TANZIA Grivas Mwangoka afariki dunia kwa ajali ya Gari

TANZIA Grivas Mwangoka afariki dunia kwa ajali ya Gari

Seems ni uchovu na mwendo mkali. Yaani kama umechoka aiseee park lala kwa muda then amsha mashine kama kawaida. Usingizi una mambo ya kipuuzi sana yaani unadhani uko ON kumbe brain ilishafunga mawasiliano muda mrefu sana. Hadi kuichakaza hio gari hivyo hio speed haikua ya dunia hii
Hili jambo waweza kudhani ni jambo dogo lakini hapana aise...usingizi ni hatari na hauna hodi.
 
Quality ya gari zinauzwa uku Africa zikiwa mpya huwa quality yake iko chini sana kulinganisha na na magari yanayouzwa kwenye nchi za wenzetu wanaofatilia quality za gari. Safety, security, body strength etc. Ni bora ununuwe mtumba wa gari toka Europe or America utapata quality nzuri.
Hyo nadharia tu,lakini product Ni ile Ile.... sababu kampuni Ni hyo hyo,teknolojia Ni hyo hyo,sema location ndo tofauti ..Sasa hv Kuna scania G series special edition for Africa,inatengenezwa south Africa,watumiaji wanasema hzo Ni nzuri kuliko za uingereza

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni kweli kabisa..... Kuna siku nilikua naendesha gari usiku wa manane kumbe nimesinzia nikajikuta niko upande wa pili wa barabara niliogopa sn nikapaki gari nikalala (HIKI NI KISA CHANGU CHA KWELI KABISA=
Na kulala si mpaka uwepo eneo rafiki?.

Nimewahi kukutana na hiyo situation na ilikuwa mchana maana nilidamka saa 9 alfajiri by saa kumi nikang'oa.

Mida ya nane hivi mchana kumbe kausingizi kalininyemelea...ghafla nilikurupuka nikahisi nimeshakula mzinga, kutoka hapo mikono na miguu ilipoteza nguvu, roho inadunda....nikaanza kuutafuta mji, maana ni highway na ni pori sidhani kama ingekuwa busara kupaki popote na kulala....nikafika kwenye Mji nikaingia Motel moja, nikavunga kama nimefata msosi nikarudi garini nikaupiga kama saa nzima hivi.
 
Sina hakika na hili mkuu ila MWANGOKA ni ukoo mkubwa sn.....
Okay sawa, hata hivyo wakina Mwangoka wa Majengo wameonesha kutomfahamu...

Itakuwa huyu ni wa ukoo mwingine tu
 
... na hasa ukute walikuwa na ligi barabarani; hakuna anayetaka kushindwa; kuoneshana umwamba. Nina Ranger utanipitaje na "matako ya nyani"; ukikutana na obstacle however small it is, hayo ndio majibu yake sawia - huchomoki! Tunalaumu sana tochi ila sometimes zinasadia ku--save life; tycoon huyu angekuwa ameokoa maisha yake na wote wanaomtegemena - familia, wafanyakazi, etc.
Death comes to us all. You can't escape it. Inaweza isiwe leo au kesho au keshokutwa ila kifo kipo tu. It's part of life.
 
ujue kuna wakati unashangaa na kujiuliza inakuaje watu wanapata ajali, ila yakikukuta ndio utajua, Ajali inakuwa sekunde chache na kukuacha mzima, mahututi, au maiti... Tuendesheni tu magari ila likiamua kukufanyia maajabu, utafurahi mwenyewe...
 
Back
Top Bottom