Mtu asie na utaalam wa mambo ya afya na utabibu(Bishop Gwajima) anauliza maswali kuhusu chanjo, mtaalam wa afya na utabibu MD na waziri wa afya badala ajibu maswali kitaalam ana amua kumshambulia personally muuliza maswali.
Hapa weledi wa waziri uko wapi? Kuna majibu mawili tu unapata ukifikiria majibu ya waziri kwa bishop. Haijui corona wala chanjo zake na anachokifanya ni kwenda tu na script.
Hamna wakati Antony Fauci alipitia wakati mgumu kama kipindi maambukizi yako kwenye peak USA ila hamna wakati huyu mtaalam aliwashambulia personally wauliza maswali.
Waziri wetu uswahili unamzidi hadi anapitiliza miiko na maadili ya kazi yake.
Mi nimuulize maswali mtaalam mmoja JF kuhusu mambo nisiyoyaelewa hapa jukwaani halafu badala anijibu kitaalam aanze kunishambulia kuhusu user name yangu, avatar, muda niliojiunga JF, aina ya mada nazovutiwa kuchangia nk! Si utoto kabisa?