Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

Ngigana nakuunga mkono 100℅, kunawatu wanakalili maandiko eti 7×70, Mungu mwenyewe mpaka Leo kashindwa kumsamehe Shetani , je Yesu nae alimsamehe Yuda Iskariote? Nabii Musa naye akatembeza mapanga kwa waabudu ndama woote 3000.Makonda aweke vyeti mezani .Wametusumbua sanaa hawa jamaa kwenye uhakiki wa vyeti sinahata hamu nao!

Mbona Makonda kumradhi, Daudi Bashite, alipokuwa akidhalilisha Wamama na wafanyakazi wa Jiji hakuambiwa 7x70? Mimi nasema apigwe tu na Atapigwa apotee maana hakuna jinsi nyingine.
 
Najua Mchungaji Josephat Gwajima upo hapa JF.
Tumepata taarifa jumapili ijayo kuna wageni watatoka Kolomije village kuja kuongea na familiya ya wana Ufufuo,tumesikia wengine ni waalimu waliomfundisha Mh Makonda na wengine ni wanakijiji.

Naomba nikuombe neno moja,samehe na kusahau kwa kuwa ndio tulioitiwa,waendao katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu,wewe ni mtu mkubwa katika jamii na unaheshimika,hivi unaweza kufundisha somo la kumsamehe adui yako?

Naomba uwe mfano wa kuigwa ili usipoteze kondoo unao waongoza,kumbuka maneno ya Yesu,akulazimishae kutembea maili moja tembea nae mbili,na akuny,ang,anyae koti mwachie na shati.
Yesu alipopigwa HAKUTISHA
Alipoudhiwa ALINYAMAZA KIMYA
Alipotemewa mate. HAKURUDISHA neno
Alipoulizwa ADHIHIRISHE kama yeye ni MWANA wa Mungu, akajibu "WEWE UMESEMA". "Ufalme wangu SI wa dunia HII".
Akiwa msalabani wale WALIOMSULUBISHA aliwaombea BABA WASAMEHE maana HAWAJUI nini wandendalo.
Yesu akasema Mti HUTAMBULIKA kwa matunda yake.
MTAWATAMBUA kwa MATUNDA YAO!
 
sawa namuomba mungu anipe uzima nicheki hii kitu mpaka mwisho
 
Kuna Nyakati Hata Binadamu Anachukizwa Na Visa Vya Watu Waovu, Kama Ni Kweli Makonda Alitumia Vyeti Vya Kughushi Na Akapata Nafasi Anayoitumia Kufanya Uovu Kwa Watu Hivyo Anastahili Kukemewa Kwa Kauli Moja Na Watu Wote Wenye Mapenzi Mema Na Imani Kwa Mungu.

Pia Wachungaji Wana Nafsi Kama Binadamu Wa Kawaida, Na Shambulio La Mchungaji Ni Shambulio La Kanisa. Hata Yesu Akiwafundisha Watumishi Wake Somo La Imani Kupitia Pale Alipoona Njaa Wakati Anaelekea Mjini (Bethania) Akaona Mti Kando Ya Njia Akauendea Na Asione Kitu Juu Yake Ila Majani Tu Akakemea Yasipatikane Matunda Kwako Tangi Leo Hata Milele. Mti Ukanyauka Mara.

Kwa Tafsiri Rahisi Yesu Alitegemea Matunda Kwenye Mti Ule Na Alipokuta Hamna Kitu Akashikwa Na Hasira Akakemea Mti. Lakini Akatumia Kitendo Kile Kufundisha Imani. Sasa Makonda Anafundishwa Nguvu Za Wachungaji Ili Atambue Nguvu Ya Imani Kwa Mungu Aliye Mkuu Asiwe Anapenda Kuchafua Makanisa Kwa Manufaa Yake Binafsi.

