Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.
Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!
Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.
Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.
Kwaheri kuonana ni majaliwa.