasaha zaidi.

Utashi huru ni moja kati ya topic ilonivutiaga nikaandika katika blog

Mwanzo niliandika kwa kutumia neno utashi huru/freewill kumbe kiuhalisia nilielezea zaidi utashi pekeyake yaani will. Sasa nikija kuandika FREEWILL PART2 nitakuwa nimetenganisha vizuri will na free-will asanteni akina Kiranga Kisai Scars , hasa Scars maana ndiye tumeinteract naye zaidi.

Ipo hapa kuhusu will na ukiweza ingia na kwenye blog[kuna link katika thread] iliyoandika kwa ureeefu [kuhusu hiyohiyo will] Mbinu ya kutumia akili na utashi binafsi kuiendesha afya na mwili wako - A biological appeal to free-will
Mtu ambaye hana hata control ya mawazo yanayotokea kichwani kwake anawezaje kuwa na free will?
 
Nenda kwenye ule uzi utuonyeshe namna ya kusali na kutoa zaka toka kwenye Qur'aan.

Hili mpaka unakufa, huwezi kujibu.
Hahahaha, koijana nakupa darsa, kwanza uelewe salat imeanzia wapi, umeelewa sasa? Au bado?

Ulikuwa unaelewa kuwa Qur'an imebainisha salat ilipoanzia?

Unakumbuka nilikupa ayat zinazufundisha nyakati za salat? Usisahau hilo.

Halafu nilikuuliza kule unataka kuelewa sala ipi?

Yote umeshindwa hata kujaribu au kukiri tu, sas kabala sijakujibu ujuha wako, natumai umeelewa lakini kabala sijakufafanulia salat zaidi, nakuuliza unaelewa maana ya neno "salat" ni nini? Na unaelewa kwaninoi una sali?

Hayo maswali ukishindwa kuyajibu hapa, ntayahamishia na kule na kwengone, mpaka utie akili.

Qur'an itakuchambulia salat mpaka utaielewa kama likuwa huielewi.

Unataka kushindana na Allah? Yaani wewe binadam aliyekuumba uijuwe sala kuliko Allah?

Unakufuru za ajabu wewe.
 
Mtu ambaye hana hata control ya mawazo yanayotokea kichwani kwake anawezaje kuwa na free will?
Watu wa neuroscience wamefanya majaribio na kuonesha kuwa ubongo na hata misuli huwa inaandaliwa kwa 'action' kabla lile wazo halijafika kwenye 'conscious' brain! Hisia zipo haraka zaidi.

Wanatumia hiyo kuipinga free -will.

Mimi hiyo niliiacha kwenye will binafsi ya huyo mtu[japo mwanzo nilitumia nenofreewill] maana naamini kwamba huyo mtu amejengwa na uzoefu wote alionao hadi kufikia muda huo anafanya maamuzi.

Anayetetemeka [bila kujiamurisha] akimuona nyoka [mfano chatu mdogo] porini ni matokeo ya anachokijua yeye kuhusu nyoka wapoje hadi muda huo. Kwa hiyo ntasema 'ameamua' kutetemeka sababu ni hatari [kwake]. Ni will yake inafanya kazi.

Lakini mtaalamu wa wanyamapori yeye atarelax sababu anachokijua hadi saa hiyo ni kuwa chatu hana sumu, na hako kadogo hakawezi kummeza. So 'ameamua' kurelax na kumshika. Ni will yake inafanya kazi.

Kuwa free au kutokuwa free itategemea na kitu kimoja kwamba. Je? wakati anafanya hayo maamuzi alikuwa na taarifa za upande wa pili? Je alizin'gamua? akachagua A or B? So sio watu wote duniani hufanya mambo yote kwa utashi huru kila wakati, mda mwingine tunachagua kiotomati
 
Sidhani kama ni exclusive hivyo. Kwani mtu hawezi kusema: Kwa hichi nilichothibitisha, nimeamini mwamba ni noma.

