Wewe kama wewe hauna tatizo , don’t ever doubt yourself. Tatizo ni namna sio mtu, na hapa ni dogo tu , huwa unafanya U-Jecha, unakuja na matokeo yako mfukoni.
Pia jifunze kanuni za mjadala, na soma kiasi kuhusu mantiki, Kuna kanuni za mjadala ukizivunja hazina madhara sana, ila zingine ukizivunja unavuruga inakuwa hakuna sababu ya kuendelea kujadili na mtu husika, wakukuelekeza watakuelekeza, wengine watakuignore tu sababu wataconclude mambo fulani fulani.
ukishazifahamu kanuni za mjadala ongeza kuifahamu content yako (Kama wewe ndiye mleta mada) Kama wewe ni mchangiaji sio lazima ufahamu sana content iliyopo mezani unaweza kuwa critic kwa njia ya maswali, again hata ukiuliza lazima uulize kwa mantiki.
Unamuona mtu kama Natafuta ajira, zamani tulikuwa tunampinga sana akileta mada, unafahamu kwanini? Alikuwa bado yuko shallow kwa mada zake, kuna makosa ya wazi alikuwa anafanya au alikuwa anayafanya makusudi (manipulative) Lakini siku hizi weeeee! Akiandika bandiko hapa utatafuta pakupinga utapakosa, unafahamu nini kimebadilika? Amesoma, amepitia maandiko mengi au amekuwa more observant kwa area yake ya specialization (mi naiita sayansi ya mahusiano, au sayansi ya tabia) Hili ndilo hapo juu nimeliita kuifahamu content yako.
Kingine, ukileta data lazima uwe unazifahamu kanuni za data, ukileta rejea lazima ujue hiyo rejea imepingwa na wangapi huko ilipofanyika, it’s whole a lot of a sport kwahiyo kuwa mjanja, lete mjadala huru halafu rejea watu wakazisome huko duniani ili mtu mwenyewe akapambane na maandiko elfu huko yanayozungumzia kitu kimoja kama anajali(Kuna mahali Denno alinibana nilete data, nilikataa nilikuwa nafahamu exactly ninachokifanya, lakini hapo hapo kwenye huo mjadala Kuna mtu simkumbuki alileta data/rejea, baadae Binti wa zamani akaja akaandika kuna mtu ana trigger a researcher in her, nilimuelewa sana anachomaanisha, alimaanisha hiyo rejea iliyoletwa ilishapingwa au kukataliwa na watafiti wa mbele😅😅)
Kingine; lazima uwe na lengo la kujiingange kwenye mjadala, Kama ni kujifunza kama ulivyosema lazima uzingatie hayo hapo juu, ila kama ni kuchangamsha genge, kukera watu, kugaslit watu you can argue anyhow utakuwa umekosea lakini si kitu JF sio sehemu serious ki vile it’s just an online platform and we use fake IDs…
Humu kuna watu ni wajinga na mi nawapenda, unajua kwanini? Mtu anakuwa sio mjinga per se, inakuwa sio lazima watu muda wote wawe na akili wajadili kama wapo TLS.
Ngoja nikutie moyo, Ukiacha watu waliosoma filosofia kama somo , basi watu wengi tumejifunza kujadili humu, Kiranga watu wengi hawampendi wanamuona ni mbishi 😅 Lakini amini nakwambia huwa anafuata kanuni zote za mjadala na mantiki….. Na kuna mtu mwingine nimemuona hapa simtaji atajikuta sana 🤣 Nimemtaja Kiranga sababu anakumbukika kwa urahisi na watu wengine wengi wa zamani wanajua sana.
La mwisho si kwa umuhimu, wana sayansi wengi hawajui kujadili, someone tell me why…na hii haimaanishi hawana akili, wana akili sana ndio maana ni wana sayansi , some of them are geniuses. We can’t reduce them to this, Kwahiyo sometimes mi sioni kama ni issue kubwa mtu akiwa hajui kujadili, Tbh.
No one is perfect, tunajifunza na shule haiishi. ukiona mtu anasoma na kulike tu either anajifunza au anaburudika na maandishi ya humu.