Hata Yesu Alipatwa Na Hasira Pale Ekalu La Bwana Lilipogeuzwa Soko Watu Wakawa Wanafanya Biashara, Yasiyo Ya Haki na Wizi. Ndiyo Maana Aliwafukuza Pale Si Mahali Pake Pa Kufanya Mambo Yale. Hata Makonda Ile Ofisi Aliyopewa Ni Kwa Huduma Wala Si Visasi Na Kuweka Watu Polisi Kiholela Holela Tu. Mamlaka Na Ofisi ZaSerikali Lazima Ziheshimiwe
Asante kwa mchango SAAAAAFFIIIII
 
Gwajima anawatetea wanyonge wasioweza kujitetea walionewa na bashite
 
Unajua nyie Gwajima fanboys mnachekesha sana.

Mpaka sasa hamna ushahidi wowote ule juu ya tuhuma mnazozishabikia.

Mnasukumwa na hisia tu. Chochote kijitokezacho ambacho kwenye akili zenu mnaona kinammulika vibaya Makonda basi mnaruka ruka tu kama vikinda vya sungura.

Sasa hivi chochote atachoropoka Gwajima mnameza tu. Hakuna cha kuhoji wala kuuliza.

Sasa wewe hapa eti nawe unakuja kunihoji kama nilimkanya Makonda...nimkanye kwani mi babake?

Endeleeni ni huo ujinga wenu wa kishabiki.

Wewe huoni kwamba jibu lako ni lakishabiki. Unauhakika na unachokisema?
 
Aisee, Gwajima anakosea sana kwa kuitunishia serikali misuli kwa mwamvuli wa Kanisa, Biblia na U-askofu wake.

Unaelewa, huwa naandika hapa JF kwa kifupi sana wakati mwingine wenye akili wanaelewa ila waliokwisha jazwa upupu wa dini za kigeni zote huwa hawaelewi.

Mfano, Manji aliitunishia sana misuli serikali siku nyingi sana mfano, mwaka 2005 katika serikali ya awamu ya nne (4) juu ya NSSF deal na Ufukwe na kila mtanzania mwenye nia safi kwa Watanzania alielewa kabisa kuwa Manji anaelekea kukwaa jabali sasa hivi habari yake kwisha kabisa.

Sasa, Gwajima naye anaelekea uelekeo ule ule wa Manji.

"No matter he is a bishop or he calls himself as a Bishop, Dr. or whoever he calls himself!

A state will never accept 'the opium of people' to distabilize the fight against drugs and drug lords" The interests of the state always will prevail no matter what it cost to be attained!
For further details refer: Carl Max and Realism Theory By David.

"Time is a Good' Teacher"

anaitunishia serikali au anafundisha Bashite mipaka yake. Viongozi muingu inatengenezwa na fikra kama hizo. Hamna anabishia vita dhidi ya madawa ya kulevya
 
gwajima nachafua dhana ya viongozi wa dini na haswa haswa [HASHTAG]#wachungaji[/HASHTAG] ...... mchungaji kama gwajima ni bure kabisa

Ngoja nikupe somo la msamaha. Msamaha unagawanyika katika sehemu mbili, yaani kusamehe (to forgive) na kupatana (reconciliation). Kupatana ina vitu viwili ndani yake, huo masamaha (forgiveness) na toba (penance). Bila toba hakuna kupatana na hilo hata mungu analikubali. Toba ni nini? Mtu akikuibia, msamehe, lakini kama hajutii, haoni kosa lake, hajirekebishi, hamna reconciliation - yaani hamna kupatana. Mfukuze kazi. Toba au penance kwa mhalifu ni kama kifungo, kwa mtoto mdogo ni kuchapwa nk. Haizekani mtu anafanya uhalifu wewe unaachilia tu. Utageuzwa fala. Atarudia tena. Bashite sisi WOTE tunamsamehe lakini lazima atoe "penance" yake. Akubali kosa ajiuzulu ili tupatane. Achapwe ajifunze alafu tupatane nae otherwise Ma-Bashite wengine wataendelea kufhadisha wanyonge. Baba Gwajima wasaidie wanyonge, msamehe Bashite lakini endelea na zoezi ili toba ipatikane. Kwani muendesha mashitaka wa serikali hawezi kwenda mbinguni kwa kutafuta haki? Bwana asifiwe!
 
