Mkuu,
Kwanza pole sana kwa changamoto unazozipitia. Nakuelewa mimi. Kikawaida,japo maelezo hapa ni kama hayajitoshelezi,ila kuna haya:
1. Kiukweli mpaka CT-Scan, ni kwamba kuna tatizo.
2. Ili ifanyike hiyo CT-Scan au vipimo vya mashine hizo, lazima kuna daktari aliyekuandikia kufanya hivyo vipimo.
Mara zote iwe hiyo X-ray, Iwe CT-Scan, iwe MRI, Cd zinazotolewa huambatana na karatasi inayoripoti waliokupima wameona nini.
Hawa watu wanaokupima, ni watumiaji tu wa mashine hizo,hawawezi kamwe kuintapreti walichokiona na kumwambia mgonjwa. Wanaheshimu sana maagizo. Hivyo,unapopewa majibu,yanakuwa yamefungwa na hurudishwa kwa daktari alieomba vipimo hivyo tu.
Ikitokea hayupo karibu,huomba anaemfahamu mwenye uwezo wa kusoma na kuelewa.
Nadhani kutoka huko ulikozipata,iwe praiveti au hospitali ya serikali kwenda Muhimbili, ulipewa referal na ulitakiwa umuone either doctor fulani au uende kitengo furani na majibu yako,wakutengee doctor wa kuyasoma na kukusaidia.
Kama uliondoka na CD tu,bado unakosa ripoti inayoelezea ugonjwa wako,kwa sababu wengine akishasoma ile ripoti ataelewa tatizo lako hata asipocheza hiyo CD.
Kingine nachokiona hapa,hutaki kukili lakini ulikosea. Na kamwe usirudie au na mwingine asijaribu.
Wewe umesema kwamba hiyo CD kwenye computer inacheza. Ni kweli.
Ulijuaje inacheza?
Kwa sababu inapotoka sehemu kwenda sehemu nyingine,licha ya kuwa labda aliyekuandikia mara ya kwanza aliitazama,hawezi kukupa wazi wazi kuipeleka bila kufungwa,hiyo ni siri ya mgonjwa na ajuae ni daktari tu.
Labda yeye akwambie mwenyewe. Sasa,kuna uwezekano pia wa wao kuisusia baada ya kuona imeletwa katika mazingira yasiyo salama. Kama ulifungua,ulitakiwa uombe radhi na uahidi kutorudia.
Maana akisema ulipewa uwaletee,ukapeleka kwingine,ana point.
Harafu,kwa jazba ulonayo hapa,inaoekana huenda ulifika ukawagombeza. Na wale jamaa wana akili mbovu asikwambie mtu. Japo hupaswi kubembeleza tiba,inapobidi huna namna.
Mi nahisi haya makosa mawili ulifanya.
Japo sikumbuki vizuri,si lazima watu wa ICT waupload ndo aicheze,kama ana computer inayoisoma ni rahisi.
Changamoto ipo tu kwenye hizo gharama.
Nadhani ungeweka wazi kitengo,na waliotakiwa wafanye hivyo.
JF ina kila aina ya watu na si kwamba hili hawalioni. We elezea shida bila kupindisha maneno,nakuhakikishia utapata msaada tena haraka sana. Na kama ni kosa ulifanya,we jishushe uwe mkweli,wengine ni watu wazima wanaelewa ujana na maumivu,utasaidiwa