Sense haikatai hata babalai...
Hiyo ni illogic, katumia neno kimazoea lakini sio kwa usahihi kama inavyotakiwa

Ukisha thibitisha hauwi na imani
 
Watu wa neuroscience wamefanya majaribio na kuonesha kuwa ubongo na hata misuli huwa inaandaliwa kwa 'action' kabla lile wazo halijafika kwenye 'conscious' brain! Hisia zipo haraka zaidi.

Wanatumia hiyo kuipinga free -will.

Mimi hiyo niliiacha kwenye will binafsi ya huyo mtu[japo mwanzo nilitumia nenofreewill] maana naamini kwamba huyo mtu amejengwa na uzoefu wote alionao hadi kufikia muda huo anafanya maamuzi.

Anayetetemeka [bila kujiamurisha] akimuona nyoka [mfano chatu mdogo] porini ni matokeo ya anachokijua yeye kuhusu nyoka wapoje hadi muda huo. Kwa hiyo ntasema 'ameamua' kutetemeka sababu ni hatari [kwake]. Ni will yake inafanya kazi.

Lakini mtaalamu wa wanyamapori yeye atarelax sababu anachokijua hadi saa hiyo ni kuwa chatu hana sumu, na hako kadogo hakawezi kummeza. So 'ameamua' kurelax na kumshika. Ni will yake inafanya kazi.

Kuwa free au kutokuwa free itategemea na kitu kimoja kwamba. Je? wakati anafanya hayo maamuzi alikuwa na taarifa za upande wa pili? Je alizin'gamua? akachagua A or B? So sio watu wote duniani hufanya mambo yote kwa utashi huru kila wakati, mda mwingine tunachagua kiotomati
Hata hapo, huyo mtu anaweza kuwa hana uhuru wa kuamua akutane na nyoka au asikutane na nyoka.

Sasa hapo ana freewill gani wakati muda wowote anaweza kukutana na nyoka bila kupanga wala kutaka?

Kama mtu hachagui anazaliwa nchi gani, na wazazi gani, ana genetic makeup gani, hachagui hata kama azaliwe au asizaliwe.

Huyo utasemaje ana freewill?
 
Hiyo ni illogic, katumia neno kimazoea lakini sio kwa usahihi kama inavyotakiwa

Ukisha thibitisha hauwi na imani
Imani ni neno moja tu kiswahili ila kingereza kina maneno mengi na mengine yanaendana na uthibitisho kabisa mfano; belief [haina uthibitisho] ila trust [ina uthibitisho]. Mfano nika sema faith yenyewe iko na balanced uthibitisho na hamna uthibitisho.

Kuna mengine kama hope pia see bro uthibitisho unaweza kuwepo na imani ikawepo pia kwa wakati mmoja.
 
Hata hapo, huyo mtu anaweza kuwa hana uhuru wa kuamua akutane na nyoka au asikutane na nyoka.

Sasa hapo ana freewill gani wakati muda wowote anaweza kukutana na nyoka bila kupanga wala kutaka?

Kama mtu hachagui anazaliwa nchi gani, na wazazi gani, ana genetic makeup gani, hachagui hata kama azaliwe au asizaliwe.

Huyo utasemaje ana freewill?
Ana mengi tu aliyochagua hadi njia ya kupita, muda wa jua kali. Yaani inapotokea tukio fulani jua kabisa kwamba vimehusika vyote; nguvu za Mungu na nguvu za mtu na nguvu za malaika na nguvu za shetani kila kitu. Vyote vimeinteract hadi kulileta tukio kila mmoja ni mchezaji.

We, all of us make things happen
 
Imani ni neno moja tu kiswahili ila kingereza kina maneno mengi na mengine yanaendana na uthibitisho kabisa mfano; belief [haina uthibitisho] ila trust [ina uthibitisho]. Mfano nika sema faith yenyewe iko na balanced uthibitisho na hamna uthibitisho.