Haina namna acha Bashite afundishwe adabu na...... hufunzwa na ulimwengu Sasa Askofu gwajima Ni Mlimwengu acha afundishe.
 
[emoji125] [emoji125] dini hapo iko wapi bana acha wafu wazike wafu wenzao[emoji241]
 
Hii issue ndogo inafanywa hii onekane kubwa Bashite inabidi amalize utata otokea hadhalani akanushe basi si vinginevyo tunajua awezi ku kubali jina lake licha furiwe vijana wa mitandaoni
 
Najua Mchungaji Josephat Gwajima upo hapa JF.
Tumepata taarifa jumapili ijayo kuna wageni watatoka Kolomije village kuja kuongea na familiya ya wana Ufufuo,tumesikia wengine ni waalimu waliomfundisha Mh Makonda na wengine ni wanakijiji.

Naomba nikuombe neno moja,samehe na kusahau kwa kuwa ndio tulioitiwa,waendao katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu,wewe ni mtu mkubwa katika jamii na unaheshimika,hivi unaweza kufundisha somo la kumsamehe adui yako?

Naomba uwe mfano wa kuigwa ili usipoteze kondoo unao waongoza,kumbuka maneno ya Yesu,akulazimishae kutembea maili moja tembea nae mbili,na akuny,ang,anyae koti mwachie na shati.
Gwajima ya Mungu mpe Mungu ya Kaisari mpe kaisari
 
Kweli kosa vyote ila usikose upeo.! Umeambiwa we ni shoga si mfungulie mashtaka alokuambia wewe shoga ili ukweli upatikane?! Sasa BASHITE kaambiwa aliprove EARTH IS SPHERE yaani aligonga FWE FWE zoote ila alitumia vyeti visivyo vyake sasa si ajitokeze aoneshe vyeti ili tujue ya kwamba GWAJIMA ni Askofu muongo na mzandiki asiye na haya.?!
Hapa ndo Faiza huwa anawaambia sijui huko shule mlienda kusomea ujinga.?!
Kati ya watu ambao huwa hawakurupuki ni Gwajima, Jamaa anaongeaga kwa fact saana.
 
Najua Mchungaji Josephat Gwajima upo hapa JF.
Tumepata taarifa jumapili ijayo kuna wageni watatoka Kolomije village kuja kuongea na familiya ya wana Ufufuo,tumesikia wengine ni waalimu waliomfundisha Mh Makonda na wengine ni wanakijiji.

Naomba nikuombe neno moja,samehe na kusahau kwa kuwa ndio tulioitiwa,waendao katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu,wewe ni mtu mkubwa katika jamii na unaheshimika,hivi unaweza kufundisha somo la kumsamehe adui yako?

Naomba uwe mfano wa kuigwa ili usipoteze kondoo unao waongoza,kumbuka maneno ya Yesu,akulazimishae kutembea maili moja tembea nae mbili,na akuny,ang,anyae koti mwachie na shati.

Gwajima hana kinyongo na Makonda, anachokifanya sasa ni kuuweka ukweli ambao utatuweka huru.

Go Gwajima Go
 
Jino kwa jino,hatutaki mambo kama ya yesu ukipigwa shavu ili et ugeuze na lingine.hiyo itakua ni funzo kwa wengine wafanye kazi kwa weledi,sio kuwapakazia watu.nae atulie,maana wakati anawataja watu mbele ya waandishi wa habari,tulikua tumetulia.
Kabisa mkuu, hata Yesu alisema apandacho mtu ndicho avunacho. Alichopanda Makonda ndicho atakachokwenda kuvuna. Amen!
 
Back
Top Bottom