Goli la Yanga dhidi ya Mamelodi mzozo ni mkubwa South Africa kuliko Tanzania, CAF inapoteza credibility

Goli la Yanga dhidi ya Mamelodi mzozo ni mkubwa South Africa kuliko Tanzania, CAF inapoteza credibility

Usiseme matokeo hayawezi kubadilika, Yanga wanapeleka malalamiko ya match fixing Mamelody anaondolewa Yanga wanapewa ushindi. Inawezekana kabisa without a doubt
Achana na motivational speakers je kitu kama hiki kilitokea lini ?
Unaikumbuka fainali iliyoleta vurugu ya Esperance Vs Wydad Casablanca ? Kama ile fainali haikurudiwa ndio irudiwe mechi ya Yanga ?
 
Huyo mpira una uangaliaga peke yako? Wacha urongo wewe. Ni mara ngapi tunashuhudia marefa wanaenda kuhakikisha kama it was a clear goal or not
Mechi ipi labda refa alienda kuangalia kama goli limevuka mstari, tutajie hapa tuangalie
 
Iwe upande wako saafi, siku ikigeuka inaumiza Roho. Basi ndio walimwengu.
 
Achana na motivational speakers je kitu kama hiki kilitokea lini ?
Unaikumbuka fainali iliyoleta vurugu ya Esperance Vs Wydad Casablanca ? Kama ile fainali haikurudiwa ndio irudiwe mechi ya Yanga ?
Sijasema mechi irudiwe nimesema Mamelody washitakiwe for match fixing then waondolewe mashindanoni Yanga wapite
 
Gumzo linaloendelea hapa South Africa kwenye mitandao ni kwamba Yanga ndio wameshinda mechi lakini Mamelodi ndio walionufaika.

Nikiweka ushabiki wangu pembeni Mimi huwa napenda Sana kujifunza Vitu nisivyovijuwa.

South Africa wapinzani ni Chiefs na Orlando, lakini ukiwafuatilia vizuri unakuta wote wameungana kumshutumu Motsepe na kuilaani Mamelodi.

Inshort Ile Support ambayo kocha wa Mamelodi amelalamika haipati sasa ndio hatoipata kabisa hasa Kwa Wazulu wa Johannesburg, mechi za nusu fainali good option wakacheze Cape town watapata full support Kwa sababu Cape town hizi mechi za Champions league timu za Cape town hazina ubavu wa kutobowa.

Mashabiki wengi wa South Africa wanauza, kama refa alikwenda kuangalia VAR ili ampe Kadi nyekundu Lomalisa, NI Kwa nini hakwenda kuangalia VAR kuhusu goli?

Ushauri wangu Yanga watume malalamiko rasmi CAF, refa aadhibiwe hizo pesa za Motsepe ndio ajikimu nazi, ila matokeo ya uwanjani huwa hayabadirishwi na Mimi si muumini wa ushindi wa mezani.

Yanga ndio Wahindi ila Mamelodi wamenufaika.

Sisi siyo milimani, Al Kisasi hakhi.
Na ni vema zaidi Yanga wahamie SA ili wakutane na waungane na wanaoipinga Masandawana ili kuongeza nguvu.
 
Hata mimi nilishangaa kapteni kutomzonga refa kidogo kumlazimisha aende kutama yeye mwenyewe...
Kapteni wa Yanga anazifahamu fika sheria za matumizi ya VAR ndio maana hakumzonga refa
 
Yanga wakate rufaa haraka sana CAF, refa kanunuliwa wazi wazi, lile ni goli la wazi
 
Katika kuangalia kwangu mpira nilishangaa refa kukataa lile goli maana hata kabla ya VAR mpira ulivyogonga ndani na kutoka nje unaonyesha kabisa mpira uliingia ndani ila refa hakutaka kabisa kufatilia marudio ya VAR daah rushwa ni mbaya sana jamaa wananunua wachezaji wa gharama na wanatoa rushwa ili wapate makombe...
Nyerere aliona mbali kukemea rushwa

Rushwa ni adui wa haki rushwa inaumiza sana moyo

Moyo wangu umeumia sana tukio la jana
 
Katika kuangalia kwangu mpira nilishangaa refa kukataa lile goli maana hata kabla ya VAR mpira ulivyogonga ndani na kutoka nje unaonyesha kabisa mpira uliingia ndani ila refa hakutaka kabisa kufatilia marudio ya VAR daah rushwa ni mbaya sana jamaa wananunua wachezaji wa gharama na wanatoa rushwa ili wapate makombe...
Kama ambavyo timu flani hapa nyumbani zinanunua wachezaji kwa gharama kubwa halafu zinatoa rushwa kwa waamuzi.
 
Sijasema mechi irudiwe nimesema Mamelody washitakiwe for match fixing then waondolewe mashindanoni Yanga wapite
Okay hapo ushahidi wa match fixing umeutoa wapi ?
Kama ile mechi tena fainali VAR ilizimwa watu wakanyimwa goli, ikatokea vurugu mpaka mechi ikaishia pale pale hawakusema match fixing ndio iwe hii ?
 
Back
Top Bottom