Kuna mengine kama hope pia see bro uthibitisho unaweza kuwepo na imani ikawepo pia kwa wakati mmoja.
Naelewa hilo na hata humu kuna mada nilishawahi kuzungumzia kuhusiana na hilo

Kuna faith, trust na belive

Hayo maneno yote katika lugha ya mkswahili yana maana moja "imani" ila katika tafsiri na kimatumizi ndio hapo utofauti unapokuja

"Watanzania wana imani na samia" hii ni statement inayoonesha watu kuwa na confidence na mtu mwingine haihusiani na mambo yajayo ambayo unatarajia kuyaona kama ulivyo ya amini/kuyafikiria

Hiyo ni mada ambayo tushawahi ijadili sana humu sikunbuki tu ni uzi gani
 
Ana mengi tu aliyochagua hadi njia ya kupita, muda wa jua kali. Yaani inapotokea tukio fulani jua kabisa kwamba vimehusika vyote; nguvu za Mungu na nguvu za mtu na nguvu za malaika na nguvu za shetani kila kitu. Vyote vimeinteract hadi kulileta tukio kila mmoja ni mchezaji.

We, all of us make things happen
Nakwambia hivi, kama hata hakuchagua tarehe aliyozaliwa, hakuchagua njia aliyopita.

Maana hiyo njia amepita kwa sababu kwa bahati alizaliwa na kuikuta njia ipo.

Angezaliwa kabla njia haijajengwa asingeweza kupita.

Unaweza kufikiri "nimechagua kusoma shule ya Tambaza". Kumbe umeweza kuchagua kwa sababu umezaliwa tarehe fulani, ungezaliwa na kuishi maisha yako yote kabla shule ya Tambaza haijajengwa, usingeweza kuchagua shule ya Tambaza.

Kwa hivyo, kama hujachagua tarehe ya kuzaliwa kwako, hujaweza kuchagua kingine chochote kwa namna ambayo ni significant.
 
Jielimishe kwanza kabla ya kubishana.

Kiingereza unajua lakini? Maana haya mengine hayajapata kuandikwa Kiswahili bado.

Cause and effect is no longer fundamental, it is only so to people who do not know the most basic things about quantum physics. Like you.
Kiingereza sijui, nisaidie kuniwekea kwa Kiswahili kisha nimalizs mjadala.

Haya mambo ya Quantum si halisi ni dhana za Wanasayansi wa kileo katila kujaribu kuelezea mambo ambayo akili imeshindwa kuyadiriki, sisi huwa tunaziita "Ngano na uongo wa Wanasayansi"

Ulitakiwa ujibu hoja yangu kwa wepesi sana, huko kwenye hizo link ingebaki kwa maelezo zaidi, ila siyo kwa kuelezea msingi wa hoja. Ulitakiwa kabla ya kujenga hoja au kujadiliana ujifunze adabu za kufanya mijadala ya kielimu.

Kisha katika kujenga hoja zako uweke na mifano ili jambo liwe wazi zaidi
 
Naelewa hilo na hata humu kuna mada nilishawahi kuzungumzia kuhusiana na hilo

Kuna faith, trust na belive

Hayo maneno yote katika lugha ya mkswahili yana maana moja "imani" ila katika tafsiri na kimatumizi ndio hapo utofauti unapokuja

"Watanzania wana imani na samia" hii ni statement inayoonesha watu kuwa na confidence na mtu mwingine haihusiani na mambo yajayo ambayo unatarajia kuyaona kama ulivyo ya amini/kuyafikiria

Hiyo ni mada ambayo tushawahi ijadili sana humu sikunbuki tu ni uzi gani
Basi tuweke mambo sawa hapa;

Kama ulihisi imani yangu ni belief kwa wingi nakataa. Mimi imani yangu mara nyingi ni trust na faith najua mambo mengi tu yanayosapoti vitu ninavyoviamini.
 
Hahahaha, koijana nakupa darsa, kwanza uelewe salat imeanzia wapi, umeelewa sasa? Au bado?

Ulikuwa unaelewa kuwa Qur'an imebainisha salat ilipoanzia?

