Gwajima akisema CHADEMA wapewe 'minimum reforms' anatuambia CCM ni wenye hati milki ya Katiba na kuwaamulia vyama vingine wapewe nini, kwa kiasi gani?

Gwajima akisema CHADEMA wapewe 'minimum reforms' anatuambia CCM ni wenye hati milki ya Katiba na kuwaamulia vyama vingine wapewe nini, kwa kiasi gani?

Kwa muda mfupi nilidhani Gwajima ni mtu mwenye busara na uwezo wa kutafakari mambo. Lakini kwa hii Press Conference yake nimemtoa tena kwenye watu wenye hekima.

Bila aibu kabisa anasema CCM iwape Chadema minimum reforms na kuwaruhusu waingie kwenye uchaguzi. Ni aibu sana mtu kama Gwajima kuongea utopolo kama huu. Nadhani hii Press Conference yake lengo lake ilikuwa kujipendekeza tena kwa Samia na CCM kwa ujumla.

Gwajima anapaswa kuelewa Chadema wanapodai Reforms, hawaombi huruma ya CCM, na sio juu ya CCM kuamua Chadema wapewe kiasi gani cha reforms. Gwajima anafikiri CCM ni nani katika nchi hii, wenye hati miliki ya Katiba ya Tanzania?

Hivi tunawezaje kuwa na viongozi wenye kufikiria kwa level ya kijinga kiasi hiki?

Chadema hawajadai Reforms za Katiba ya CCM, na taratibu za uchaguzi sio mali ya CCM, ni za Watanzania. Chadema wanadai kitu ambacho ni kwa faida ya Watanzania wote, vyama vyote vya siasa. Kwa hiyo sio juu ya CCM kusema "tuwape Chadema minimum reforms". Who do you think you guys are, gods of Tanzania? Huu ujinga wa kujiona nyie ndio wenye nchi umewaingia sana kichwani hadi mnajisahau kabisa.

Hivi mnataka Watanzania wafanye nini hasa ndio mjue wako serious, wapindue nchi?
Kwahiyo wewe hadi saizi hulijui hilo??
Inabidi ufanyiwe surgery ya ubongo wako
 
_/ Tuwape Reform kidooogo afu Tuwapige""" 😃 hapa nikaona heheeee niyale yale tu hamna kitu
 
Kwahyo kwenye yooote hili pekee ndio umeokota mkuu!!
Vipi kuhusu hili la mamlaka ya raisi na freedom ya vyombo vya Dola 🤔

Hujaona kabisa kama ni kitu?
Leo Gwajima kuzungumza kwa sura tatu
1.Kama mzalendo anayetizama maslah ya taifa na sio chama chochote cha siasa

2. Kapandikiza roho za mapinduzi kwenye vyombo vyote vya dola, na kuwafanya wajitafakari upya.....
maana kawapromis uhuru na true power ndani ya nchi
(Kwa lugha fupi hii n shifting of power kutoka taasisi ya uraisi na kugawanyika sehemu 3 zisizotegemeana!!!
Maana nyingine n kuwa nchi itakuwa na raisi zaidi ya mmoja japo mmoja ndio atakuwa public announced,,,, hapo kutakuwa na nidhamu✍️

3.Gwajima pia n binaadam na anawatu wanamtizama, kwahyo itakuwa n ujinga kurisk maslah ya wapendwa wako kisa ukweli mchungu

(Kwahyo n lazima angetoa kauli za suluhu na CCM maana ndio wapo kwenye dola
Ndio sabb umeona pamoja na kuzungumza yote kunasehem kalegeza kidogo ili kujihakikishia usalama wake na watu wake baada ya kuzungumza huu ukweli mchungu.

Hapa alichofanya n kuchonganisha baina ya wazalendo wa kweli katika taifa na wanufaikaji wa mfumo ulipo (genge la wahuni alilomaanisha Mr Slow... halafu kakaa zake pembeni asome mchezo!!

Kiufupi jamaa Leo katumia akili kubwa sana.. yaani kabalance element zote tatu zinazosumbua kwa sasa na kaweka solution


Upinzani wakimsikiliza wanaridhika na speech 50%
CCM wakiskiliza wanaridhika 35%
Wazalendo wakimsikiliza wanaridhika 100%

Kwahyo deal done: Nadhani lengo la speech ya Leo lilikuwa n kwaajili ya hao wazalendo wa kweli katika taifa ndio maana katumia muda mwingi kuwaelezea.
Gwajima n level nyingine kabisa🚶🚶
Kabisa
 
Kwanza kabisa, Gwajima anaweza kuonekana ni mtu mwenye busara kwa sababu Watanzania wana low standards na short memory tu.

This is not to rubbish everything he says or take the side he opposes, this is just an observation on your opening sentence.
Na anaonekanaje kwa wenye high standard?
 
Gwajima kujipambanua kama mbabaishaji kama kilivyo chama chake. Anazungumzia katiba ya CCM kama kwamba ndiyo iliyo juu ya katiba na Sheria za nchi. Reforms zinatakiwa zifanyike kwa ukamilifu wake!!. Baada ya madai ya Reforms za Tume huru ya uchaguzi kinachofuata ni madai ya Katiba Mpya. #NoreformsNoelection
 
Back
Top Bottom