GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

Naona Kuna watu wanaleta utetezi kwa hoja zisizokuwa na ushahidi, nimeleta tuhuma hizi hapa ili mamlaka izifanyie kazi kwa kuwa GPSA imekuwa kichaka cha watu flani kupiga pesa za umma huku mamlaka zikiwa Kama zimewasahau.

Sina chuki na Hawa watu na wala Sina maslahi binafsi ndani ya taasisi na Kama yapo basi uchunguzi na hatua zichukuliwe, tunatoa hapa ili kuonesha mamlaka ni namna gani wameisahau hii taasisi kiasi kwamba viongozi wake kila anaekuja anaona ni fursa kapata ya kupiga pesa chini ya Engineer wa upigaji Bw. Malik Aram ambaye ni DBSS.

Bado naandaaa taarifa zingine sahihi na nitaziweka hapa kurahisisha mamlaka kufanya kazi yao, japo kwa taarifa za uhakika,Sasa wanafanya kazi ya kuficha na kurekebisha documents zenye Ufisadi lakini najua hili halitasaidia maana ukweli siku zote huwa unajulikana.

Wanaosema Kuna maslahi yangu/yetu yameguswa wanapaswa kusema ni maslahi gani hayo yalikuwa yanaathiri taasisi na mimi nitajwe niliyekuwa nayafanya ili kuweka ushahidi sawa badala ya kutumia nguvu nyingi kupinga kwa porojo. Hapa tunamsaidia raisi magufuli kujua wahujumu wake maana vyombo vya ukaguzi vilivyopewa mamlaka ya kufichua haya maovu vinanunulika...najua hapa ataona

N:B
Kuna mda nakuwa sijibu message kwa sababu ya kubanwa na majukumu mengine
 
Mkuu frame19. endelea kumwaga nyepenyepe tunakusubili
 
Nakumbuka kuna section kwenye employment standards ya ELRA -kama sikosei S.28 inakataza deduction of any kind ya mshahara wa mtumishi unless under written law na mfanyakazi akikubali inabidi a-provide express agreement, hii nyie ilikuwaje mkakatwa bila makubaliano yenu?
 
Subili wanakuja
 
Ni kweli unachosema, na ndio maana hata mimi nimeuliza kwamba wamewezaje kuingilia mishahara yetu bila idhini yetu?
Pamoja na hayo baadhi yetu tumeandika barua ya kupinga makato haya kupitia kwenye mishahara yetu bali wakate kwenye posho zingine tunazopewa kiofisi, mpaka leo hatujajibiwa na bado tunaendelea kukatwa.
hii jeuri sielewi wanapata wapi ya kuingilia mishahara yetu?.... Ikiendelea kuwa hivi kuna siku tunaweza kukuta tumekatwa mishahara ili kuchangia Birthday au harusi ya kiongozi wa taasisi...VERY STUPID MIND
 
Hao viongozi wenu sidhani kama ufikiri wao uko sawasawa
 
Uki google utapata majibu yote..tumia akili kidogo
 
nilimuulizaga bosi mmoja kwa nini anaiba huku anapokea 14m akasema ...sababu ana majukumu makubwa pia
 
na ufisadi wote huo mtashindwa kuwanunua hao mbuzi wa siejii
 
Point. Na Mimi nilitegemea Kama Kuna ufisadi wowote CAG angeuona.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jambo limenishangaza kidogo, kwa nini wafanyakazi wote wa GPSA nilioongea nao wanaonekana kufurahia hili jambo, Yaani wanaona Kama mleta mada ni mkombozi wao...hapa simuamini mtu ila kwa maelezo yao inaonekana Kuna shida....Hawa jamaa sisi ni wateja wao hasa kwenye Vifaa vya stationary
 
Cute umetisha! salute kwako!
 
Hawa jama wamejipanga sana....mi nilishawavuliaga kofia miaka mingi....huwezi kuwakuta kwenye ripoti ya CAG hata siku moja pamoja na maangamizi wanayoyafanya
 
Hawa jama wamejipanga sana....mi nilishawavuliaga kofia miaka mingi....huwezi kuwakuta kwenye ripoti ya CAG hata siku moja pamoja na maangamizi wanayoyafanya
Inawezekana ni Kama jamaa alivyosema hao juu kwamba, wanahonga..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…