Unakumbuka nilikupa ayat zinazufundisha nyakati za salat? Usisahau hilo.

Halafu nilikuuliza kule unataka kuelewa sala ipi?

Yote umeshindwa hata kujaribu au kukiri tu, sas kabala sijakujibu ujuha wako, natumai umeelewa lakini kabala sijakufafanulia salat zaidi, nakuuliza unaelewa maana ya neno "salat" ni nini? Na unaelewa kwaninoi una sali?

Hayo maswali ukishindwa kuyajibu hapa, ntayahamishia na kule na kwengone, mpaka utie akili.

Qur'an itakuchambulia salat mpaka utaielewa kama likuwa huielewi.

Unataka kushindana na Allah? Yaani wewe binadam aliyekuumba uijuwe sala kuliko Allah?

Unakufuru za ajabu wewe.
Bi mkubwa punguza stori na dibaji naona husogei mbele kila siku uko pale pale na msaada nilikupa. Hili swali huwezi kulijibu, sasa endelea kujipotezea umri wako bure. Katika hili huna cha kunipa sababu nimekutangulia umbali mrefu sana.
 
Basi tuweke mambo sawa hapa;

Kama ulihisi imani yangu ni belief kwa wingi nakataa. Mimi imani yangu mara nyingi ni trust na faith najua mambo mengi tu yanayosapoti vitu ninavyoviamini.
Kwa bahati mbaya mambo ya kiroho yahusuyo Mungu nk hutumika faith
 
Nakwambia hivi, kama hata hakuchagua tarehe aliyozaliwa, hakuchagua njia aliyopita.

Maana hiyo njia amepita kwa sababu kwa bahati alizaliwa na kuikuta njia ipo.

Angezaliwa kabla njia haijajengwa asingeweza kupita.

Unaweza kufikiri "nimechagua kusoma shule ya Tambaza". Kumbe umeweza kuchagua kwa sababu umezaliwa tarehe fulani, ungezaliwa na kuishi maisha yako yote kabla shule ya Tambaza haijajengwa, usingeweza kuchagua shule ya Tambaza.

Kwa hivyo, kama hujachagua tarehe ya kuzaliwa kwako, hujaweza kuchagua kingine chochote kwa namna ambayo ni significant.
Labda wewe unaikataa freewill kwa sababu tu hujawahi kuiexperience? Au uliiexperience halafu akaja mjinga mmoja akakuambia shtuka brooo hiyo ni illusion, ukamuamini.

Niliiexperience freewill kwa mfano wakati nilipokuwa nachagua kuwa wa Mungu au kumkataa. Muda huo nilikuwa na taarifa za kutosha kusapoti yupo na nilikuwa na taarifa za kutosha kusapoti hayupo! Nilwahi kuishi wiki kadhaa nikiwa na imani kuwa hizi ni stori tu

Ningeamua kuwa hayupo ningeendelea kuishi hivyo na ningekuwa sane vizuri tu na mwisho ningekufa sambamba na imani yangu hiyo.
Ningeamua[na nilishaamua] kuwa yupo na ninaishi sanely kabisa kulingana na imani hiyo mwisho nitaishi sambamba na imani yangu
Jambo ambalo halikuwezekana ni vyote viwili[ mutually exclusive] kwa hiyo nilikaa chini kisha freely nikachagua upande. FREE - WILLL
 
Kwa bahati mbaya mambo ya kiroho yahusuyo Mungu nk hutumika faith
Yas na haiishii hapo, maana kwa walio kiroho hadi haya mambo physical ni sehemu ya uthibitisho wa mambo hayo ya kiroho. So tunazo data nyingi sana tunazozitrust na zinazidi kutuongezea kwenye faith yetu
 
Usitumie kilichopo, kinacho thibitishika kuwa kipo kuwa ndio uthibitisho wa kitu kingine ambacho hujakithibitisha

Hiyo ni logical fallacy
 
Back
Top Bottom